Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Katika maisha hakuna cha bure,cha bure kina manyanyaso lukuki,now Makondakta watakua wanachukua nauli kabla ya daladala kuondoka,na ukiwa ni mwalimu haki ya mungu Konda atakushusha na matusi juu!,tunaanza kurudishwa enzi za ujamaa,currently we have to move on with capitalism system ndio tutaendelea kama taifa,hivi vya bure bure vinatupumbaza,tunakua hatuwezi kuwa na mapinduzi ya kifikra coz tunaamini katika bure,shida ya mwalimu sio pesa ya nauli,bali ni changamoto anazokutana nazo coz of maslahi duni huku akiwa na matatizo chungu mzima!
 
Sasa Napata Kicheko Pale Teja Amepiga Debe Wee Gari Limejaa Level Seat Na Kusimama, Konda Akamtoa Teja 500 Yake, Akalipa Ada Ya Kituo, Pale Simu 2000, Makumbusho, Mbagala, Mbezi Mwisho N.k. Basi Linaodoka, Mbele Konda Anaanza Kuchukua Nauli Kwa Abiria Wake, Anakutana Na Waalimu Lukuki Wenye Hivyo Vitambulisho!! Maana Nafuu Wanafunzi Wanatambulika Kirahisi Kutokana Na Sare Zao Na Umri Wao!! Sasa Waalimu Watakuwa Wanatambulika Vp!!!?? Au Makondakta Watakuwa Wanawakagua Mlangoni Kila Abiria Mtu Mzima!!!!!?? Ugumu Na Chanzo Cha Vurugu Na Mapambano Kati Ya Waalimu, Madereva Na Makondakta!!!
 
Katika maisha hakuna cha bure,cha bure kina manyanyaso lukuki,now Makondakta watakua wanachukua nauli kabla ya daladala kuondoka,na ukiwa ni mwalimu haki ya mungu Konda atakushusha na matusi juu!,tunaanza kurudishwa enzi za ujamaa,currently we have to move on with capitalism system ndio tutaendelea kama taifa,hivi vya bure bure vinatupumbaza,tunakua hatuwezi kuwa na mapinduzi ya kifikra coz tunaamini katika bure,shida ya mwalimu sio pesa ya nauli,bali ni changamoto anazokutana nazo coz of maslahi duni huku akiwa na matatizo chungu mzima!

nitashangaa CWT wakikaa kmya ktk hili...

maana linabagua walimu. inamaana walimu wa kinondoni au dar ndio muhimu kuliko wa sehemu zngine?
 
Walimu msikubali kudhalilishwa namna hii! yaani muanze kuzuiwa mlangoni kama watoto wa shule?!
 
Katika maisha hakuna cha bure,cha bure kina manyanyaso lukuki,now Makondakta watakua wanachukua nauli kabla ya daladala kuondoka,na ukiwa ni mwalimu haki ya mungu Konda atakushusha na matusi juu!,tunaanza kurudishwa enzi za ujamaa,currently we have to move on with capitalism system ndio tutaendelea kama taifa,hivi vya bure bure vinatupumbaza,tunakua hatuwezi kuwa na mapinduzi ya kifikra coz tunaamini katika bure,shida ya mwalimu sio pesa ya nauli,bali ni changamoto anazokutana nazo coz of maslahi duni huku akiwa na matatizo chungu mzima!

nitashangaa CWT wakikaa kmya ktk hili...

maana linabagua walimu. inamaana walimu wa kinondoni au dar ndio muhimu kuliko wa sehemu zngine?
 
Ugomvi/tatizo la walimu na serikali, hili ni janga la bara zima la afrika na baadhi ya nchi zilizo endelea lazima tulijue hilo
 
kwa mwalimu mm sitoweza kusafiri bure isije nikasodolewa kuwa unafanya kazi ipi!!!!!!! hadi ushindwe kulipa nauli ya 400 kaaah huu uzalilishaji wakiaina.. Wakitaka waanzishe gari special kwa walimu na wanafunzi tu. Hapo sawa ila kusema hz za public ivi munawajua makondoka wakiwa wanataka hesabu ya bosi au vp......

Anaetaka kitambulisho changu tutafutane nitampa wakitoa mie huko kwa bureeee no no NOOO. mshahara wangu unalipa nauli sitaki kukutana na nyodo zao toka enzi nasoma primary hadi advanced level na sasa mmmmmh hapana aiseeee.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri bure katika daladala.

Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka

Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam

Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3.Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilaya Paul Makonda

source:MILLARDAYO.COM
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.
Okay! Ameongea na makondakta pia? madereva je? ...Wangenunua mabasi special ya walimu ingekua poa sana. Vinginevyo wanataka kuleta ugomvi!
 
Taarifa kamili ya DC Makonda hii hapa:
============================
Moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa John Pombe Magufuli imefanya kuwa kipaumbele kikubwa kwenye mipango yake ya maendeleo ni suala la uboreshaji wa sekta ya elimu nchini na ndiyo maana serikali imeanza utekelezaji wa mpango huu kwa kufuta ada zote shuleni.

Kimsingi, ni ndoto hii ya Mheshimiwa Rais ambayo nina uhakika kila mmoja wetu anaelewa ukubwa wa faida zake kwenye ujenzi wa Tanzania mpya na yenye wasomi na wataalamu wa kila namna, tena wanaopatikana bila kuzingatia hali ya kipato cha familia anayotokea mwanafunzi, iliyonifanya mimi kama msaidizi wake katika nafasi ya ukuu wa wilaya nijiulize kila wakati juu ya ushiriki wangu wa kuhakikisha inatimia kimamilifu.

