Wakuu nimeibiwa

Wakuu nimeibiwa

Wakuu leo moyo wangu wauma sana, nina kiofisi changu cha kidizaini tu hapa Kitaa, sasa kuna binti tupo hapo anasimamia.
Sasa leo nimetoka mishe mishe mida ya mchana nakuta pamefungwa nkapiga namba haipatikani, basi nkamuuliza dada nyumban vip umeachiwa ufunguo, kasema upo nkaenda fungua
Machale yakanicheza, nkasema embu ncheki hela kama ipo duh hamna kitu,
Basi nikatoka kama upepo hadi anapokaa Dah Mungu wangu keshachukua begi Lake kachapa lapa muda mrefu sana,
Yan Dah usiombe aisee yakutokee haya,
Hawa watu tunaowaweka kwenye biashara zetu tuwe makini sana, roho imeniuma lakini nimesimama kama chuma hadi watu wananishangaa

Hapa chumbani huwa nalala na kipande cha nondo, akigusa mtu mlango amekwisha
Mkuu pole kwa janga hilo, nakushauri ufokasi kutafuta solutions for paying the bills e.t.c

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni binti mdogo lakini mambo yake hakuna a nae amini, alikuwa anavuta hadi sigara
UnafAnya kazi na muhuni....ukiona demu anavuta fegi basi ujue hapo hasara bin hasara hakuna kinachompa hofu,Ila pole sana....jaribu kutafuta wafanyakazi kutoka pori hadi waje kujanjaruka ni muda mrefu ushatusua achana na wavuta fegi watoto wa mbwa!!
 
Kuna tatizo lolote baina yenu?
Mbali na kumuajiri mnao uhusiano wowote nje ya ajira rasmi?

Hua unafatilia maisha yake kwa ujumla jinsi anavyoishi?
 
SAIKOLOJIA YA MWIZI WAKO KWA WAKATI HUU:

1.Ana hofu.

2.Anajua unamtafuta.

3.Anajuta.

ATAKACHOFANYA:

1.Atajificha kwenda mbali na kuzima mawasiliano yote.

2.Akihisi yuko salama ata relax. Atarudisha mawasiliano yake hewani (most likely kupitia simu yake na namba yake halali) kisha atarudi mahali pake halali anapoishi.

3.Atatumia mawasiliano yake kutaka kujua na kuhakikisha kuwa wewe sio tishio tena kwake.

Anzia hapo. Utamkamata kama kuku.
Inakuaje akichukua laini inginee na akaishi maisha mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Ninaona kuwa kuna swali linaulizwa humu zaidi ya mara Nne na halipatu majibu la...Amekuibia shilingi ngapi??...au ameibia shs ndogo sana hata wee mwenyewe unaona udhia kuzitaja?
Kama ni hivyo, achana naye Usonge mbele na mambo yako mengine...Mungu atakujalia nyingine nyingi zaidi ya aliyokuibia!
Huwezi kujua, labda huko kwao mama yake amelazwa kwa kuanguka ghafla kwa stroke na hiyo hela uliyoibiwa ndio imeenda kumuokoa huyo mama na kwa namna moja ama nyingine ukawa umepata Baraka kwa kuokoa maisha ya mtu!...japo kwa kuibiwa !!!

Itoshe kujua kaibiwa, kujua kiasi mna mpango wa kumchangia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom