Walimu wa sayansi ajira mpya kuanza na mshahara mkubwa zaidi ya walio kazini. Je, utumishi kuna shida?

Ngoja nikueleweshe kwa lugha nyepesi.
Kwa ufupi tu mwalimu wa science ajira mpya mwenye degree anamzidi mwalimu wa science aliyeanza kazi 2014 kwa Tsh 30,000/=
Hiyo ndio tafauti ya D1 na D3
Kwaio mtu analalamikia 30,000? Duuuh
 
Ukiitwa kuthibitisha kwa hichi ulichoandika utaweza ? Tafakari ndugu.
Watu tunatumikia cheo kimoja miaka 7?. ilihali utaratibu upo wazi miaka 3!.. halafu nidiriki kusema tuna viongozi?.. UTOPOLO KABISA ,,mitano mingi tusomeni tu Albadiri
 
Kwenda kufanya yenu kwenye chaguzi...
Mnakosea sana, sio walimu wote ni CCM wako walimu wengi tu ni Chadema, Act na wengine hawana vyama kabisa.
Pia kwenye uchaguzi walimu sio wasimamizi peke yao kuna watu wengi wanasimamia sio walimu
 
Ajira mpya wenye shahada kwa walimu wa science wameanza na ngazi ya mshahara wa TGTS D3.
Wakati wale walio kazini tangia mwaka 2014 bado wako ngazi ya mshahara TGTS D1. Kwenye utumishi kwa kawaida mwenye uzoefu anatakiwa awe ngazi ya juu kuliko mgeni ila hii ya sasa hivi imekuwa pindua pindua.

Utumishi kuna shida gani?
Check nao?Mshahara ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa.Kama unaona mshahara hautoshi unaenda Private kutafuta maslahi kisha tunakukamata na kuifungia hadi hio shule ya Private
 
Faida yake ipo kwenye kikotoo utaona tofauti ya 30,000/= anakupiga gap la milioni hata 15 kwenye pension.
Hata ukiacha kikokotoo, ukiongezewa 10000 inakuwa imekusaidia parefu sana.
Nakumbuka effect ya kupunguzwa kwa PAYE ilivyotusaidia, ingawa iliongezwa kidogo tu. So hiyo 30000 ni very significant
 
Back
Top Bottom