Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
Bei ya Sukari imepanda nchini; kuna hisia kwamba yawezekana kuna upungufu wa sukari. Hata hivyo gazeti la Daily News toleo la Jumatano Machi 9, 2010 lina habari ambayo si ngeni kwa wale ambao wamefuatilia siku za hivi karibuni hususan mwitikio wa serikali kwenye suala la upungufu wa sukari nchini. Gazeti hilo linaripoti maelezo toka kwa mmoja wa viongozi wa Chama cha Wazalishaji wa Sukari nchini ambaye alidai kuwa "hakuna upungufu wa sukari" bali baadhi ya wazalishaji wa sukari "wanashikilia" kiasi kikubwa sukari na akatolea mfano wa Tanganyika Plantantion Company wanashikilia kiasi cha tani elfu 15 za sukari.
Taarifa ya gazeti hilo ilidokeza kuwa lengo la baadhi ya wazalishaji sukari kushikilia sukari na kutoiachia ifike sokoni ni kutengeneza kile ambacho gazeti limeita ni "artificial shortage" yaani "mwonekano wa upungufu' wa sukari sokoni na hiyo kufanya ugavi wa sukari kuwa kidogo kitu ambacho kitapandisha bei ya sukari.
Lengo ni kutengeneza faida kwa haraka haraka kwa kutumia migongo iliyopindika kwa kazi ngumu ya Watanzania. Matokeo ya kufanya ongezeko la bei ya sukari ni kama yale ambayo yamewahi kusababisha vurugu huko India (bei ya Vitunguu) na sehemu nyingine kama huko Misri (bei ya mikate) n.k. Vitu hivi kwa watu wengine ni vitu vidogo lakini ni vitu ambavyo vinasumbua maisha ya watu.
Ninaamini tatizo la umeme kwa mfano, linagusa asilimia 14 tu ya Watanzania moja kwa moja, lakini bei ya sukari inagusa maisha ya karibu kila Mtanzania aliye tajiri na aliye maskini, inagusa mahoteli, mashule n.k Hili ni jambo linalotishia zaidi hali ya kisiasa nchini kuliko maandamano ya Chadema - isipokuwa kama watasisitiza kuandamana dhidi ya kupanda kwa bei ya sukari.
Serikali ilitolea tamko suala hili mwishoni mwa mwezi wa pili pale Waziri wa Viwanda na Biashara alipotoa maelezo marefu ambayo yanasimama kama ushahidi wa jinsi watawala wanavyozidi kushindwa kusimamia sheria zilizopo na badala yake wanajiuma uma meno mbele ya mafisadi. Waziri Cyril Chami alisema hivi kuhusu upungufu huo wa sukari na kuongezeka kwa bei yake kwenye soko la reja reja.
Rais Kikwete mwenyewe katika hotuba ya kufunga mwezi wa pili alisema hivi:
Sheria ya Uhujumu Uchumi ya 1984 iko wazi kabisa kuhusu suala la kushikilia bidhaa kwa lengo la kuchezea soko. Sheria hiyo inaweka katika orodha ya makosa ya kiuchumi ambayo yanasimamiwa na sheria hiyo kwenye jedwali la kwanza. Sheria inasema (msisitizo wa kwangu):
Sina wehu wowote wa kufikiria kuwa serikali ina uwezo au ubavu wa kuingilia kati suala hili na kuhakikisha wanaofanya vitu hivi wanakabiliwa na mkono mkali wa sheria. Serikali ambayo imeshindwa kumhoji mtu kama Rostam kwa jambo zito kama la nishati sidhani na sina sababu ya kudhani kuwa inaweza kuwatia nguvuni walanguzi wa sukari na wahujumu uchumi.
Ndio maana wengine wanapolilia kwenye luninga ati "chadema ni wachochezi" tunawashangaa kwa sababu mambo yanayowachochea wananchi kuchukia serikali yao ni kama haya mambo ya bei za bidhaa muhimu. Huu ni uchochezi unaofanywa na kushindwa kwa vyombo vya dola kusimamia sheria ipasavyo na kubaki kukodoleana macho na mafisadi na wahujumu uchumi kiasi hata cha kukaa nao mezani.
La kwanza, ni lazima wawaite kwa jina lao halisi - wahujumu uchumi"
Pili, sheria ifuate mkondo wake na siyo vikao; laiti kila mhalifu angeitwa mezani na kujadiliana naye ili afafanue kwanini anafanya uhalifu!
Amka Tanzania

Kitu ambacho Waziri Chami alikuwa anakizungumzia kama "ni jambo la kawaida" kinapakana na vitendo vya uhalifu. Kwa Waziri kama yeye anajua kabisa kinachofanywa na wafanyabiashara hao ni kumanipulate the market na naomba nipendekeze kuwa ni kinyume cha sheria. Na ni muhimu kutambua vile vile kuwa kiasi cha sukari kinachoshikiliwa hakishikiliwi na watengenezaji tu bali na wauazaji wa reja reja vile vile - ni tabia ambayo ina ripple effect.Kwa vile mahitaji ya bidhaa yoyote ya kawaida yakizidi upatikanaji wake bidhaa ile hupanda bei, ni jambo la kawaida kwa wanaoiuza bidhaa ile kuwa na nia ya kuihodhi bidhaa husika, ili bei ikipanda zaidi siku za usoni wanufaike zaidi. Hali hii inajulikana kama speculation kwa lugha ya Uchumi. Ni jambo la kawaida pia kwa baadhi ya wazalishaji na wasambazaji kuihodhi bidhaa husika kwa minajili ya kujilinda, isije ikawaishia wakati washindani wao wakingali wanayo, kwani hilo likitokea, washindani wao watanufaika na bei kubwa na hivyo kuwaondoa katika uzalishaji au usambazaji. Tabia hii ya kujilinda inaitwa hedging against competition kwa lugha ya Kiuchumi. Hivyo hivyo hapa Tanzania, nguvu hizi mbili, speculation na hedging against competition, zimewafanya baadhi ya wenye viwanda na baadhi ya wasambazaji kuweka sukari nyingi katika maghala.
