Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

mkuu wa mkoa wa Dar ajae?ila why walimu tu?wangefanya pia kwa wafanyakazi wote wenye vipato vya chini
 
Viongozi wa Darcoboa, Uwadar ambao ni wamiliki wa vyombo hivyo, pamoja na mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi maderava Tanzania (TADWU) walikuwepo na wametoa kauli ya pamoja kuhusu suala hilo. Wamesema wameridhia wenyewe kuunga mkono juhudi za serikali.
Wamiliki kukubali tu siyo issue, maana wanajua kua wao sio watekelezaji! yaani hawatakua barabarani , na wanajua anayeongea nao hana uwezo wa kutoa maelekezo kwa madereva na makondakta , maana dala dala sio mali ya umma
 
KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,

KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,

NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____

INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.

NIMEMALIZA!
Kwanini mnajenga taswira hasi kwenye kila jambo....hisia za ramli,uchauchawi...hamu yako nikuona mpango unashindwa ili uje JF bila nguo usherehekee!...mbona zamani kulikuwa na tiketi maalum kwa wanafunzi na makundi maalum na iliwezekana?
 
Sahihi ya mkuu wa wilaya "Paul Makonda?"

Anaamini atakuwa DC wa Kinondoni milele siyo?

Angesema kitambulisho kiwe na sahihi ya DC kwa maana whoever come still aendelee kutambua ID hizo!

By the way, anadhani hitaji na changmoto kuu ya walimu ni "ofa ya kupanda daladala bure" au kawaonaje hawa watu?

Changamoto kubwa ya walimu ni makazi kwa maana ya nyumba za kuishi na maslahi bora kwa maana ya mishahara inayokidhi mahitaji yao ya msingi kwa mwezi!

Itasaidia nini kupakiwa kwenye daladala bure unafika nyumbani unamkuta mwenye nyumba uliyopanga anasubiria kodi yake ya miezi sita au mwaka mzima ya vyumba vyako viwili?

Tunadhani kwa hilo pekee hata kama mwalimu amepanda daladala bure akafika kazini salama atafundisha watoto kwa amani kweli wakati makazi yake yako jeopardized?

Mimi nadhani viongozi wetu ifike wakati waache kutafuta kick za ovyo za kisiasa kupitia kwa wafanyakazi wanyonge kama walimu na badala yake wafikiri namna ya kutatua matatizo halisi yanaikabili sekta ya elimu na walimu!!

Ushahidi wa hili kuwa ni "kick ya kisiasa tu", namna ni linavyowasilishwa kwa umma na kuonesha kuwa halina uendelevu (sustainability) wowote!

Ni mpango unaoanzishwa leo, kesho unakufa!!

Huyu anayeitwa "Paul Makonda" kama DC siku akifyokolewa na hata kutumbuliwa jipu, na mpango unakuwa umefia hapohapo. Yes, si wa Makonda bwana, au?....Na bahati labda aende Tandahimba, na mpango huo utamfuata huko!!!
 
Izo..pumba sn kwangu.waalimu wana madai wanalalamika mishahara midogo we leo unazunguamzia kupanda daladala bure km sio upuuzi ni nn?? Ye makonda anapanda daladala kwenda kazini?? Km wanataka Kuwaondole waalimu kero ya usafiri wangeandaa mabasi ya shule au kungekua na usafir maalum km walivo wafanyakazi wa taasisi zingine..lkn sio eti 'wapande daldala bure' huu ni unyanyasaji
 
Walimu lilieni maslahi bora,sio kudanganywa na vijiexemption vya nauli ya daladala,mnahitaji makubwa kuliko vijinauli vya daladala
 
Makonda kijana huyu anaakili sana itabidi awe mkuu wa mkoa wa dar anafaa sana.
 
Huyu bwanamdogo ni jipu toka kitambo! Maamuzi mengine yafaa kuwa universal; k'ndoni siyo nchi, nawaunga baadh ya wadau hapo juu kwamba tatizo LA mwalimu ni zaid ya hiyo nauli!
Me ni mwalimu pia, nachoona hapo ni siasa kwenye mambo ya msingi! Maamuzu hayo hayajalenga kumsaidia mwlm was nchi hii Bali kumdhalilisha na kumfanya awe inferior. Yawezekanaje mwanafunzi anaelipa 200 akeshe kituoni na mwalm apande bure tukiamini atawahi kazini? Me naona anatutekenya walimu huku anacheka yeye!!!
Nasubir nione matokeo!
We mwalimu gani hunaakili wewe siyo yule meya anayefuga madevu?
 
