Waliitwa "wahujumu uchumi"; Sasa Serikali inakaa nao mezani!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Bei ya Sukari imepanda nchini; kuna hisia kwamba yawezekana kuna upungufu wa sukari. Hata hivyo gazeti la Daily News toleo la Jumatano Machi 9, 2010 lina habari ambayo si ngeni kwa wale ambao wamefuatilia siku za hivi karibuni hususan mwitikio wa serikali kwenye suala la upungufu wa sukari nchini. Gazeti hilo linaripoti maelezo toka kwa mmoja wa viongozi wa Chama cha Wazalishaji wa Sukari nchini ambaye alidai kuwa "hakuna upungufu wa sukari" bali baadhi ya wazalishaji wa sukari "wanashikilia" kiasi kikubwa sukari na akatolea mfano wa Tanganyika Plantantion Company wanashikilia kiasi cha tani elfu 15 za sukari.

Taarifa ya gazeti hilo ilidokeza kuwa lengo la baadhi ya wazalishaji sukari kushikilia sukari na kutoiachia ifike sokoni ni kutengeneza kile ambacho gazeti limeita ni "artificial shortage" yaani "mwonekano wa upungufu' wa sukari sokoni na hiyo kufanya ugavi wa sukari kuwa kidogo kitu ambacho kitapandisha bei ya sukari.

Lengo ni kutengeneza faida kwa haraka haraka kwa kutumia migongo iliyopindika kwa kazi ngumu ya Watanzania. Matokeo ya kufanya ongezeko la bei ya sukari ni kama yale ambayo yamewahi kusababisha vurugu huko India (bei ya Vitunguu) na sehemu nyingine kama huko Misri (bei ya mikate) n.k. Vitu hivi kwa watu wengine ni vitu vidogo lakini ni vitu ambavyo vinasumbua maisha ya watu.

Ninaamini tatizo la umeme kwa mfano, linagusa asilimia 14 tu ya Watanzania moja kwa moja, lakini bei ya sukari inagusa maisha ya karibu kila Mtanzania aliye tajiri na aliye maskini, inagusa mahoteli, mashule n.k Hili ni jambo linalotishia zaidi hali ya kisiasa nchini kuliko maandamano ya Chadema - isipokuwa kama watasisitiza kuandamana dhidi ya kupanda kwa bei ya sukari.

Serikali ilitolea tamko suala hili mwishoni mwa mwezi wa pili pale Waziri wa Viwanda na Biashara alipotoa maelezo marefu ambayo yanasimama kama ushahidi wa jinsi watawala wanavyozidi kushindwa kusimamia sheria zilizopo na badala yake wanajiuma uma meno mbele ya mafisadi. Waziri Cyril Chami alisema hivi kuhusu upungufu huo wa sukari na kuongezeka kwa bei yake kwenye soko la reja reja.

Kwa vile mahitaji ya bidhaa yoyote ya kawaida yakizidi upatikanaji wake bidhaa ile hupanda bei, ni jambo la kawaida kwa wanaoiuza bidhaa ile kuwa na nia ya kuihodhi bidhaa husika, ili bei ikipanda zaidi siku za usoni wanufaike zaidi. Hali hii inajulikana kama speculation kwa lugha ya Uchumi. Ni jambo la kawaida pia kwa baadhi ya wazalishaji na wasambazaji kuihodhi bidhaa husika kwa minajili ya kujilinda, isije ikawaishia wakati washindani wao wakingali wanayo, kwani hilo likitokea, washindani wao watanufaika na bei kubwa na hivyo kuwaondoa katika uzalishaji au usambazaji. Tabia hii ya kujilinda inaitwa hedging against competition kwa lugha ya Kiuchumi. Hivyo hivyo hapa Tanzania, nguvu hizi mbili, speculation na hedging against competition, zimewafanya baadhi ya wenye viwanda na baadhi ya wasambazaji kuweka sukari nyingi katika maghala.
Kitu ambacho Waziri Chami alikuwa anakizungumzia kama "ni jambo la kawaida" kinapakana na vitendo vya uhalifu. Kwa Waziri kama yeye anajua kabisa kinachofanywa na wafanyabiashara hao ni kumanipulate the market na naomba nipendekeze kuwa ni kinyume cha sheria. Na ni muhimu kutambua vile vile kuwa kiasi cha sukari kinachoshikiliwa hakishikiliwi na watengenezaji tu bali na wauazaji wa reja reja vile vile - ni tabia ambayo ina ripple effect.

