Mama Naa
JF-Expert Member
- Aug 31, 2020
- 385
- 949
Amani iwe juu yenu nyote.
Mwalimu wa Nchi hii nadhani ametengenezewa UMASKINI kuanzia anaajiliwa mpaka anastafu. Kwanza ni watu wanaotoka kaya Maskini bado akiajiliwa anaishi kwenye umaskini akistaafu bado anakutana na KIKOKOTOO.
Mwalimu akiajiriwa anaanza na mshahara wa TGTS D1 (SANAA) 771,000/= na SAYANSI ni 750,000/= na hawa ni wa Degree Moja.
Hapo Mwalimu alipe kodi ya nyumba, Maji , Umeme, asomeshe, Ale, ahudumie familia na wengine ukoo Mzima. Bado mnataka avae apendeze kama kada zingine.
Mwalimu ili apande daraja afikie TGTS E1 basi itamchukua miaka 4 mpaka 5 nayo inategemeana na Rais wa wakati huo. (SIASA).
Hivi ni kwa nini daktari umlipe TGHS D1 (1270000) tofauti ya laki tano na mwalimu wa Degree na yeye ana degree wakati wengine walisoma wote hadi F6?
Walimu ndio nguzo ya Taifa, Taifa bora linatokana na raia wake walioelimika vizuri kwa kuwa na Walimu bora.
HAKUNA WALIMU BORA BILA MASLAHI BORA.
UALIMU ni vile tu umebebwa sana na watoto wa maskini ila SIO kazi ya kufanya.
Mwalimu hana House allowance, hana perdiem, hana extra duty, hana overtime bado awe mtumishi bora, Watu wanafanya bora liende tu.
Serikali waangalieni Walimu kwa jicho la pekee kama mnataka Taifa liwe bora.
Serikali haishindwi kuhudumia vizuri walimu 250,000+ (Msingi 170,000+ na sekondari 89,000+ huku walimu wa masomo ya Sayansi na hisabati wakiwa 23,000+)
Sio haki eti Mwalimu wa Degree kufikia Mshahara wa 1280,000 ambao ni TGTS F1 ni mpaka akae kazini miaka 8 - 10+ BADO TUNATAKA TAIFA LILILOELIMIKA?
INATIA UCHUNGU SANA, WANASIASA MMEJIWEKEA MASLAHI BORA SANA ILA WATUMISHI MKAAMUA KUWAPA KIKOKOTOO.
WATZ NI KWA NINI TUMEKUBALI MBUNGE MIAKA 5 APEWE MILIONI 270+ HALAFU MTUMISHI APEWE MILIONI 40+ KWA MIAKA 30 - 40 YA UTUMISHI?
TAIFA HILI LINA LAANA WALLAH.