majohe kona
JF-Expert Member
- May 23, 2018
- 257
- 262
Hii brand mwanzo sikujua ila nilisikia tu nilivyoenda Nairobi nikakuta infinix ndio zimebamba Kenya kuliko huku kwetu na yangu nilikuta imebaki moja tu redmi 4x Dahhh nikaichek spec zake na bei ilikuwa 370k kwa bei ya kwetu tz nikachukua nimekuja ipenda na nitaipenda saana sababu ni tofauti na Tecno itel samsung HTC. ambazo nimewahi kuzitumia sisemi samsung ni Mbaya Hapana ila vitu ilivyonavyo xiaom sikuwahi kuviona kwanza betri ya mah 4100 haijawahi kupunguza ubora wake. Camera ya mp 13 iko safi kuliko mp 16 za tecno Duall app yaani kila app unaweza kuweka zikawa double, Fingerprint ya ukweli kabisa inayofanya kazi bila kustak app lock, kikubwa tena ni second space hii simu ya pili ndani ya simu moja. Water proof nimetumbukiza sana kwenye maji lakini chombo bado kipo imara. NAIPENDA SANA XIAOMI KWANGU NDIO BORA