Walimu na Wanafunzi Serengeti Watapeliwa

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,991
1,364
Walimu na Wanafunzi Serengeti Sekondari Walizwa kizembe!!

Wahenga walisema ‘Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao’ Kuna mtu anayesadikika alifika kwenye ofisi ya Mkuu wa shule mapema juma hili tarehe 28/03/2022 na kujitambulisha kwa jina la Ditric, mwenyeji wa Mbeya na amekuwa akifadhiliwa na BONBOSCO iliyoko Mbeya . Kwa sasa anaendelea na masomo nchini Italia na yupo nchini kwa ajiri ya Likizo. Hivyo kipindi hiki cha likizo anaomba kuwa anafundisha kama mwalimu wa Muda.

Kuwa kabla ya kwenda Italia, alisoma chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM) masomo ya Sayansi na kupata ufaulu wa First Class. Ni mtaalamu wa practicals na anavifaa vya kisasa vya kufundishia practicals ambavyo ufanya ujifunzaji wa hizo practical kuwa rahisi.
  • HOJA ALIZOTUMIA
  • Aliahidi wanafunzi kuwa viongozi wote wa wanafunzi watapewa Tablets zitakazo wasaidia kwenye masomo yao.
  • Monitors na classmonitress watapewa computer(laptops) zitakazo wafanya wafuatilie vipindi wakiwa popote bila usumbufu na laptop hizo haziitaji bando kujiendesha.
  • Wanafunzi yatima na wale wanaoishi mazingira magumu watapewa Review za masomo yote bure na dictionary, hivyo wajiandikishe ili taratibu zifanyike waletewe.
  • Wanafunzi walio na wazazi waliahidiwa kila mmoja kupewa Review za masomo yote na Dictionary.
NAMNA UTAPELI ULIVYOFANYIKA
Wanafunzi waliambiwa wachangie kila mmoja Tsh 5000, ili waletewe hivyo vifaa, mwitikio ukawa mkubwa, watoto wakachanga. Siku iliyokuwa imeahidiwa ilikuwa siku ya jumatano saa 5;00 asubuhi kuwa vifaa vitafika.

Pesa zilichangwa kimadarasa, madarasa yaliyokamilisha yalimkabithi pesa, siku moja kabla ya siku ya ahaadi kufika mtoa ahadi hakuonekana, hakuna anaejua, anaishi kwa nani, na yupo wapi na alitokea kwa nani, pesa zimechukuliwa kilaiiiiini

Pesa zilikusanywa kama sadaka zikisubiri ziesabiwe na mhasibu, hakuna anayejua kiasi
 
Hii sio inside job..
 
La casa de papel
images.jpg
 
Back
Top Bottom