Kwanini wapande bure.. si wawaongezee mishahara wanunue magari yao au wanunue magari yawabebe wao.. maana foleni ni ile ile au wasipolipa nauli ndio watawahi kufundisha??
 
Itakuwaje kama mwalimu kapanda basi saa1.30 na konda anadai Nauli saa2.15?.Sote tunajua kwamba unaweza kukaa ndani ya basi kwa zaidi ya SAA mbili.
 
Mi mwalim,ila mpango huu siafikiani nao maana utakua wa manyanyaso na kudhalilishana,nadhan SUMATRA DSM wasimamie suala la upandishaj wa naul kiholela,huko nakofanyia kaz abiria wa kutumainiwa kwenye daladala au noah nzima ni walim,je itakuaje???
 
KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,

KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,

NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____

INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.

NIMEMALIZA!
Nimecheka sn lakini umeongea POINT za msingi.
 
Viongozi wa Darcoboa, Uwadar ambao ni wamiliki wa vyombo hivyo, pamoja na mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi maderava Tanzania (TADWU) walikuwepo na wametoa kauli ya pamoja kuhusu suala hilo. Wamesema wameridhia wenyewe kuunga mkono juhudi za serikali.

Kama ni suala la kudhalilika, basi tuseme askari wetu wa Polisi, Magereza, JKT na JWTZ nao wanadhalilika kwa sababu wao walipewa fursa hiyo na Chama cha Wenye Daladala Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 1990 na uamuzi ukaungwa mkono nchi nzima.

Tungesubiri tuone, kwa sababu daima kuna mahali pa kuanzia.

Wasi wasi wangu,kiongozi,ni time limit.Mwalimu anaweza kupanda basi mbagala SAA 10.30,konda akadai nauli banana,saa 12.30.Muda wa makonda umekwisha,konda anadai Nauli kamili upo hapo?
 
Huyu bwanamdogo ni jipu toka kitambo! Maamuzi mengine yafaa kuwa universal; k'ndoni siyo nchi, nawaunga baadh ya wadau hapo juu kwamba tatizo LA mwalimu ni zaid ya hiyo nauli!
Me ni mwalimu pia, nachoona hapo ni siasa kwenye mambo ya msingi! Maamuzu hayo hayajalenga kumsaidia mwlm was nchi hii Bali kumdhalilisha na kumfanya awe inferior. Yawezekanaje mwanafunzi anaelipa 200 akeshe kituoni na mwalm apande bure tukiamini atawahi kazini? Me naona anatutekenya walimu huku anacheka yeye!!!
Nasubir nione matokeo!
Huyu si ameahidiwa kuwepo kwenye uteuz ujao wa ma DC na RC. Kwahiyo anaongezea misifa
 
Upuuzi mtupu sasa hayo masaa yanamaanisha nini? dar es salaam huwez kupanga wakati maalum kwa safari ni issue ya foleni sasa vipi wakati utaenda sambamba na mafoleni? kama ni bure iwe ni bure tu bora wangetoa jumamosi na jumapili kuliko hayo mambo ya ajabu kuhusu masaa.,

Na vipi kuhusu raia kusafiri bure itaanza lini? Qatar public transport wanalipwa na serikali wananchi wanasafiri bure, tunataka tuone hili pia likitokea na Tz kama kweli munajali wananchi.
 
Amekaa na walimu wakamwambia wanashida hiyo au ameona walimu ni Kama madenti!! Kwa taarifa yake walimu wanataka kukopeshwa magari kama wabunge na wengine pikipiki.
Tusiwachukulie walimu kimaskini kiivyo,mbona manesi,madaktari hajawafanyia huo mlango au wao hawawahi kazini.
Ubunifu Wa kilofa kabisa,tuko karne ya 21 jamani,nlienda nchi flani wapishi washule ndio wanafanyiwa mpango kukopeshwa magari,walimu gari sio kitu ya kuuliza Tena wanalipiwa na kodi nyumba za heshma wasiwe na msongo wa mawazo kuhusu makodi. Hapa walimu vyumba viwili tu na bado kodi inamuwazisha.
 
Back
Top Bottom