nampongeza pia kwa sababu anataka kuibua mgogoro ambao labda utasaidia kurekebisha baadhi ya sera za usafiri pamoja na kero za walimuSafi sana Makonda
Serikali ikumbuke na kuwapatia mafuta wamiliki wa daladala walau 500 lts kwa mwezi hapo serikali itakuwa imewaweza makondakta wakorofiKama watatengenzewa kitambulisho ambacho kinawekeka mfukoni au kwenye handbags sioni Kama kutakuwa na manyanyaso mana mwalim ataingia kwenye Gari bila hata kujulikana Kama ni mwalim ila wakat wa konda anadai chake ndo pale anaonyeshwa kitambulisho, pia nafkiri iwekwe sheria kali kwa konda yoyote atakae mnyanyasa mwalim.mbona hatujawah kuskia wanajeshi wananyanyasika kwenye madaladala? Hii nchi sheria zikisimamiwa vizuri kila mtu atakuwa na adabu na hata mwanafunzi anaweza kusafiri bure tuache ujinga ujinga
Kama wamiliki wa magari wameridhia, Kondakta au dereva atakataa vipi?Okay! Ameongea na makondakta pia? madereva je? ...Wangenunua mabasi special ya walimu ingekua poa sana. Vinginevyo wanataka kuleta ugomvi!
Hizo Nchi Ambazo Zimeendelea Zenye Hilo Tatizo Ni Zipi!!?? Au Ukiona Ama Uganda Ndio Unaelewa Bara Zima La Africa!!! Weka Evidence Zako Sio Porojo!! Humu Jf Ni Great Thinkers Mkuu!! Evidence Ndio Mtaji Wako!!Ugomvi/tatizo la walimu na serikali, hili ni janga la bara zima la afrika na baadhi ya nchi zilizo endelea lazima tulijue hilo
Sawa na kusema unaenda kwenye sherehe unapewa unakaribishwa chakula we unasema umeshiba ila wakupe hela utanunua chakula ukiumwa njaa wanasaidiwa ambao wanashida ya usafiri wenye magari wao wana nafuu..basi wapaki magari wapande bure.Je, Waalimu wenye vyombo vyao vya usafiri wamefikiriwaje kwenye mpango huu
Hivi unajua kusoma kweli?Wamiliki wamekubali kutoa Huduma bure?
Huyu dogo akipewa huu mkoa hakika mtaona mengi msiyoyatarajiaMkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri bure katika daladala.
Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka ’
‘Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam’
‘Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3.Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilaya Paul Makonda’
source:MILLARDAYO.COM
Nawa mikoani muwape pikipiki na baiskeli kuongeza tija, bila hivyo mtakuwa mnaleta utengano kwenye kada ya ualimu.Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wanazungumza na wanahabari hivi sasa.
Walimu wstatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.
Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.
Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.