Maswali hayo yamenifikisha kwenye wazo la kuboresha sekta hii kwa kuchagua kufanya jambo ambalo wakati serikali ikiendelea kupigania changamoto nyinginezo za kuboresha ajira za walimu, ikiwemo upandishwaji wa madaraja na mishahara, basin a mimi katika nafasi yangu nishiriki kwenye mchakato huu mzima kwa kutoa motisha ya usafiri wa bure kwa walimu wote wanaotufundisha kwenye shule za serikali zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa tatu: Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi, na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Rais za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia.

Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.

Kwa sababu hizo nilizoziainisha hapo juu, ninaomba kuwatangazia walimu wangu bwa shule zote za serikali kuanzia za msingi paka sekondari ya kwamba, sasa watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao.

Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na hatimaye mazungumzo hayo kuhitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.

Kipee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwao wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wamesema ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.

Utaratibu kwa walimu juu ya utumiaji wa fursa ambayo tumeipata utakuwa kama ifuatavyo: Moja, nimemuelekeza ofisa elimu wa sekondari na shule za msingi kutoa maelekezo kwa wakuu wa shule zote za serikali zilizopo wilayani kwangu na wilaya nyinginezo za Jiji la Dar es Salaam, kutengeneza vitambulisho vya shule zao vitakavyokuwa na picha ya mwalimu, jila lake kamili, jina la shule anayofundisha, namba ya simu ya mkuu wa shule husika pamoja na saini yangu mimi mwenyewe Paul Makonda ili kuepuka udanganyifu.

Nimewataka zoezi hili walifanye na kulikamilisha ndani ya wiki moja ambapo baada tu ya kukamilika itakuwa ni furaha yangu kuwatangazia walimu wote wa shule za serikali jijini Dar es Salaam kuwa, watakuwa wakipanda daladala bure ila tu kwa siku za Jumatatu mpaka Ijumaa na kwa muda was aa 11:30 mpaka saa 2:00 asubuhi, na kati ya saa 9:00 alasiri hadi saa 12:00 jioni.

Ingawa kila mwalimu atalazimika kuonyesha kitambulisho chake alichotengenezewa kwenye shule yake pamoja na kile cha ajira ya serikali.

Imetolewa na:

Paul Makonda

Mkuu wa Wilaya - Kinondoni
 
Uzalilishaji kwa walimu waongezewe maslai wapewe ela za nauli waweze kusafiri kwa Uhuru huku ni kufanya walimu waonekane ni wafanyakazi Wa chini katika jamii yeye angesema wanafunzi wasafiri bure
Do you mean polisi na wanajeshi nao ni wafanyakazi wa chini sana?
 
Kipee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwao wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wamesema ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.
Angefanya vema sana kuongea na makondakta na madereva , maana ndio wanaoshinda barabarani na ndio wanaosaka cha juu baada ya kupeleka mzigo kwa boss ( mmiliki)!
 
serikali italeta magari ya walimu kama tunayoona idara nyingine kama mahakama, mem, bot etc? kama ni huu usafiri wa umma haitawezekana
 
Bado adui wa mwalimu,kushuka kwa elimu,kufanya vibaya kwa shule za serikali utatuzi unakimbiwa;suruhu sio kupandisha daladala walimu bure;hapo ni dar,vp huku nyarusunguti,ngerengere,na maeneo mengine ambayo mwalimu anaendesha baiskeli masaa mawili kuelekea kazini?!!
Bado nchi inaendeshwe kiujanja ujanja na mikakati ya ujanja ujanja isiyo na mantiki;
Ni kwa kipindi kirefu serikali imekua ikikimbia njia maridhawa za kutatua changamoto za walimu na badala yake huja na mipango ya ujanja ujanja km hii ya Makonda...Inasikitisha sana
 
Mawazo ni mazuri lakini changamoto yake ni kubwa Sana. Walimu wetu watanyanyasika Sana. Wazo nzuri ni kuwapa pre-paid card ambazo zimelipiwa tayari na makonda waelemishe maana ya hizo pre-paid cards,lakini bure itakuwa kuwavunjia heshima walimu mbele ya jamii na wanafunzi wao.

Viongozi wa Darcoboa, Uwadar ambao ni wamiliki wa vyombo hivyo, pamoja na mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi maderava Tanzania (TADWU) walikuwepo na wametoa kauli ya pamoja kuhusu suala hilo. Wamesema wameridhia wenyewe kuunga mkono juhudi za serikali.

Kama ni suala la kudhalilika, basi tuseme askari wetu wa Polisi, Magereza, JKT na JWTZ nao wanadhalilika kwa sababu wao walipewa fursa hiyo na Chama cha Wenye Daladala Dar es Salaam (MUWADA) mwanzoni mwa miaka ya 1990 na uamuzi ukaungwa mkono nchi nzima.

Tungesubiri tuone, kwa sababu daima kuna mahali pa kuanzia.
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri bure katika daladala.

Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka

Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam

Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3.Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilaya Paul Makonda

source:MILLARDAYO.COM
makonda kumbe ana coverage kubwa Dar nzima? Tungejiuliza kwanza kama hiyo ndo priority ya walimu wa sm na sec. Je walimu wanatumia % ya mshahara kwenye nauli?
 
Safi sana makonda,bado sijaona mkuu wa wilaya au mkoa aliye creative kama ww.
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Ukisikia kukurupuka ndio huku, Rais ana watu wa ajabu sana chini yake, huyu anataka kila daladala iwe inawakimbia walimu, hii ingefanya kazi kama mabasi yangekuwepo wangekua na kadi special kirahisi tu, japo kila mtu angekomaa na yeye kupata kadi hiyo ili asafiri bure. Walimu walipwe vizuri tu basi, ili wawe na uwezo wa kujilipia wenyewe usafiri, au waongezewe hela ya usafiri kila mwezi wajue wanavyoitumia wenyewe.
 
Back
Top Bottom