Wale wa Mbeya Day

daaaah nami pia nakumbuka sana..but nimepita juzi juzi ngoma siku hizi imekuwa kama seminary..zamani ful machata ukutani siku hizi eti ukuta msafiiiiii...
 
Ee bana wewe uliyetoa k2 hiki cha mbeya dei ni Mkali,umenikumbusha mbali sana hasa wale waalimu waliokuwa wanoko kama si wazee wa noma(bakora).kwa kifupi napenda kuwakumbuka wachache. Mwl Mwakamele(marehemu),Mwl Mwandeko (marehemu) Mwl ZOYA mzee wa typing(marehemu) na bila kumsahau mbunge aliyepigwa chini na DENT wake kwenye uchaguzi wa ubunge jimboni Mbeya ndugu Benson Mpesya.Enzi hizo mie niko form 1 mr TWO alikwa form 4 mwaka 1991 mazee.
 
Hata mademu wa pale Mbeya dei walikuwa wakali si mchezo jamani.Lakini si unajua tena enzi hizo mchizi huna hata jero mfukoni utampta nani? basi hasira zetu tulikuwa tunazielekeza kupiga book kama hatuna akili nzuri vile na ndio maana tulikuwa tunapasua paper kinoma
 
Handeni;

Mzee Mwakamele na Zoya walifariki? lini tena jamani. Pia najua mwl Simwanza (geography) na yule mrefu wa Physics alikuwa anatokea Iyunga au Nzovwe pia alifariki (alikuwa anaitwa Labani)

Vipi unamkumbuka Seme wa hesabu na Mwakyembe wa Raia Mwema?
 
Napakumbuka Mbogoso-ndizi za kuchoma kwa katapela,kikundi kikali nyanda za juu kwa sanaa za maonesho,black devils-nani anawakumbuka? na kikubwa ziidi mwaka 1990 tulichukua ubingwa wa basketball wa mkoa wa kwanza kule Rungwe.
 
kwa wale waliosoma Mbeya Secondary School (Mbeya Day), Kama mpo humu jamvini hebu tukumbushana kidogo enzi zile. Ile awamu ya kwanza ya vigae na streams mbili 'A' na 'B' kwa form 1&2 na science na commerce kwa form 3&4 na ile awamu ya pili ya baada ya vigae kuondolewa na kuwa bati tupu na streams nyingi kuongezwa na kuanzishwa A level.
I was there from 1980 wakati wa vigae na streams mbili na Headmaster NISAJILE

Yaani hiyo title ndugu yangu, Wambea day! Dah!
 
Napakumbuka Mbogoso-ndizi za kuchoma kwa katapela,kikundi kikali nyanda za juu kwa sanaa za maonesho,black devils-nani anawakumbuka? na kikubwa ziidi mwaka 1990 tulichukua ubingwa wa basketball wa mkoa wa kwanza kule Rungwe.

Dah!ndugu yangu GIUSEPE umenikumbusha mihogo ya kukaanga pale mbogoso.ile ilikuwa ikilika sana wakati wa mapumziko saa nne. Pia nakumbuka zile bustani za mboga kule chini pembeni ya mto na msimamizi wake Mwl.Mela alikuwa mkali sana na masuala yanayohusu bustani.

Dah, pia namkumbuka Mwl.Mwamwaja alikuwa akifundisha physics.Pia tuition zilikuwa zinafanyika kule chini kwenye madarasa ya sanaa!!!!
 
Dah! Ndugu zangu mliopita mbeya day miaka hyo mmenifurahisha sana. Me nimesoma pale 2006-2009, now days hakuna shft za mchana wote wanaingia hasubui sisi ndo 2lmaliza na huo mtindo.
 
Namkumbuka Mwalimu Barnabas Mwakamele. Kilikuwa kichwa cha Literature miaka hiyo. Atakuwa kashastaafu
 
na sie wa Loleza.....
Mbeya kuzuri nilinjoi sana my stay mjini pale
 
Zoya Mwalimu wangu wa michezo! Nakumbuka Mwaka 1990 tulichukuwa ubingwa wa Basket ball Umiseta mkoa, mashindano yalifanyika Rungwe Sec, ulikuwa ni ubingwa wa kihistoria maana Sangu na Iyunga walikuwa wako fiti sana na katika ngazi ya wilaya walitufunga na tukaenda ngazi ya mkoa kama washindi wa 3. Huko upepo ulibadirika tukawachapa wote na kuwa mabingwa wa mkoa.
 
Nilidhani unaongelea siku ya wana mbeya kumbe ni shule!
Sorry napita tuu!
 
kwa wale waliosoma Mbeya Secondary School (Mbeya Day), Kama mpo humu jamvini hebu tukumbushana kidogo enzi zile. Ile awamu ya kwanza ya vigae na streams mbili 'A' na 'B' kwa form 1&2 na science na commerce kwa form 3&4 na ile awamu ya pili ya baada ya vigae kuondolewa na kuwa bati tupu na streams nyingi kuongezwa na kuanzishwa A level.
I was there from 1980 wakati wa vigae na streams mbili na Headmaster NISAJILE
Mastiff yuko wapi, Quit from the dark to light?
 
Back
Top Bottom