Walimu wa kiume baadhi mjiheshimu

Walimu wa kiume baadhi mjiheshimu

Shule gani? Mwalimu anaitwa nani? Hapa JF waziri wa hiyo sekta n mwanachama.

Tafadhali toa details ni rahisi kufuatilia na kuchukua hatua, vinginevyo unafurahisha baraza au unafurahia mwanao kuliwa mate na mwalimu unayemuita Sharobaro.

Kwamba anampa points mkuu mpwayungu za kuwabomoa zaidi waalimu badala ya kutatua tatizo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tv ni hatari Sana zinaharibu ubongo Mimi namshukuru Sana Mama yangu hakupenda kununua TV Hadi namaliza masomo ya sekondari .

Kiufupi wazazi Kazi mnayo nipo hapa Temeke ila watoto wadogo hasa miaka 15+ aisee ni hatari jamani Mungu awasaidie Sana.

Then na ugumu wa Maisha ya utafutaji unachangia Mama na baba wanaamkia katika kutafta RIZIKI wanarudi usiku so mtoto anashinda mtaani anaranda randa.

Then walimu mtawafunga Sana Ila hata wao ni zao la malezi mabovu.

Mzazi hata Kama hauna PESA hakikisha mwanao haumpi smartphone na Tv Bora umpe laptop ajifunze kuandika makala
 
Watoto wanapewa UTI, kaswende, gono, clamidia, HIV na mimba juu kisa kurubuniwa na vipesa vya mihogo na lift lift....hawa wanaume ni dont care na wachafu kwenye kila kitu anakojoa kwa kila mwanamke kila dak na kila saa
Aisee, hapa walezi tuna kazi nzito. ndiyo maana mie bora nijinyime mie lkn niwape madogo coz najua kuna vitu wanavitamani,,,,,,kuepusha vitamaa ya vitu vidogovidogo.
 
Kulea mtoto wa kike ni shughuli pevu, mbaya zaidi ukute mama yake naye ni mdoli utatokwa jasho zito. Kina mama wengine wanalea watoto wao wa kike vibaya sana. Wanawalea as if ni wadogo zao, wana share story za mapenzi hawaheshimiani. Unakuta mama anajua ramani nzima na michongo ya kimapenzi ya binti yake wala hamkemii anaona mwanae anafaidi vinono.
 
Hiyo ni kweli, nikikumbuka mama alivyokuwa mkali kwetu, nami napita mulemule,

Hiyo mzazi kujua ramani ya mwanae ipo sana baadhi ya wazazi wanaishi kwa mgongo wa watoto wao, kuna dogo ana mtoto na anaishi kwao, ni juzi tu jioni alikuwa anamuaga mama yake kuwa anatoka,,,mama mtu akamjibu mwanae kazingatie maokoto.
 
Sijui nikueleze vipi, huyu dogo ni bado mtoto, kwa hayo mambo ni bado.
Hii sentensi ya bado mdogo sana, mwenzio aliiongea mwaka 2021 mtoto wake akiwa form 2, (Shule ya Bujiku S, Mwanza. kilichokuja kutokea, HEAD MAMA/Mmwalimu mkuu wa kikie ni kumchukua binti hadi Polisi na kulalamikia Mwalimu kufanya mapenzi na mwanafunzi. Polisi wakamuita mzazi wa binti, binti mwenyewe + Head Mama na kuelekea Hospital kupata vipimo. Majibu ya vipimo/Dokta ni mimba + HIV. Binti kuhojiwa anasema kapewa na mwalimu wake wa kemia.
Polisi walifungua kosa la KUMPA MIMBA MWANAFUNZI. Ila mwalimu alichosomewa mahakamani ni ktk hati ya mashtaka ndio balaa...
1) Kumpa mimba mwanafunzi.
a) Kutorosha mwanafunzi.
b) Kubaka mtoto chini ya miaka 18.
c) kufanya mapenzi na mwanafunzi na kumpa maambukiki.
Hukumu iliyotoka ni JELA MIAKA 30 kwa kosa la kubaka mwanafunzi chini ya miaka 18.

