Walimu 14 Dar es Salaam wanashikiliwa kwa kukiuka sheria katika mitihani ya Darasa la 7

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Walimu 14 kwa tuhuma za kukiuka sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za mitihani ya darasa la saba iliyofanyika Oktoba 5-6, 2022.

Uchunguzi wa suala hili unaendelea na taarifa zitatolewa na mamlaka zinazohusika na masuala ya elimu.


===============

JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA 24 KWA TUHUMA MBALIMBALI ZA KIHALIFU, WAKIWEMO WEZI SUGU WA MAGARI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mifumo ya kuzuia vitendo vya kiuhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Mohamed Amani (45)@kiziwi, mkazi wa Dar es Salaam na Mwanza pia Salome Richard (32) mama G, mkazi wa Mwanza na wenzao wanane kwa tuhuma za wizi wa magari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika Operation hiyo kali, Jeshi la Polisi limeyakamata magari 23 aina mbalimbali, ambayo ni IST 5, fuso 1, Nissan Civilian 1, Coaster 1, Toyota Hilux pickup 1, Nissan patrol 1, Toyota

Premio 2, Probox 1, Spacio 2, Harrier 2, Ravfour 3, Town Hiace 2 na Hiace 1, magari haya yamekamatwa katika Mikoa ya Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Kagera, na Dar es Salaam.

Baada ya kuwahoji kwa kina watuhumiwa na hivyo kuwapeleka wapelelezi yalipo mgari hayo. Upelelezi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa watuhumiwa hawa kabla ya kuiba huvizia magari hayo yakiwa yameegeshwa kwenye maegesho ya jumla, binafsi na majumbani baadae kuvunja vitasa vya milango ya upande wa dereva na kuwasha gari kwa kutumia fungo bandia na kuondoka.

Aidha watuhumiwa hao baada ya kuiba magari hayo hubandika namba za usajili na chasses za magari yaliyopata ajali na kuuzwa kama vyuma chakavu na makampuni ya bima baadae kuyauza tena magari hayo waliyoyaiba. Baadhi ya magari yameshatambuliwa na wamiliki na upelelezi unaendelea.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limewakamata na linawashikilia watuhumiwa sita (majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa tuhuma za wizi wa vifaa mbalimbali vya miundombinu ya TANESCO vinavyotumika katika ujenzi umeme wa msongo wa kati (REA).

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 06/10/2022 majira ya saa nane mchana maeneo ya Mwenge, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa na vifaa mbalimbali vya miundombinu ya TANESCO kwenye gari aina ya Noah yenye namba za Usajili wa T 165 DPR.

Upelelezi wa Jeshi la Polisi umebaini kwamba vifaa hivyo ambavyo ni mali ya kampuni ya State Grid Electrical and Technical LTD na Tropical Industrial LTD viliibwa Mkoa wa Morogoro na Lindi, na watuhumiwa hao walikuja Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta soko.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kukwamisha maendeleo kwa miradi hiyo imejengwa kwa manufaa ya umma. Ufuatiliaji na uchunguzi wa kina unaendelea.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pia linawashikilia jumla ya Walimu 14 kwa tuhuma za kukiuka sheria, kanuni, na taratibu mbalimbali za mitihani ya darasa la saba iliyofanyika tarehe 5-6 mwezi wa 10, 2022. Uchunguzi wa suala hili unaendelea na taarifa zitatolewa na mamlaka zinazohusika na masuala ya elimu.
 
Huo mtandao wa wizi wa magari, aisee umetia fora! Magari yote hayo!! Sasa sisi wa Mikoani si ndiyo rahisi sana kununua hayo magari ya wizi!
 
Umeona ukiweka walimu ndio tittle itanoga sio!?

Hivi hamjui KADA ya ualimu ndio imechangia 50% ya maendeleo ya nchi hii!?

Yaani marais sita watatu ni walimu by profession Mwinyi,jpm na NYERERE !kuliko KADA nyingine zote !!!

Aiseh bas Sawa
 
Wapigaji wa KYLANDA hawakamatwi na polisi na kufanyiwa uchunguzi ili pesa za wadau zirudi ila walimu 14 wanakamatwa simply because?!

Polisi wakita kuwashika KYLANDA waanze na huyu 👉🏿 Jazajuan atawasaidia katika upelelezi wao

Nisiseme sana..
 
Back
Top Bottom