Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,861
Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mitaala ya elimu toleo la 2023 utaanza kwa awamu mwakani, huku walimu watakaofundisha shule ya msingi wakipaswa kuwa na stashahada ya ualimu.

Walimu na Wadai wa Elimu endeleeni kutoa maoni ya Sera Mpya ya Elimu,mchakato unaendelea kabla ya kuja na final.

Akiwasilisha rasimu za sera na mitaala hiyo kwenye semina ya wabunge jijini hapo, Kamishna wa Elimu Tanzania, Dk. Lyabwene Mtahabwa, alisema katika mapendekezo ya rasimu hizo, walimu watakaofundisha elimu ya msingi itakuwa lazima wawe na stashahada ya ualimu baada ya kumaliza kidato cha sita.

Alisema kwa watakaofundisha elimu ya sekondari, ni lazima wawe na shahada ya ualimu, hivyo walimu waliopo kazini ambao hawatokuwa na sifa hawataondolewa kwenye ajira bali watapewa fursa ya kujiendeleza ili kufikia viwango.

Akitoa ufafanuzi kwa wabunge, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema hakutokuwa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi badala yake kutakuwa na mtihani wa upimaji, ili kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya chini.

Chanzo: Nipashe
 
labda kwa intake mpya .

Ila wengi wapo mbali walioingia na cheti na experience inawabeba..
Haya ni maelezo Yako ila Kwa mujibu wa maelezo ya mtaalamu hapo Juu watapewa nafasi wajiendeleze..

Mimi.mzee wangu alikuwa Mwalimu wa UPE akiwa.mtu mzima.ilikuja.order ajiendeleze vinginevyo Ajira inakata na alilazimika kufanya mtihani wa form 4 na kusoma upya cheti ,saizi alishaga staafu.
 
Ni sahihi tena ingawa sio sahihi sana

Sasa hivi shule nyingi kwa wenzetu mfano Kenya, Uganda nk
Walimu wote kuanzia chekekechea wana digrii

Mfano Mwalimu wa Chekechea anatikiwa kuwa na Bachelor degree in Early Childhood Education, Mwalimu wa shule ya Msingi anatakiwa kuwa na degree in Primary Education na Sekondari anatakiwa kuwa na digrii In Secondary Education.Uzuri shule xa private zishaanza siku nyingi as usual private sector siku zote huwa mbele kuliko Public sector .Public sector inakumbuka shuka wakati kumekucha

Tanzania vyuo vyetu vikuu vinatoa degree zote hizol lakini wengi wanaenda shule.za.Private ndio.maana performance ya shule za Private kuanzia,chekechea,Msingi na sekondari ziko vizuri sana

Hata hivyo nipongeze wizara walau kwa kuanza taratibu lakini kwa huo mtaala mpya nadhani ingekuwa waanze kuajiri walimu pia wenye digrii za education za checheka,msingi na sekondari ili taratibu hl hao wa diploma wawe faced out taratibu hadi tufikie mahali digrii tupu ziwe zinafundisha shule xote kuanzia chekechea hadi sekondari
 
Kuufuta mtihani wa darasa la saba Professor Adolf Mkenda nimekupongeza na unazo sifa Za kujaza fomu 2025.

Huo mtihani ni kero, Gharama kubwa Za bure, usimbufu na ni eneo la maafisaelimu kupiga fedha Za Umma.

2. Walimu wenye diploma huko secondary warudishwe Msingi Ili kutoa mwanya kwa kuajiri wapya walimu wa sekondari wenye Degree

3. Walimu wenye cheti wapewe Muda wa miaka 2 kujiendeleza baada ya hapo wasioweza wapishe wenye diploma.

3. Baadhi ya shule Za sekondari Za kata ziwe shule Za ufundi Za kata.

3. Baadhi ya vyuo vikuu viondolewe kwenye mfumo Mfano arusha university, masomo yanayotolewa huko hayana faida kabisa kwa vijana wetu.

4. Baadhi ya Course zinazotolewa SUA ni mzigo na haxiendani na Soko la ajira zifutwe.
 
Ha
Ni sahihi tena ingawa sio sahihi sana

Sasa hivi shule nyingi kwa wenzetu mfano Kenya, Uganda nk
Walimu wote kuanzia chekekechea wana digrii

Mfano Mwalimu wa Chekechea anatikiwa juwa na Bachelor degree in Early Childhood Education, Mwalimu wa shule ya Msingi anatakiwa kuwa na degree in Primary Education na Sekondari anatakiwa kuwa na digrii I Secondary Education

Tanzania vyuo vyetu vikuu vinatoa degree zote hizol lakini wengi wanaenda shule.za.Private ndio.maana performance ya shule za Private kuanzia,chekechea,Msingi na sekondari ziko vizuri sana

Hata hivyo nipongeze wizara walau kwa kuanza taratibu lakini kwa huo mtaala mpya nadhani ingekuwa waanze kuajiri walimu pia wenye digrii za education za checheka,msingi na sekondari ili taratibu hsta hao wa diploma wawe faced out taratibu hadi tufikie mahali digrii tupu ziwe zinafundisha shule xote kuanzia chekechea hadi sekondari
Halafu diploma zifutwe?
 
Haya ni maelezo Yako ila Kwa mujibu wa maelezo ya mtaalamu hapo Juu watapewa nafasi wajiendeleze..

Mimi.mzee wangu alikuwa Mwalimu wa UPE akiwa.mtu mzima.ilikuja.order ajiendeleze vinginevyo Ajira inakata na alilazimika kufanya mtihani wa form 4 na kusoma upya cheti ,saizi alishaga staafu.
Duh🙄
 
Walimu ambao hamna diploma Jiandaeni kufanya mtihani wa form six na kusomea Masomo ya Diploma.

Wale ambao hamna Digree Jiandaeni Kurudi vyuo Vikuu kuwa wanafunzi tena.
Elimu ya diploma kwa sasa imerahisishwa. Siyo lazima ufanye mtihani wa form six.

All in all, nimefarijika sana na huu mtaala mpya wa elimu. Naamini ukisimamiwa ipasavyo, basi miaka kadhaa ijayo wimbi la ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana nchini, litapungua kwa asilimia kubwa.
 
Maelezo ni lazima wafike Form six Ili wawe na sifa ya kufundisha primary
 
Back
Top Bottom