Rais Kikwete mwenyewe katika hotuba ya kufunga mwezi wa pili alisema hivi:

Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ni bei ya Sukari. Hivi karibuni bei ya sukari nchini imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa na katika baadhi ya maeneo nchini bei ya sukari ilifika zaidi ya shilingi 2,200 kwa kilo.NilimuombaWaziri Mkuu kufuatilia kwa karibu tatizo hilo na amefanya hivyo. Alikutana na wadau wote wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa sukari nchini. Kilichobainika ni kuwa bei ya sukari ilipanda sana kwa sababu ya kuwepo upungufu wa sukari katika soko. Upungufu wa sukari katika soko ulikuwa umesababishwa na sukari iliyokuwepo katika maghala ya viwanda vya sukari na ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari kutofikishwa kwa wingi madukani kwa hofu ambazo hazikuwa na msingi. Aidha, mahusiano mabaya kati ya wazalishaji na wafanyabiashara wakubwa wa sukari ilikuwa sababu kubwa. Wenye viwanda wakawa wanatoa kiasi kidogo kuliko wafanyabiashara walichokuwa wanaagiza. Kwa upande wao wafanyabiashara wakubwa nao wakawa wanasambaza kiasi kidogo kidogo kwa madai kuwa wasijekuishiwa kabisa na bidhaa hiyo.

Katika mazungumzo hayo ilibainika kuwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa wanayo sukari ya kutosheleza mahitaji mpaka mwezi Mei, 2011. Kutakuwa na uhaba katika miezi ya Mei na Juni kutokana na ukweli kwamba viwanda vya sukari nchini husimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Februari hadi Mei kila mwaka. Hiki ni kipindi cha mvua nyingi, miwa hunyonya maji mengi hivyo huwa haitoi sukari nyingi. Wenye viwanda hutumia muda huo kusimamisha uzalishaji na kufanya matengenezo ya mitambo.


Ndugu Wananchi;

Waziri Mkuu aliagiza sukari yote iliyoko katika maghala itoke mara moja na kufikishwa katika soko ili watu waipate tena kwa bei nafuu. Katika mazungumzo ya pamoja na wadau, ilikubalika kabisa kuwa hata kwa maeneo yaliyo mbali na viwanda vya sukari bei haiwezi kuzidi shilingi 1,700/= kwa kilo. Atakayeuza kwa bei kubwa zaidi ya hiyo anadhulumu, taarifa zitolewe ili hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kufutiwa leseni ya biashara.



Sheria ya Uhujumu Uchumi ya 1984 iko wazi kabisa kuhusu suala la kushikilia bidhaa kwa lengo la kuchezea soko. Sheria hiyo inaweka katika orodha ya makosa ya kiuchumi ambayo yanasimamiwa na sheria hiyo kwenye jedwali la kwanza. Sheria inasema (msisitizo wa kwangu):

4.-(1) A person, whether or not licensed to carry on the business of selling commodities
of any description, is guilty of the offence of hoarding commodities against this
paragraph if, not being a manufacturer or producer of the commodities-
(a) he is found in possession of an unusually large or big amount or quantity of
commodities which are in demand by the public in the locality concerned, in
circumstances in which it can be inferred that they are not displayed or stocked
for lawful sale or use or available for purchase by any persons offering the lawful
price; or