Sasa dada yangu hii kauli ya ni mdogo hafanyi sio usiipende kuitumia maana sio rafiki. Walimu wenyewe wa sasa ni vitoto vya boding, hawaelewi hata jamii ikoje.
 
Hiyo ni kweli, nikikumbuka mama alivyokuwa mkali kwetu, nami napita mulemule,

Hiyo mzazi kujua ramani ya mwanae ipo sana baadhi ya wazazi wanaishi kwa mgongo wa watoto wao, kuna dogo ana mtoto na anaishi kwao, ni juzi tu jioni alikuwa anamuaga mama yake kuwa anatoka,,,mama mtu akamjibu mwanae kazingatie maokoto.
Kama mama anamwambia mwanae azingatie maokoto, kisha mwanangu wa kiume aniambie kuhusu kuoa ktk hiyo familia mmoja kati ya watoto wa familia hiyo. Mwanangu akatafute na baba yake. Hiyo familia kwangu ni kirusi, siwezi kukubali kinivae.
 
Kumbe TVs zinafundisha mambo mabaya? Kwanini tunaruhusu watoto wetu waangalie?

Malezi yaanzie nyumbani.
Siku hizi mzazi kakulia boding, hivyo hajapata malezi ya kijiji/mtaa/jamii nje ya boding. Malezi yanabaki kua ya mzazi tu kwa kusaidiwa na binti wa kazi. Ni marufuku mtu wa nje kumrudi mtoto asie wake afanyapo kosa. Ukimchapa tu umetafuta bifu la maisha, utaulizwa hadi alipotokea kama unapajua.
 
Mwambie huyo. Mimi wananisogezeaga hadi tunyonyo twao lakini wapiii. Miaka kenda sasa naendelea kutunza heshima yangu[emoji120]
20230930_013345.jpg
 
Kama mama anamwambia mwanae azingatie maokoto, kisha mwanangu wa kiume aniambie kuhusu kuoa ktk hiyo familia mmoja kati ya watoto wa familia hiyo. Mwanangu akatafute na baba yake. Hiyo familia kwangu ni kirusi, siwezi kukubali kinivae.
Nilishangaa,coz wengine na utu uzima huu kuaga tu unawaza naagaje?
 
Assalaam,

Ni hivi nina kawaida ya kuwahoji wadogo zangu maisha ya shule na marafiki wao wa aina gani?

Nina wadogo zangu wawili wapo kidato cha kwanza, na shule wanayosoma ni mpya ipo kidato cha kwanza tu.

Leo niliwauliza vipi shule kuna walimu wa kiume vijana wangapi? Madogo wakasema wapo wanne, wawili ni watu wazima lakini wawili ni masharobaro.

Nikawapa onyo/vitisho kuhusu hao vijana, yaani wasidanganyike maana ni bado wapo na akili za kitoto sana.

Mmoja akasema kuna siku nilikuwa napeleka daftari ofisini nikamkuta ticha na fulani walikuwa wanafanya kama kwenye TV….nikamuuliza walikuwa wanafanyaje? akasema walikuwa wananyonyana mate huku wamekumbatiana.

Aisee na huyu ticha ana mke na mtoto.

Walimu hii haipo sawa,waacheni watoto wasome, wewe ushasoma na upo kazini, imagine mtoto wako anafanyiwa hivyo kama unavyomfanyia mtoto wa mwenzio?

Msiwaharibie future wadogo zetu nao wanataka kuwa kama nyie.

Mjitahidi kubalance hiyo mihemko.
Nenda pale shule omba kuonana na Mpwayungu village akija ,mkanye na umtishe unampeleka Kwa mwenye shule.Utakuja kutoa ushuhuda hapa.
 
Back
Top Bottom