Wale mliooa wake zenu wakiwa na zaidi ya miaka 30 na wadada mlioolewa mkiwa na zaidi ya miaka 30 pia, karibuni kwa maoni na uzoefu wenu

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
17,134
40,699
Hello wakuu!,

Happy Sunday to everyone, karibuni kwa maoni yenu, je ni kweli ukiwa above 30yrs kuna possibility ya kutokuolewa kwa wadada? Sababu ni nini, kwani suala la ndoa linazingatia umri na si upendo baina yenu mnaotarajia kuwa wanandoa? Mliooa na kuolewa katika umri huo je kuna tofauti yoyote mnayoiona? Maisha yanaendaje? Ushauri wenu ni upi kwa wengine?.

Kumekuwa na maneno ya kutishana mitaani na hata baadhi ya threads humu kwamba mdada ukiwa na 30s ndiyo basi tenaa, sometimes hupelekea wadada kuolewa tu na mtu yeyote hata wasiyempenda sababu tu ya kigezo hicho kwamba she's in her 30s na anahofia atakosa ndoa.

Zamani mtaani kwetu nilikuwa nikisikia wakisema aunt fulani hajaolewa hadi leo, wanamshangaa, naona sasa kibao kimegeuka nimekuwa huyo aunt pia aah😂.

Karibuni na muwe na Jumapili njema...
 
Hello wakuu!,

Happy Sunday to everyone, karibuni kwa maoni yenu, je ni kweli ukiwa above 30yrs kuna possibility ya kutokuolewa kwa wadada? Sababu ni nini, kwani suala la ndoa linazingatia umri na si upendo baina yenu mnaotarajia kuwa wanandoa? Mliooa na kuolewa katika umri huo je kuna tofauti yoyote mnayoiona ? Maisha yanaendaje ?ushauri wenu ni upi kwa wengine?.

Kumekua na maneno ya kutishana mitaani na hata baadhi ya threads humu kwamba mdada ukiwa na 30s ndiyo basi tenaa, sometimes hupelekea wadada kuolewa tu na mtu yeyote hata wasiyempenda sababu tu ya kigezo hicho kwamba she's in her 30s na anahofia atakosa ndoa.

Zamani mtaani kwetu nilikua nikisikia wakisema aunt fulani hajaolewa hadi leo, wanamshangaa, naona sasa kibao kimegeuka nimekua huyo aunt pia aah😂.

Karibuni na muwe na jpili njema...
🐅 Usikate tamaa, my ex girlfriend kaolewa mwezi uliopita akiwa na 43 yrs
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo.

Kwa nini tunaipa ndoa uzito mkubwa ambao haistahili. Kwani maisha bila ndoa hayawezekani?

Unamkuta dada wa watu mzuri tu na tabia yake safi lakini analiwa ovyo na wanaume wasioeleweka na wasiompenda kisa kutafuta ndoa. Tena wengine shida yao ni kuvaa shela tu awakoge kina Mwajuma Nchokonoe kwenye vijiwe vya umbea vya kisasa vya instagram na whatsapp.

Ladies you can make your life beautiful even in absence of marriage.
 
Back
Top Bottom