(b) he sells or offers any commodity for sale at a price or subject to a term or condition
which is unlawful or which, having regard to all relevant circumstances, is
unreasonable; or
(c) in the course of carrying on the business of selling any commodity, he engages in
any trade practice which is intended or likely-
(i) to create an artificial shortage in the supply of any commodity; or
(ii) to aggravate an actually existing shortage in the supply of any comcommodity;
or
(iii) to cause an unlawful increase or decrease in the official or commercially
accepted price of any commodity; or
(iv) to adversely affect the fair distribution of any commodity amongst the
purchasing population of the area concerned.
Sasa wakati wa Nyerere hakukuwa na vikao kama hivi na hata nchi nyingine kama Marekani wanazo sheria kali kabisa kuhusu suala hili la black market (ulanguzi) na magendo. Lugha hii ya "uhujumu uchumi", "ulanguzi" na "magendo" inaonekana inataka kupotea kutoka katika vyombo vya usimamizi wa sheria kiasi kwamba serikali inaogopa au haina ujasiri tena wa kukabiliana na vitendo hivi kwa sababu watu watalia "suala la uhujumu uchumi". Lakini hiki ndicho kinachotokea sasa hivi na ni wakati serikali ioneshe uongozi.

Sina wehu wowote wa kufikiria kuwa serikali ina uwezo au ubavu wa kuingilia kati suala hili na kuhakikisha wanaofanya vitu hivi wanakabiliwa na mkono mkali wa sheria. Serikali ambayo imeshindwa kumhoji mtu kama Rostam kwa jambo zito kama la nishati sidhani na sina sababu ya kudhani kuwa inaweza kuwatia nguvuni walanguzi wa sukari na wahujumu uchumi.

Ndio maana wengine wanapolilia kwenye luninga ati "chadema ni wachochezi" tunawashangaa kwa sababu mambo yanayowachochea wananchi kuchukia serikali yao ni kama haya mambo ya bei za bidhaa muhimu. Huu ni uchochezi unaofanywa na kushindwa kwa vyombo vya dola kusimamia sheria ipasavyo na kubaki kukodoleana macho na mafisadi na wahujumu uchumi kiasi hata cha kukaa nao mezani.

La kwanza, ni lazima wawaite kwa jina lao halisi - wahujumu uchumi"
Pili, sheria ifuate mkondo wake na siyo vikao; laiti kila mhalifu angeitwa mezani na kujadiliana naye ili afafanue kwanini anafanya uhalifu!

Amka Tanzania
 
Mkuu MMK
Sirikali ya wezi hii, kuna watu wananufaika sana na ugumu wa maisha unaotukumba, actually wanautengeneza huu ugumu
 
Mkuu MMK
Sirikali ya wezi hii, kuna watu wananufaika sana na ugumu wa maisha unaotukumba, actually wanautengeneza huu ugumu


I like the way you put it; thanks. Halafu wanajitokeza kutuokoa.. the same template ya mafisadi.. tengeneza upungufu wa nishati ya umeme halafu jitokeze kuwaokoa Watanzania! gademu!!
 
Hivi wew huchoki fitina kila kukicha? Hujuwi kuwa Tanzania ni soko huru? Na hujuwi kuwa Bei za vyakula zimepanda duniani?
 
I like the way you put it; thanks. Halafu wanajitokeza kutuokoa.. the same template ya mafisadi.. tengeneza upungufu wa nishati ya umeme halafu jitokeze kuwaokoa Watanzania! gademu!!

Kujitokeza kwa fitina? Si uje Tanzania ujumuike na wanaharakati wenzio kushusha bei za vitu kwa maandamano?

Hivi nawauliza, pesa za maandamano mnazo, pesa za kuagiza Sukari ya bei nafuu mkaisambaza nchini bila faida, kwa gharana tu, ili kusaidia wanyonge hamna? Au hilo hamuwezi? Nyie mradi mtie chokochoko tu?
 
Hivi wew huchoki fitina kila kukicha? Hujuwi kuwa Tanzania ni soko huru? Na hujuwi kuwa Bei za vyakula zimepanda duniani?