Rais Kikwete mwenyewe katika hotuba ya kufunga mwezi wa pili alisema hivi:
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ni bei ya Sukari. Hivi karibuni bei ya sukari nchini imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa na katika baadhi ya maeneo nchini bei ya sukari ilifika zaidi ya shilingi 2,200 kwa kilo.NilimuombaWaziri Mkuu kufuatilia kwa karibu tatizo hilo na amefanya hivyo. Alikutana na wadau wote wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa sukari nchini. Kilichobainika ni kuwa bei ya sukari ilipanda sana kwa sababu ya kuwepo upungufu wa sukari katika soko. Upungufu wa sukari katika soko ulikuwa umesababishwa na sukari iliyokuwepo katika maghala ya viwanda vya sukari na ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari kutofikishwa kwa wingi madukani kwa hofu ambazo hazikuwa na msingi. Aidha, mahusiano mabaya kati ya wazalishaji na wafanyabiashara wakubwa wa sukari ilikuwa sababu kubwa. Wenye viwanda wakawa wanatoa kiasi kidogo kuliko wafanyabiashara walichokuwa wanaagiza. Kwa upande wao wafanyabiashara wakubwa nao wakawa wanasambaza kiasi kidogo kidogo kwa madai kuwa wasijekuishiwa kabisa na bidhaa hiyo.
Katika mazungumzo hayo ilibainika kuwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa wanayo sukari ya kutosheleza mahitaji mpaka mwezi Mei, 2011. Kutakuwa na uhaba katika miezi ya Mei na Juni kutokana na ukweli kwamba viwanda vya sukari nchini husimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Februari hadi Mei kila mwaka. Hiki ni kipindi cha mvua nyingi, miwa hunyonya maji mengi hivyo huwa haitoi sukari nyingi. Wenye viwanda hutumia muda huo kusimamisha uzalishaji na kufanya matengenezo ya mitambo.
Ndugu Wananchi;
Waziri Mkuu aliagiza sukari yote iliyoko katika maghala itoke mara moja na kufikishwa katika soko ili watu waipate tena kwa bei nafuu. Katika mazungumzo ya pamoja na wadau, ilikubalika kabisa kuwa hata kwa maeneo yaliyo mbali na viwanda vya sukari bei haiwezi kuzidi shilingi 1,700/= kwa kilo. Atakayeuza kwa bei kubwa zaidi ya hiyo anadhulumu, taarifa zitolewe ili hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kufutiwa leseni ya biashara.
Sheria ya Uhujumu Uchumi ya 1984 iko wazi kabisa kuhusu suala la kushikilia bidhaa kwa lengo la kuchezea soko. Sheria hiyo inaweka katika orodha ya makosa ya kiuchumi ambayo yanasimamiwa na sheria hiyo kwenye jedwali la kwanza. Sheria inasema (msisitizo wa kwangu):
Sasa wakati wa Nyerere hakukuwa na vikao kama hivi na hata nchi nyingine kama Marekani wanazo sheria kali kabisa kuhusu suala hili la black market (ulanguzi) na magendo. Lugha hii ya "uhujumu uchumi", "ulanguzi" na "magendo" inaonekana inataka kupotea kutoka katika vyombo vya usimamizi wa sheria kiasi kwamba serikali inaogopa au haina ujasiri tena wa kukabiliana na vitendo hivi kwa sababu watu watalia "suala la uhujumu uchumi". Lakini hiki ndicho kinachotokea sasa hivi na ni wakati serikali ioneshe uongozi.4.-(1) A person, whether or not licensed to carry on the business of selling commodities
of any description, is guilty of the offence of hoarding commodities against this
paragraph if, not being a manufacturer or producer of the commodities-
(a) he is found in possession of an unusually large or big amount or quantity of
commodities which are in demand by the public in the locality concerned, in
circumstances in which it can be inferred that they are not displayed or stocked
for lawful sale or use or available for purchase by any persons offering the lawful
price; or
(b) he sells or offers any commodity for sale at a price or subject to a term or condition
which is unlawful or which, having regard to all relevant circumstances, is
unreasonable; or
(c) in the course of carrying on the business of selling any commodity, he engages in
any trade practice which is intended or likely-
(i) to create an artificial shortage in the supply of any commodity; or
(ii) to aggravate an actually existing shortage in the supply of any comcommodity;
or
(iii) to cause an unlawful increase or decrease in the official or commercially
accepted price of any commodity; or
(iv) to adversely affect the fair distribution of any commodity amongst the
purchasing population of the area concerned.