Waliitwa "wahujumu uchumi"; Sasa Serikali inakaa nao mezani!

Mimi natoa maoni wewe upo kazini!!
Ukimaliza somo la soko huria rejea JF ili tuendelee na mjadala. Kwasasa smahani, ni- wrong person in wrong place at wrong time.

Have a good one Majimshindo.

Naona huna la kusema, hilo somo naomba kalisome wewe ulielewe "I am living it".

Hakuna sababu za kutaharuki kuhusu kupanda bei ama ya Sukari au kingine chochote kile, ni kutumia mbinu za kuweza kuishusha hiyo bei, kama Serikali imeshindwa, Jee, chama cha ushindani tena chenye kuongoza kambi ya upinzani bungeni, pamoja nanyi washauri wake! mna-mpango upi wa kuhakikisha mnatatuwa hili tatizo kwa haraka sana ili kusaidia jamii? Msiniambie mpango ni kuandamana!

Nimewapa ushauri wa bure, "action speaks louder than words", wakati kama huu ndio mngeonyesha uwezo wenu kwa vitendo, agizeni sukari, muisambaze mitaani kupitia mtandao wenu wa ofisi za chadema Tanzania nzima, na si bure, bali kwa gharama. Hapo aaah, mtakuwa vipenzi vya wa Tanzania, badili yakukaa humu JF na kuihusisha bei ya sukari na "Rostam". na kulalamika, serikali hivi serikali vile.

Nikukumbushe tu usemi wa John F. Kennedy "ask not what your country can do for you; ask what you can do for your country", huoni kuwa hii ndio fursa ya kutimiza huo usemi?
 
Kujitokeza kwa fitina? Si uje Tanzania ujumuike na wanaharakati wenzio kushusha bei za vitu kwa maandamano?

Hivi nawauliza, pesa za maandamano mnazo, pesa za kuagiza Sukari ya bei nafuu mkaisambaza nchini bila faida, kwa gharana tu, ili kusaidia wanyonge hamna? Au hilo hamuwezi? Nyie mradi mtie chokochoko tu?

Majimshindo Mimi nasikitika sana ninaposoma michango yako hapa Jf, nikiingalia sana comment yako hii nashindwa nikuweke kundi gani, nimeshindwa kukuweka katika kundi la mlalamikiwa wala mlalamikaji ila ni mvuruga mijadara.
 
Ezan, si mlalamikaji wala mlalamikiwa kama ulivyoshindwa pa kuniweka, huna kosa.

Kwanza, nadhani "mijadara" ulimaanisha mijadala? au sio? kama ni hivyo, napenda kukuhakikishia, mimi si nia yangu kuvuruga mjadala wowote ule, ila tu, naomba uniambie, hivi kuhusisha jina la "Rostam" na kupanda bei ya sukari, unaona kuwa ni sawa hivyo?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Na kutokana na kushindwa kwa serikali kutekeleza sheria ya uhujumu uchumi inatupa picha kuwa serikari ina wasupport wafanyabiashara zaidi kuliko raia walio wengi wanaoumia na upandaji wa bei hata swala la kupunguza bei kutoka 2000 hadi 1700 kwa mwananchi wa kawaida haimsaidii kitu.
 
mjomba,kazi unayo!lakini si vizuri kuleta siasa kwenye maisha ya watu!TAFAKARI
 
Soko la dunia?
Wakati wa mkapa soko la dunia halikuwepo? Hakika ww n miongoni mwa hayo mafis.
Lets stick on the reality, who is supposed to control price flactuations? na atawezaje angali hayo mafis ndo yamemuweka hapo madarakani?
 
mjomba,kazi unayo!lakini si vizuri kuleta siasa kwenye maisha ya watu!TAFAKARI

Maisha ya watu huendeshwa na siasa lakini si siasa uchwara za maandamano na kuhusisha mpaka jina la "Rostam" katika kupanda bei ya sukari, au hilo wewe unaliona sawa?
 
Hivi serikali ilikuzuwia wewe kuleta Sukari na kuuza? Kuilima na kuisambaza? Au Chadema hamna waziri kivuli wa kilimo? Wa biashara? Kama mnao si muanze na mkakati wa Sukari bei poa? Wafanya biashara si mnao? Au hamna?

Kaka jukumu la serikali ni nini?yaani serikali inawafanyia nini wananchi wake walioichagua kuhusu bei ya sukari kupanda??nani anapaswa kuhakikisha bei inakuwa affordable nchini?embu tueleze wewe unayejua "demand and supply"kinked demand and whatever!!
 
Na kutokana na kushindwa kwa serikali kutekeleza sheria ya uhujumu uchumi inatupa picha kuwa serikari ina wasupport wafanyabiashara zaidi kuliko raia walio wengi wanaoumia na upandaji wa bei hata swala la kupunguza bei kutoka 2000 hadi 1700 kwa mwananchi wa kawaida haimsaidii kitu.

Tatizo hapa si serikali kuweza au kushindwa, tatizo hapa ni kwa nini bei imepanda? muanzisha mada amefikia mpaka kumuhisha "Rostam". Haaa, ajabu.

Bei za vyakula zimepanda duniani kote, na jinsi hali za kisias zilivyo, bei zitaendelea kupanda. Jee, wa Tanzania, tufanye nini kwa haraka haraka kuweza kuhimili kupanda kwa bei? mawili, ama kufanya mikakati ya haraka kuongeza kipato, ama kufanya mikakati ya haraka kuongeza uzalishaji.

Hili la kuongeza uzalishaji naona ndio chaguo zuri na jema, na hili JK alishaliona zamaaaani, ndio maana aakaanzisha "kilimo kwanza". Kazi iliopo saa ni sisi wa Tanzania wenyewe, kutumia fursa zilizotolewa na mpango wa "kilimo kwanza" kuongeza uzalishaji, tukishindwa kutumia hizo fursa tusimlaumu mtu.
 
Inaonesha ni vipi mlivyokosa sera na kubaki ooh "unalipwa na Rostam", hivi huyu Rostam mnataka awafundishe mpaka basics za biashara? Au hanjuwi kuhusu "demand and supply".

Ushauru wa bure wa kusaidia wananchi: Chadema mna wafanya biashara na mna mabepari wakubwa tu kwenye uongozi, si agizeni sukari muijaze nchini kwa gharama, bei itashuka ikitaka isitake.

Hapo ndio itakuwa "action speaks louder than words" kwa upande wenu. Kuliko majungu na ufataani.

wee Majimshindo, umetumwa?? au wewe ndo rostam... heeee, huna hata chembe ya huruma...mweeeee
 
Kaka jukumu la serikali ni nini?yaani serikali inawafanyia nini wananchi wake walioichagua kuhusu bei ya sukari kupanda??nani anapaswa kuhakikisha bei inakuwa affordable nchini?embu tueleze wewe unayejua "demand and supply"kinked demand and whatever!!

Naomba soma post yangu #50 ina hilo jibu.
 
jamani tutambue kuwa asilimia kubwa ya viongozi wetu ni wafanyabiashara kwa hiyo wanaelewa kila kitu kinachoendelea na wao ndio wanao fanya hii biashara ya black markets

na wanafahamika hao viongozi kwa nini wasichukuliwe hatuwa? nani asiye juwa kuhusu umilikaji wa viwanda vya sukari vya kilombero na mtibwa? ni viongozi wakubwa sana na wanajuwa matatizo haya lakini kwa nini wamekaa kimya?
 
wee Majimshindo, umetumwa?? au wewe ndo rostam... heeee, huna hata chembe ya huruma...mweeeee

Unanichekesha sana. Na wewe si wa mwanzo kusema hayo kuhusu mimi. Hapana sikutumwa, najituma. Na hapana mimi si Rostam. Na si kweli kuwa sina chembe ya huruma. Huruma nilionayo haina mfano ndio maana hupenda kusema kweli na hutetea pale panapohitaji utetezi.

Mfano, kwa nini Rostam ahusishwe na kupanda bei ya sukari? sioni uhusiano na ndio maana namtetea.

Sipendi kuona wa Tanzania wakiteseka kwa kupanda bei za vyakula, lakini, natazama na nashauri njia mbadala badala ya "kusaka mchawi" na kwenda kuhusisha watu wasio husika.
 
Nchi ambayo viongozi wake wengi ni wafanyabiashara ama wana hisa ni vigumu kupambana na wahujumu uchumi..
 
Maisha ya watu huendeshwa na siasa lakini si siasa uchwara za maandamano na kuhusisha mpaka jina la "Rostam" katika kupanda bei ya sukari, au hilo wewe unaliona sawa?
Rafiki!katika hoja ya Mm cjaona jina Rostam,wewe ndiyo umemuweka,MM kasema wahujum uchumi,umejuaje kama rostam yumo?tujadili kam Watz,tuache kutafuta siasa,ukweli hali ni mbaya mkuu,VAA AKILI YA Mtz,Acha ya mtetezi wa rostam
 
Inaonesha ni vipi mlivyokosa sera na kubaki ooh "unalipwa na Rostam", hivi huyu Rostam mnataka awafundishe mpaka basics za biashara? Au hanjuwi kuhusu "demand and supply".

Ushauru wa bure wa kusaidia wananchi: Chadema mna wafanya biashara na mna mabepari wakubwa tu kwenye uongozi, si agizeni sukari muijaze nchini kwa gharama, bei itashuka ikitaka isitake.

Hapo ndio itakuwa "action speaks louder than words" kwa upande wenu. Kuliko majungu na ufataani
.

Hapo juu kwenye nyekundu uko sahihi kabisa.....ndio maana Chadema na wapinzani wengine makini wanataka kuiondoa CCM madarakani na kukamata serikali kwani haya ni majukumu ya serikali na wala si chama cha siasa!!
 
This nation cant prosper coz it only favours the prosperous . Chami anajaribu kutueleza janja ya kutumia mbinu mbalimbali za kiuchumi kutengeneza faida .Anaacha kujadili mantiki ya kutumika kwa janja hizo kwenye mazingira watanzania waliyonayo . Kama hao Tanganyika planatation wanahodhi tani zote hizo na hawataki kuzileta sokoni ni upumbavu mkubwa . Watawala wanabaki wabembelezaji kwa hawa wajanja badala ya kuchukua sheria stahiki . Mtu wa chini kila siku anakuwa mpokea bei tu ( price takers ) kwa hiyo hata kama wajanja wataspeculate bei iende kwenye 2000 mtu wa kawaida atapokea bei hiyo tu . Pato lake kwa siku huenda likaenda kwenye sukari .
 
Rafiki!katika hoja ya Mm cjaona jina Rostam,wewe ndiyo umemuweka,MM kasema wahujum uchumi,umejuaje kama rostam yumo?tujadili kam Watz,tuache kutafuta siasa,ukweli hali ni mbaya mkuu,VAA AKILI YA Mtz,Acha ya mtetezi wa rostam

Naona hujaisoma vizuri, rejea post ya mwanzo ya mjadala huu, nadhani para ya tatu kutoka mwisho, jaribu kusoma tena, utakuta.

Hivi Rostam anahusika nini na kupanda bei ya sukari? au nisimtetee kwa kuwa anaitwa "Rostam"?
 
Back
Top Bottom