Anamfitina na alimfitina nani?? Kama wewe unalipwa na rostam huna budi kuzungumza haya lakini kama mama yako au watoto wako wanakosa sukari kwa sababu ya uzembe na upumbavu wa serikali iliyopo madarakani utaelewa linalozungumzwa hapa kama huelewi funga mdomo wako na ukae kimya. Sisi wengine tuna uchungu unaposikia mama anasema mwanangu leo tumekosa kupata kifungua kinywa kwa vile sukari imeisha. Lala usingizi ukiyasikiliza maneno na kilio hiki ambacho ni cha watanzania wengi utaujua uchungu wake. Otherwise hamia nyumbani kwa rostam ukawe mk%%$#&&^ maana baada ya yote utalipwa upate pesa ya kununua hiyo sukari.
 
mi nafkiri wanawakumbatia hao wezi, wahujumu uchumi na mafisadi papa kwa sababu tu walichangia pesa zao na mali zao kwa CCM wakati wa uchaguzi so ndo wanarudisha chao bila aibu wala huruma, huku viongozi wakijiumauma wanachofanya ni kuwabembeleza badala ya kuwashtaki huku sheria iko wazi kabisa dah tanzania!
Cha muhimu sis kama wananchi ni kuikataa ccm na wapambe wake chama pamoja na rasilimali zake zooote bado wanatembeza bakuli hawafai na 2015 ndo watakopa hela mingi sana tukiwapa tena ridhaaa mama yangu! Watatunyonyaje? Zingatia chukua hatua coz life now ni gumu mbaya kabisa
 
Anamfitina na alimfitina nani?? Kama wewe unalipwa na rostam huna budi kuzungumza haya lakini kama mama yako au watoto wako wanakosa sukari kwa sababu ya uzembe na upumbavu wa serikali iliyopo madarakani utaelewa linalozungumzwa hapa kama huelewi funga mdomo wako na ukae kimya. Sisi wengine tuna uchungu unaposikia mama anasema mwanangu leo tumekosa kupata kifungua kinywa kwa vile sukari imeisha. Lala usingizi ukiyasikiliza maneno na kilio hiki ambacho ni cha watanzania wengi utaujua uchungu wake. Otherwise hamia nyumbani kwa rostam ukawe mk%%$#&&^ maana baada ya yote utalipwa upate pesa ya kununua hiyo sukari.

Inaonesha ni vipi mlivyokosa sera na kubaki ooh "unalipwa na Rostam", hivi huyu Rostam mnataka awafundishe mpaka basics za biashara? Au hanjuwi kuhusu "demand and supply".

Ushauru wa bure wa kusaidia wananchi: Chadema mna wafanya biashara na mna mabepari wakubwa tu kwenye uongozi, si agizeni sukari muijaze nchini kwa gharama, bei itashuka ikitaka isitake.

Hapo ndio itakuwa "action speaks louder than words" kwa upande wenu. Kuliko majungu na ufataani.
 
Mkuu MMK
Sirikali ya wezi hii, kuna watu wananufaika sana na ugumu wa maisha unaotukumba, actually wanautengeneza huu ugumu

Hivi serikali ilikuzuwia wewe kuleta Sukari na kuuza? Kuilima na kuisambaza? Au Chadema hamna waziri kivuli wa kilimo? Wa biashara? Kama mnao si muanze na mkakati wa Sukari bei poa? Wafanya biashara si mnao? Au hamna?
 
Hivi serikali ilikuzuwia wewe kuleta Sukari na kuuza? Kuilima na kuisambaza? Au Chadema hamna waziri kivuli wa kilimo? Wa biashara? Kama mnao si muanze na mkakati wa Sukari bei poa? Wafanya biashara si mnao? Au hamna?
wezi wanahold bidhaa ili upungufu uonekane na wewe unajidai unaleta theory za supply na demand hapa wizi mtupu
 
kwanini bei za vitu vishuke wakati kuna soko huru?

Huna sera, leta Sukari kwa wingi na iuze kwa bei poa, uone kama haijashuka bei. Tena ili kuzuwia "uhujumu uchumi" uisambaze na kuiuza kwenye ofisi za chadema. Hapo tutawaona wa maana. Kuliko Sukari ikipanda bei "Rostam". Mkikosa kura "Rostam" Umeme hakuna "Rostam" Mbowe anahodhi fedha kibao za akiba ya wazee na hataki kulipa kwa kisingizio kuwa kala hasara, nalo pia "Rostam".

Ikiwa sera na juhudi zenu ni za namna hiyo, hakuna mnalo/mtakalo liweza zaidi ya fitina na majungu.

Kama hamna uwezo wa biashara toweni mawazo "productive" ya kibiashara ili kuzuwia upandaji wa bei au majungu ndio yatasaidia kushuka bei za sukari?
 
Huna sera, leta Sukari kwa wingi na iuze kwa bei poa, uone kama haijashuka bei. Tena ili kuzuwia "uhujumu uchumi" uisambaze na kuiuza kwenye ofisi za chadema. Hapo tutawaona wa maana. Kuliko Sukari ikipanda bei "Rostam". Mkikosa kura "Rostam" Umeme hakuna "Rostam" Mbowe anahodhi fedha kibao za akiba ya wazee na hataki kulipa kwa kisingizio kuwa kala hasara, nalo pia "Rostam".

Ikiwa sera na juhudi zenu ni za namna hiyo, hakuna mnalo/mtakalo liweza zaidi ya fitina na majungu.

Kama hamna uwezo wa biashara toweni mawazo "productive" ya kibiashara ili kuzuwia upandaji wa bei au majungu ndio yatasaidia kushuka bei za sukari?

unafikiri kuna sababu ya bei ya sukari kushuka?
 
wezi wanahold bidhaa ili upungufu uonekane na wewe unajidai unaleta theory za supply na demand hapa wizi mtupu

Ukosefu wa maarifa mwishowe unakupeleka kushutumu na kujenga chuki katika jambo ambalo halipo na si la kufikirika. Hao wezi walioficha sukari kama unawajuwa basi kuna uwezekano mkubwa ni washirika wako. Mbona hatukuoni kutuambia fulani ana Sukari kiasi fulani kaificha?
 
Hivi wew huchoki fitina kila kukicha? Hujuwi kuwa Tanzania ni soko huru? Na hujuwi kuwa Bei za vyakula zimepanda duniani?

Ni soko huru la kutengeneza mikataba feki na kuibia watanzania, kila mwizi yuko huru kuja Tanzania na kutuibia rasilimali zetu bila kikwazo, wakikaribishwa na jambazi sugu RA kwa baraka za JK, nadhani huu ndio uhuru wa soko la Tanzania unaouzungumzia wewe majimshindo.
 
MMK,
Ukiuma kidole kinachokulisha ujue unajiweka kwenye mashaka ya kupata mlo unaofuata.
Hao ndo wafadhili wakubwa wa chama cha "Wakoloni" wetu (wanalazimisha kututawala bila matakwa yetu). Hao ndo wanaowaweka madarakani. Watapata wapi gutz za kuwanyooshea kidole? Nani mwenye ubavu huo?
Mpaka tutakapopata viongozi, hapa namaanisha rais, atakayeingia ikulu bila kutegemea pesa za mafisadi, ndo serikali itapata nguvu ya kusema.
Kama ni soko huria kwa nini serikali isiruhusu sukari kuagizwa kwa wingi toka nje? Wanajua ikifanyika hivyo viwanda vya wafadhili vitakufa.
 
Ukosefu wa maarifa mwishowe unakupeleka kushutumu na kujenga chuki katika jambo ambalo halipo na si la kufikirika. Hao wezi walioficha sukari kama unawajuwa basi kuna uwezekano mkubwa ni washirika wako. Mbona hatukuoni kutuambia fulani ana Sukari kiasi fulani kaificha?

