Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
Kwema Wakuu!
Moja ya matukio ambayo mpaka leo sijayapatia majibu ni pamoja na tukio lililotokea mwaka jana katika chumba changu(kwani nimepanga chumba kimoja)
Nimeamka asubuhi nakuta kwenye mapazia nzi wametanda, ni wale nzi wakubwa wa chooni. Yaani ni wengi haswa.
Wametoka wapi sijui.
Sasa shemeji yenu kuamka, naye akakuta jambo hilo. Kama mjuavyo wanawake wanavyojishaua. Hofu, kinyaa na utatanishi vikatusonga.
Shemeji yenu akapendekeza tuwafukuze, nikamwambia achana nao. Kukawa na ubishi wa hapa na pale kwani ukipita walikuwa wanaruka ruka na kuna wakati wanagusa vyombo(si unajua tena chumba kimoja kimejaa mavyombo tele) nikamwambia achana nao.
Hiyo ilikuwa jumapili.
Kama kawaida tukawa tunaomba. Ni utaratibu wa nyumba yetu kuomba kila asubuhi na jioni. Na pia jumanne na Ijumaa ni siku ya maombi ikiwa ni pamoja na kufunga.
Basi bhana, ratiba zinaendelea. Jumatatu wakazidi zaidi. Shemeji yenu hofu ikaongezeka kuwa hiyo inasababishwa na nini na pia kuhofia ishu ya kiafya ukizingatia yeye kitaaluma ni Tabibu.
Jumanne tukaomba maombi ya maji ambayo huwa ni maombi yenye nguvu Sana. Tuliamka usiku saa saba kuelekea sàa nane. Tulipomaliza kuomba, tukamwagia yale maji pande zote cha chumba kama ilivyo kawaida. Kisha tukalala. Kesho yake tunaamka tunashangaa nzi wote wapo chini wamekufa.
Nini kimetokea hata sisi hatujui.
Alhamisi tukamuona panya akiwa anarandaranda, ni wale panya warefu alafu wembamba. Kaingiaje wakati sisi mlango hatufungui fungui.
Hatukuwaza mambo ya kishirikina au kichawi kama ilivyo kwa wale nzi. Haikuwa tishio sana.
Basi tukafanya mpango wa kununua dawa ya panya.
Cha ajabu wapitisha dawa za panya ukiwa na shida nao hawapiti mtaani kwako.
Jumamosi tunamkuta yule panya amekufa.
Nini kimemuua mpaka leo najiuliza.
Jambo moja la uhakika ni kuwa Maombi hata kama wapo wasio haamini lakini maombi yanafanya kazi.
Shahidi ni mimi mwenyewe.
Ingawaje siamini katika kuombewa hasa na mtu nisiyemjua kwa undani lakini naamini maombi ya mtu binafsi yananguvu zaidi kuliko maombi ya kuombewa.
Visa vingine kwa ajabu ajabu ninavileta hivi punde.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam