Walimu wa mjini Vs walimu wa bush.

Walimu wa mjini Vs walimu wa bush.

dorry

Senior Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
136
Reaction score
28
Mwanafunzi wa darasa la nne huko kijijini alikuwa akisafiri na baba kwenda mjini kwa shangazi yake. Basi lilipoanza kuingia mjini mtoto wa watu alikodoa jicho dirishani si kidogo, na alionekana kuwa anatafakari jambo. Mara akamgeukia baba yake na kumwuliza:-

Mtoto:- Baba, walimu wa mjini wana akili sana kuliko wa kijijini?
Baba:- Hapana mwanangu, wote wako sawa.
Mtoto:- Baba, walimu wa kijijini ni wavivu na wana upendeleo kuliko wa mjini?
Baba:- Hapana mwanangu, wote wako sawa. Kwa nini unauliza hivyo mwanangu?
Mtoto:- Baba, walimu wetu usahihisha kwenye daftari zetu tu na unaweza kupata vema au kosa, lakini huku mjini ni kosa tu tena mpaka majumbani na vibaoni barabarani.
 
Ebanae uko juu ka kikombe cha babu tena wanapiga kosa hadi kwenye computer
 
Hahaha! huyu atakuwa ameona 'X' za Magufuli kwenye majengo/matangazo.
 
mtoto alitafakari sana...kwanin kila nyumba na vibao barabarani vyote ni X......magufuli bana..amemkwaza sana mtoto huyu
 
Waalimu wa wakala wa barabara hao....wote "wavuvi" kweli kweli kila kibao na nyumba ni X wakati yeye amezoea kuona tuu kwenye daftari lake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom