Wakwapuliwa Mkoba Sinza Mapambano

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ndugu zangu

Kuna tukio limetokea hapa Sinza maeneo ya Mapambano njia ya nyuma kama unaenda Mwenge kwenye miti mirefu bar moja inaitwa kwa jimmy .

Kuna vijana 2 walikuwa wanatembea njiani mmoja kabeba begi lake la vitabu ghafla gari ndogo ikampitia kwa pembeni mtu aliyekwepo ndani ya gari akakwapua begi la yule kijana ambapo kulikuwa na simu na karatasi zake .

Huyo kijana alipiga kelele kidogo nilikuwa mbele yao nikajua labda ni tatizo lengine kumbe wenyewe wameibiwa bei lao kwahiyo ile saloon car nyeupe ikakimbia moja kwa moja

Kijana aliyeibiwa anaitwa Erick Thomas Jongela simu yake anasema ilikuwa na line 2 moja ni 0715 241204 na 0756 816 770 hizi line zilikuwa kwenye simu hiyo iliyokwepo kwenye begi lililoibiwa

Mwenzake mwenye simu anaitwa Fadhili no yake ni 0713 76 59 05

Kwa mtindo huu jamani muwe makini mnavyotembea na mabegi yenu pamoja na mali zingine zisivutie sana wahalifu hawa .

Nimetoa kisa Hichi kama tukio la kweli lililomkuta mtu naamini tigo pamoja na voda kwa kushirikiana na vyombo vya dola vitaweza kufuatilia simu ya kijana huyo na kuweza kupata taarifa zingine zinazohusiana na simu hiyo toka ilipozimwa mara ya mwisho

Usiku mwema
 
Dah hali ya uhalifu inazidi kuongezeka tu niliwahi kukwapuliwa mkoba wangu maeneo ya Aga khan hosp!
 
Dah inanikumbusha jinsi mke wangu alivyoibiwa hukohuko sinza ila mm ilikuwa pale Mori barabara iendayo meeda, mke wangu alilia sana maana pochi ilikuwa na simu pamoja na mshahara ndo alikuwa ametoka kuchukuwa ofisini kwake
 
Hii ni aina mpya ya uwizi!
Lakini in case akienda mbele akakwama, ni halali kuibonda bonda gari iwe chapati!
Sasa mtu unatumia gari kukwapua mfuko wa mtoto wa shule..huh!
 
HUU NDIO WIZI ULIOINGIA sana hapa mjini.. Wale wenye LAPTOP kuweni waangalifu na hawa VIBAKA jamani. WENGI WAMELIZWA maeneo ya IFM, CBE nk.
 
Kutunga tena wakati matukio ndo yameshika moto ..masaki chole road na mitaa ya o-bay watu wengi especially madada wamelizwa...kuna moja nilishuhudia live pale chole rd iliniuma sana...hawa dawa yao ni kuwapiga moto tu ukiwakamata
 
Hilo begi lilikuwa na zaidi ya simu na daftari............halafu kuna uwezekano huyo siyo mwanafunzi ni mtu wa deals na wale jamaa wa gari wanamfahamu fresh.......shtuka
 
Hi tatizo sio geni na liko within Telephone companies hata kabla ya polisi. Telephone companies zinaweza kusaidia polisi

kudhibiti simu zilbiwa tanzania kutumika ndani ya tanzania au kuwakama wahalifu linawezekana.

TCRA walazimishe kampuni za simu wawe na List ya kumonitor na ku block IMEI number ya simmu zote zilizoripotiwa kuibwa.

TCRA ilazimishe kampuni za simu ku share IMEI number za simu zilizoibwa ili ziwe blocked na kampuni zote.

Hii angalau itazuia simu iliyoibwa kuendelea kutumika tanzania na itapunguza idadi ya watu wanaonunua simu za mtaani/wizi

Bila TCRA kuwalazimisha hawa jamaa kuna resouces hawatumii ili kupunguza gharama za uendeshaji. wao wanachojali ni faida upende wao tu.

Sababu hivi sasa mtu unaweza kubiwa simu yenye simcard ya voda. Na aliyeuziwa. au mwizi akaweka simcard ya Voda na akaitumia vizuri tu. Utaripoti lakini hakuna kitakachotokea. Kuna resoruces hazitumiki kenye haya makampuni kwa faida yao

TRCA ilazimishe kampuni kuwa na rejister ya Black list Phone IMEI No. Na pia TRCA iifanye au ipewe nguvu ya kufanya Information system/Technical Auditing kwenye haya makampuni.
 
TRCA ilazimishe kampuni kuwa na rejister ya Black list Phone IMEI No. Na pia TRCA iifanye au ipewe nguvu ya kufanya Information system/Technical Auditing kwenye haya makampuni.
Hii mwana NUKTA.Na kwa kufanya hivyo kutapunguza wizi wa simu mtu akiiba hataweza kutumia handset.Kwa kweli bongo bado tupo nyuma sanaa kwenye uthibiti wa mawasiliano ya simu na internet ( i mean ICT -information Communication Technology)..ila naamini taratibu tutafika walipo wenzetu mana safari ni hatua
 
Hii ni kweli kabisa mimi mwenyewe nilishaibiwa H/bag yangu kwenye gari mitaa ya Morogoro road katikati ya mji. Hata wenye pikipiki hatari sana. Wanatumia magari hata wakati wakiiba vifaa vya magari ili wakikutwa tu wanakimbia na gari lao. Dar es Salaam siku hizi inatisha.
 
Back
Top Bottom