Walimu wa kisasa kwaya za ibada za kikatoliki wanaua ladha halisi ya ibada za kikatoliki

Kyenyabasa

JF-Expert Member
Mar 8, 2023
249
711
Zamani ilikuwa kwaya za kiibada zinavutia na kusisimua lakini wamekuja vijana wa hovyo wanajiita walimu wa kwaya yaaji Wana edit kila kitu mwisho wa siku kwaya za ibada hazigusi mioyo na kusisimua, ilikuwa kawaida mwanakwaya wa Bukoba kuimba kwaya Mtwara bila shidaa yoyote ila sasa ni ngumu...

Yamebaki majimbo machache yaliyotunza kwaya halisi za ibada za kikatoliki, hapa nilipongeze Jimbo la Bukoba na majimbo karibu yote ya kagera.

USHAURI: Naishauri TEC kuhakikisha wanadhibiti kirusi cha uharibifu wa kwaya halisi za ibada za kikatoliki,siyo kila kitu kiwe cha kisasa hii itakuwa vurugu kanisani na kutukosesha Iadha tam na muruaaaa ya ukatoliki.

Sasa hivi hata mapadri wa kisasa hawana ladha kwenye kuimba injili mpaka mtu unahisi unapaa mbinguni.

Mapadri wa zamani walikuwa na vionjo bwana wawapo madhabahuni mpaka tukawa tunavutiwa kuwa mapadri
 
Kanisa
Waturudishie rc ya zamani ukitoka kanisani unakuwa unatafakari ibada sio hii ya Sasa hivi imejaa michango busy nzima ya ibada michango.

Waturudishie rc ya zamani ukitoka kanisani unakuwa unatafakari ibada sio hii ya Sasa hivi imejaa michango busy nzima ya ibada michango.
Kanisa linajengwa na wenye moyo! Ukiona vyaelea ujue vimeundwa! Shida yng ni hawa walimu wa hovyo wanaobadili ladha ya kale ya kwaya zetu za ibada
 
Bahati mbaya watunzi wengi wa nyimbo nzuri za Kikatoliki wameshatangulia mbele ya haki! Mfano watu kama John Mgandu, Fr. Kayeta, Mkomagu, na wengineo wengi; hatunao tena.

Binafsi bado ninawakubali watunzi wachache wa sasa mfano David Wasonga, Ben Nturama, Ernest Nyanza, Beatus Idama, Ernest Ogeda, nk. Walau nyimbo zao bado zinaenzi yale mapigo ya zamani ya Kikatoliki.
 
Bila kumsahau mzee Mwarabu! Naye yuko vizuri sana!
 
Naunga mkono hoja,Kanisa katoliki Kuna shida sehemu
Kila mtu Kawa kambale .

Kuhusu mada yako wapo mapadre na maaskofu wasio ijua liturjia vizuri na wanakwenda na usasa kwao kutunza mapokeo ya kikatoliki hata sio issue kwao. Hawa ndio wanaowavimbisha kichwa hao akina Mukasa na genge lake.

Tazama hta nyimbo za kwaya wanazopiga radio Maria na tumaini tv n hayo hayo masebene ya watunzi wafanyabiashara ,what do you expect?

Miaka kumi ijayo kanisa katoliki halitokuwa na tofauti ya nyimbo za kiibada na haya makanisa tunayaita ya kipentekoste.
 
Unapoteza muda tu
Hao mapadre na maaskofu wanachojali n mtonyo kwa kwenda mbele hayo ya kuhusu nyimbo hayawangaishi hta kidogo.

Kanisa limekuwa la kujali vitu zaidi kuliko ustawi wa watu hasa maskini.

Ndo mana wenye akili siku hizi hawaendi makanisani
Upuuzi upuuzi mtupu.
 
Bahati mbaya watunzi wengi wa nyimbo nzuri za Kikatoliki wameshatangulia mbele ya haki! Mfano watu kama John Mgandu, Fr. Kayeta, Mkomagu, na wengineo wengi; hatunao tena.

Binafsi bado ninawakubali watunzi wachache wa sasa mfano David Wasonga, Ben Nturama, Ernest Nyanza, Beatus Idama, Ernest Ogeda, nk. Walau nyimbo zao bado zinaenzi yale mapigo ya zamani ya Kikatoliki.
Vipi akina Ngurumo na Mukasa ?
 
Ansbert Ngurumo yuko vizuri. Kivumbi ni hao akina Bernard Mukasa na wenzake!! Hao ndiyo wanaosemwa chini chini kuharibu misingi ya liturujia ya nyimbo za Kikatoliki nchini.
Mukasa ameharibu nini?
Kuna Jimbo Moja sitolitaja baadhi ya mapadre wake walipiga marufuku nyimbo za Mukasa!!!
Btw ngoja nirudi church nikapashe vidole, Nina wimbo mpya wa kusolve!!
 
Mukasa ameharibu nini?
Kuna Jimbo Moja sitolitaja baadhi ya mapadre wake walipiga marufuku nyimbo za Mukasa!!!
Btw ngoja nirudi church nikapashe vidole, Nina wimbo mpya wa kusolve!!
Kitambo sana amekuwa akishutumiwa yeye na wenzake kama Gabriel Mkude, nk kutunga baadhi ya nyimbo zenye maudhui tofauti na zile zilizo zoeleka ndani ya Kanisa. Nothing more.
 
Back
Top Bottom