Yawezekana hauna uwezo wa kujua tunachozungumzia au kwa mapenzi yako kwa serikali hutaki kuona hata ambacho serikali yako yenyewe inaona ni tatizo:

By DAILY NEWS Reporter, 8th March 2011 @ 20:00, Total Comments: 0, Hits: 504

SUGAR producers say there is enough stocks of the commodity in the country, but some traders have plans to create artificial shortage for the purpose of lifting prices.

"It is a big lie to say Tanzania is now facing acute shortage," Tanzania Sugar Producers Association (TSPA) Chairman, Mr Robert Baisack told the 'Daily News.'

Most producers have stocks that may last up to the end of March. There is no need for the public to panic," Mr Baisack said.

He said Tanganyika Plantation Company (TPC) in Moshi is currently holding more than 15,000 tonnes. Other producers are also having adequate stocks, he added without revealing the figures.

He said prices of sugar in international markets were still high, but the imports could not cause prices to go beyond 2,000/-.

He said TPC ex-factory price is 69,500/- for 50kgs bag and after transport and other costs, the price could reach 77,700/- for 50kg bag.

This, he said, translates to 1,554/- per kg on reaching retailers who can comfortably sell the commodity at the recommended price of 1,700/- a kg.

He said Tanzania has annual 30,000 tonnes sugar supply deficit and the government recently allowed some traders to import the commodity.

Analysts say the deficit and anticipation for the ever rising sugar prices at international markets prompted traders including some distributors to hoard the commodity -- both imported and the one locally procured.

He said there are fears a lot of sugar is in warehouses as traders anticipate increased prices in international markets and the earlier announcement that importers will be allowed to bring in sugar duty free.

However, after the government changed its position by demanding the Value Added Tax (VAT) paid,there are notable changes in the domestic market.

Initially, some importers had asked the Prime Minister Mizengo Pinda during a meeting he had convened on February 21, to discuss the purported sugar shortage that they be allowed to bring in the commodity without paying import duty and VAT.

Mr Baisack said the rush for buying sugar at TPC has dramatically dropped by over 50 per cent from sales of around 360 tonnes a day to 125 tonnes over the last two weeks.

"This is an indicator of increased supply in the market," he said.
 
Ni soko huru la kutengeneza mikataba feki na kuibia watanzania, kila mwizi yuko huru kuja Tanzania na kutuibia rasilimali zetu bila kikwazo, wakikaribishwa na jambazi sugu RA kwa baraka za JK, nadhani huu ndio uhuru wa soko la Tanzania unaouzungumzia wewe majimshindo.

Na wale wanaokopa na kuzuwa kuwa wamepata hasara ili tu wasilipe mikopo yao, huku wenyewe wakiendesha mavogue na kukodisha ma helikopta, tuwaiteje?

Hivi mtu anaepata hasara ataendesha vogue? Na kukodi helikopta kwa kampenoi zake?

Hi nyinyi inawaingia akilini?

Si angenunuwa na Sukari basi aisambaze bei ishuke?
 
Hii sheria ipo kaka, ila inasimamiwa na PCCB; Nadhani unajua kuwa PCCB wapo usingizini tokea 2005.

We angalia humu JF Invisible kaleta taarifa za Mshauri wa kikwete wa Uchumi ukikokotoa miaka yake unapata kuwa alianza Darasa la Kwanza akiwa na miaka miwili (2); 1979 inawezekana kweli! hata kama vyombo vyetu vya dola wamebwiya unga!! Sheria ya kudanganya kwa vyeti ipo kwenye vifungu vya rushwa na pia ipo kama sheria ya forgery.

MKJJ hamna nchni hapa, huu uozo ni kuanzi Rais hadi vyombo vyake vya Dola vyote hovyo vimelala labda wananchni sasa wafikirie kuchukua madaraka mkono, maana kama dola ipo kwa ajili ya wachache maana yake nini?
 
Back
Top Bottom