Walimu wa kiume baadhi mjiheshimu

Walimu wa kiume baadhi mjiheshimu

MawardatDellapina

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2021
Posts
30,334
Reaction score
152,700
Assalaam,

Ni hivi nina kawaida ya kuwahoji wadogo zangu maisha ya shule na marafiki wao wa aina gani?

Nina wadogo zangu wawili wapo kidato cha kwanza, na shule wanayosoma ni mpya ipo kidato cha kwanza tu.

Leo niliwauliza vipi shule kuna walimu wa kiume vijana wangapi? Madogo wakasema wapo wanne, wawili ni watu wazima lakini wawili ni masharobaro.

Nikawapa onyo/vitisho kuhusu hao vijana, yaani wasidanganyike maana ni bado wapo na akili za kitoto sana.

Mmoja akasema kuna siku nilikuwa napeleka daftari ofisini nikamkuta ticha na fulani walikuwa wanafanya kama kwenye TV….nikamuuliza walikuwa wanafanyaje? akasema walikuwa wananyonyana mate huku wamekumbatiana.

Aisee na huyu ticha ana mke na mtoto.

Walimu hii haipo sawa,waacheni watoto wasome, wewe ushasoma na upo kazini, imagine mtoto wako anafanyiwa hivyo kama unavyomfanyia mtoto wa mwenzio?

Msiwaharibie future wadogo zetu nao wanataka kuwa kama nyie.

Mjitahidi kubalance hiyo mihemko.
 
Shule gani? Mwalimu anaitwa nani? Hapa JF waziri wa hiyo sekta n mwanachama.

Tafadhali toa details ni rahisi kufuatilia na kuchukua hatua, vinginevyo unafurahisha baraza au unafurahia mwanao kuliwa mate na mwalimu unayemuita Sharobaro.
 
Shule gani? Mwalimu anaitwa nani? Hapa JF waziri wa hiyo sekta n mwanachama. Tafadhali toa details ni rahisi kufuatilia na kuchukua hatua, vinginevyo unafurahisha baraza au unafurahia mwanao kuliwa mate na mwalimu unayemuita Sharobaro.
Hilo nalifanyia kazi coz shule ipo kitaani hapa hapa, na huyu kijana ni mgeni tu.
 
Mwanamke au binti kama hajakukubalia basi huwezi kulala naye.

Shida mabinti wa sasa, wanaangalia kama kwenye TV halafu wanafanya kwa vitendo.

Kumbuka jamii yoyote kuna watu wema na wabaya. Hapo ulipo mnaweza kuwa watu 12 na zikaletwa soda 12, utashangaa mmoja kati yenu amechukua soda 2 wakati anajua mpo 12.

Muhimu vijana wapewe elimu ya mahusiano na madhara yake. Itasaidia sana
 
Muhoji vizuri huyo binti inawezekana yeye ndio akawa mshirika mwenza wa kunyonyana mate na teacher.

Ikiwa tayari una ushahidi toka kwa dogo nini kilikuzuia kwenda kumkabili mwalimu husika na uongozi wake?? Au unataka mpaka usikie katia mimba mwanafunzi?
 
Alikujibu kwamba....Walikua wanafanya kama kwenye Tv...🤨

Ebu tuanze na huyo mdogo wako, hiyo kama kwenye TV aliiona wapi?

Je unapata wapi ujasiri wa kumsema mwalimu wakati mdogo wako anajua hadi na mfano amekueleza?

Unajua...... nimejikuta najiukiza maswali mengi sana baada ya kupata hilo jibu la mdogo wako...🤨
 
Pamoja na kuwaasa walimu wajiheshimu, ila sisi kama wazazi tuna jukumu kubwa sana la kuhakikisha watoto wetu wanapata malezi bora n stahiki.

Hao wadogo zako, wanaonaga kwenye TV. Kukumbatiana na kunyonyana ndimi, unaona ni jambo la kawaida. Kwamba, wanafurahia shows.

Ila ukumbuke vitoto vya sasa balehe ni miaka 12 mpaka 15. Hao wapo form 1 au 2. Vinakuwa na mchecheto na mgegedo. Wakishawishiwa kidogo tu, na walichokiona kwenye TV, wanakuwa fundi kuliko hata wazazi wao. Ukijumlishia na vinavyojua kucheza mziki kwa kunengua, ptyuuu mbaka.

Wazazi tujitahidi kutilia mkazo malezi ya watoto wetu. Huyo hata akitongozwa, anakataa. Anajua si jambo jema.

Lawama zote tusizielekeze kwa walimu pekee. Bali sisi pia kama walezi tunastahili.
 
Muhoji vizuri huyo binti inawezekana yeye ndio akawa mshirika mwenza wa kunyonyana mate na teacher...
Kwa huyu hapana ni bado, hata matiti bado wala ungo hajavunja na bado ana akili za kichekechea.

Maana nishamwambia ukija kuwa mkubwa na ukaanza kuonana na mwanaume basi unapata mimba na maradhi/ ukimwi, akasema basi kuanzia leo simuangalii mwanaume usoni[emoji23]
 
Back
Top Bottom