Wale wasafiri wa zamani waliopita mlima Sekenke, unakumbuka nini?

Wale wasafiri wa zamani waliopita mlima Sekenke, unakumbuka nini?

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Achana na Sekenke ya sasa hivi iliyochongwa, kuna ile ya zamani ambayo haikuwa na lami. Mara ya kwanza napita pale 2006 kwanza tukashushwa kwenye gari wakabaki wazee, watoto na wagonjwa, bus likaanza kukata mlima. Kwakweli ilikuwa hali ya kutisha.

G9zH5v9WsAAAbqx.jpg
 
Nakumbuka mwaka 1988 nilimuona Mwigulu Nchemba Madelu akichunga mbuzi pembezoni mwa mlima huo.Enzi hizo alikuwa ni kijana mwema tu asiyejua hata kutamka neno "guys"!
 
Ule mlima ulikuwa ni balaa, ukiivuka ile kona ya S unapumua kidogo inabaki sasa kumpambana na breki zako kwenye ule mteremko mkali.
Kwa sisi tulioishi hapo mlimani kushuhudia ajali ilikuwa ni kila siku
 
Hivi ni kweli Kuna Magali mengi yamekwama hapo hadi leo yameshindikana kuyatoa?
 
Basi Zima huwa linakuwa na Hali ya ukimya mpaka kivuka hapo
 
Arusha kwenda Mwanza, wababe walikuwa kimotco na Jordan. 2004 n hv kuna watu walikula krismas pale, lori ilikwama ikaziba njia yote, mvua ikinyesha palikuwa panateleza sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom