Walimu wa sayansi ajira mpya kuanza na mshahara mkubwa zaidi ya walio kazini. Je, utumishi kuna shida?

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Ajira mpya wenye shahada kwa walimu wa science wameanza na ngazi ya mshahara wa TGTS D3.

Wakati wale walio kazini tangia mwaka 2014 bado wako ngazi ya mshahara TGTS D1. Kwenye utumishi kwa kawaida mwenye uzoefu anatakiwa awe ngazi ya juu kuliko mgeni ila hii ya sasa hivi imekuwa pindua pindua.

Utumishi kuna shida gani?
 
Vipi mkuu imekuuma sana eeh? Au hutaki watu wawe na kipato kizuri kumudu ukali wa maisha na gharama zake?
 
TGTS D4 ni shilingi ngapi? D1,D2,D3,D4 unajua wanapishana shilingi ngapi?.Mkuu tuache kwanza tuko na Vaccine huku Habari ya mishaara subiri kwanza, wangevushwa madaraja sawa ila kama madaraja ni yale Yale chapa kazi subiri daraja uende E.
 
Tofauti ni ndogo ila heri hafifu kuliko sifuri
 
Weka na bei yake yaani ni sawa na laki ngapi?
TGTS D4 ni shilingi ngapi? D1,D2,D3,D4 unajua wanapishana shilingi ngapi?.Mkuu tuache kwanza tuko na Vaccine huku Habari ya mishaara subiri kwanza, wangevushwa madaraja sawa ila kama madaraja ni yale Yale chapa kazi subiri daraja uende E.
 
Kawaida tu ila waturekebishie na sisi wazoefu

Nyinyi uzoefu wenu upo katika kuisaidia CCM kuiba kura wakati wa uchaguzi tu, So if you are not happy with salary you are getting, employ yourself or go to HELL and present this nonsensical claims. Mwalimu gani unawaonea wivu wa kishamba wenzio!!!
 
Jadilini mlio kwenye hizo ajira, wengine tupo tunawa-zoom tu alafu hata hatujui hayo maD1 ,D2,nk
 
Ajira mpya wenye shahada kwa walimu wa science wameanza na ngazi ya mshahara wa TGTS D3.
Wakati wale walio kazini tangia mwaka 2014 bado wako ngazi ya mshahara TGTS D1. Kwenye utumishi kwa kawaida mwenye uzoefu anatakiwa awe ngazi ya juu kuliko mgeni ila hii ya sasa hivi imekuwa pindua pindua.

Utumishi kuna shida gani?
Kama maelekezo yametoka mwaka huu, nyie hayatawahusu.

Usinichukie "law cannot act retrospective"
 
Nyinyi uzoefu wenu upo katika kuisaidia CCM kuiba kura wakati wa uchaguzi tu, So if you are not happy with salary you are getting, employ yourself or go to HELL and present this nonsensical claims. Mwalimu gani unawaonea wivu wa kishamba wenzio!!!
Unazijua taratibu za utumishi wa umma?
 
Kwani nchi hii ina uongozi?.. ina utopolo tu!.. KUANZIA Rais wao hadi madiwani wanabwabwaja tu ili waonekane kwa TV!.. soo stupid!.
Kuna vitu huwa vinafanyika mpaka unajiuliza uwezo wa kiakili wa watu wa wizarani
 
Jadilini mlio kwenye hizo ajira, wengine tupo tunawa-zoom tu alafu hata hatujui hayo maD1 ,D2,nk
Ngoja nikueleweshe kwa lugha nyepesi.
Kwa ufupi tu mwalimu wa science ajira mpya mwenye degree anamzidi mwalimu wa science aliyeanza kazi 2014 kwa Tsh 30,000/=
Hiyo ndio tafauti ya D1 na D3
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom