Wakuu naombeni ushauri wenu

Wakuu naombeni ushauri wenu

Labda ni kweli hana tabia nzuri au labdamaana nikizungumza nae kauli zake huwa zimejaa ucha mungu na mtaani kwao wanasema anajiona kwa sababu hana tabia ya kujichanganya sana na hata historia yake (kwa jinsi alivonihadithia) si mtu mhuni kwa kuwa alinambia alikuwa na wanaume wachache mno.
 
Mwanamke amekuwa na mahusiano na wanaume zaidi ya wanne na anajitapa kawaacha wotee yeye hajawah kuachwa

Mbona logic simple tu angekua anajitambua ningekupa ushauri wa kujenga ilaa apoo bomoaa tu kabla maumivu zaidi hayajakujia ..
Asante sana
 
Kaka , mapenzi ni furaha, amani , kusikilizana, ni kuwa na lugha moja, kuaminiana, kukojozana, maendeleo, kuvumiliana, kuwajibika , kuthaminiana, uwazi na ukweli, kuinuana, na kusaidiana.
Kwenye mapenzi, kama unampenda utamshirikisha mambo yako kwa uwazi.
Kama unampenda mpenzi wako kwa dhati huwezi zuia simu yako hasiangalie anachotaka kuangalia maana utakuwa wewe utakuwa muaminifu kwake na unaweza muachia simu yako masaa 24 bila kuwa na hofu yoyote , maana kila kitu unatakiwa uwe umekiweka wazi toka mwanzo wa mapenzi yenu ilj kuepuka mambo kama yaliyotokea "kwamba sijui hujafuta SMS za ma X wako".
Pili kama kweli unampenda hukupaswa kutumia nguvu kubwa kuzuia hasikague simu yako.
Hapo ndipo ulipoharibu na kumuonyesha kuwa wewe si muaminifu kwake wakati na yeye alikuwa amekupa moyo wake.
Ushauri , tulia endelea na maisha yako fanya kama hakijafokea chochote , hasipoonekana basi endelea na maisha yako
 
Kama ni ivy basi achana nae
Uyo ni pasua kichwa

Tafuta mwngine ambae mtaendana
Asante mkuu ila sijajua kama bado ananipenda maana kaniblock kila kona nikipiga na namba ngeni akipokea ananifokea 'sikutakiii' hii wiki ya tatu nimemchunia lakini kimya.
 
Hapo usijidanganye kama una mtu... 100% wakati unamtaka alishakua na mtu tayari, na kwako lilikua behewa la kupumzika tu,.. Kukuambia bila sababu kwamba muachane lilikua jambo gumu sana kukuambia kutokana na uongo wake wa mwanzo wa kukuficha kwamba hana mtu wkt ana mtu.... Na akikuchek ulivyomwamini na kumkabidhi roho yako aliona ni jambo gumu kukuambia,.. Ndio maana hiyo janja ya lete simu ilikua mpango kabambe wa kuhitimisha plan yake... Hata asingeiona sms yyt kwenye whatsapp angekutafutia kosa kwenye contact book namna ulivyo save majina,... Kwahiyo kwake ameshinda na yuko salama,.... Kitakachoendelea hapo iwapo utamfata na kumlazimisha, tarajia maumivu au kukukutanisha na mzee baba wake... Mshukuru Mungu kwa kila jambo, kwani kama mpango ulikua ni ndoa, basi mwanzo wa safari yenu kuelekea ndoa, sio nzr... Lipokee japo linauma lkn mshukuru Mungu,.. Yaelekea unasali sana mkuu,.. Sepaaaa
 
Unafeli sana kaka. Kwamba mapenzi yameadimika kiasi hicho???? Au katika maisha yako hjawahi kuachana na dem?? Halaf ni mwanamke gani uyo asie na adabu, kwmba hata hataki kuskiliza utetezi wowote ktoka kwako!! Ukilazimisha kumuoa uyo mtu atakupeleka kwa waganga ili apate 100% ya kukucontral. Sisi madaktari wa mifugo tunaita "ku-restrain" na akikuona uko mbishi sana atakuua. Achana nae tafuta mtu sahihi. Wanawake mtaani mbona wapo wengi sana kaka?? Au unakwama wapi???
 
Mi watu yenye wivu wa kijinga jinga huwa natupilia bondeni huko.

Yaani mtu unakasirika kisa nimekunyima simu au kisa nmekuzuia kuangalia picha za simu. Pumbervuùuuuu
 
Habari za asubuhi.

Kwa kweli nimefikia katika hatua ngumu sana katika mahusiano yangu (japo huenda isiwe sahihi kwa mimi kuita ni mahusiano kutokana na hali iliopo hivi sasa.

Ishu yenyewe iko hivi, Hapo katikati ya mwaka nilikutana na mwanamke mmoja katika mazingira fulani na kiukweli baada ya mazungumzo kadhaa nilimpenda sana, basi tukabadilishana namba tukaanza kuwasiliana, baada ya mawasiliano kwa muda fulani tukaanza mahusiano ya kimapenzi ambayo mwanzoni yalikwenda vizuri tu.

Lakini changamoto ikaanza kujitokeza, pale nilipogundua yeye ni mtu mwenye wivu sana au naweza sema hana imani sana nami kwakuwa alianza kukasirikia mambo madogo madogo sana kwa mfano akinipigia simu akaona inatumika lazima ataanza kuuliza kwa ugomvi, akiona niko nae nikawa najibu sms basi anakasirika anahisi nachati na mwanamke mwingine. Kuna siku moja nilimfanyia surprise anakokaa nikampigia simu nikiwa stand lakini kwa sababu sikumwambia ukweli kuwa ningekuja siku hiyo ili nimsurprise akaanza kunihisi labda nimetoka kwa mwanamke mwingine mpaka nilipomuelewesha akaelewa akanyamaza.

Sasa kisanga kimetokea juzi tumekutana zetu baa kunywa supu ya samaki. Mara ya kwanza tumepiga stori vizuri tu na tukaongelea mambo mbalimbali, baada ya muda hamu ya sex ikampata akanambia anataka nikamwambia hapa tuko bar subiri kwanza tukitoka. Hakunielewa akaanza kunikalia mapajani, nikamwacha alipoanza kunilalia akiwa amekaa mapajani nikamwambia kaa kwenye siti yako tukitoka tutakwenda ku-do. Nilipomwambia hivyo alikubali ila ALIKASIRIKA SANA, kwa hasira akanambia lete simu yako niikague, akaanza kuikagua akakagua sms za kawaida akaona hamna chochote cha kunikamatisha.

Akataka kukagua na whatsapp, nikamwambia whatsapp hapana. Kiukweli nilikataa si kwa sababu nilikuwa na mwanamke mwingine, la hasha, nilikataa kwa sababu sikufuta sms za whatsapp za ma X wangu(mimi ni mvivu kufuta sms za whatsapp) hivyo niliogopa ikiwa angeziona na kwa jinsi nilivyomjua asingenielewa hivyo nilikataa yeye kukagua sms za whatsapp akawa anang'ang'ania nikamnyang'anya simu akawa anang'ang'ania tena huku akiniambia 'usiponiachia nikague simu yako basi jua mi na we ndo basi', nikamnyang'anya akaondoka kwa hasira. Kujaribu kumfata sikumuona.

Baadae nikaanza kumpigia simu ikawa inaita hapokei alivoona kero akaniblock, nikapiga kwa namba ingine alipogundua kuwa ni mimi akaikata na hakupokea tena. Nikamfata anapoishi nilopofika mlangoni alipogundua kuwa ni mimi akafunga mlango kwa ndani halafu KIMYA. Tangu hapo akawa hataki mawasiliano nami, nikaja nikampigia kwa namba ingine akapokea akanambia 'sitaki mahusiano nawewe' akakata nikapiga tena akapokea akasema 'sitaki hata mawasiliano na wewe na tukionana kila mtu kimpango wake, endelea na wanawake zako.'

Sasa ndugu zangu huko ni KUACHWA, kinachoniumiza ni kuwa naamini sina kosa na kwa kweli sina/sikuwa na mwanamke yeyote zaidi yake. Na mie bado NAMPENDA SANA TENA SANA, mpaka nimefikia hatua hii ya kuleta hapa sina la kufanya kwa kuwa hapokei simu yangu wala hataki mazungumzo nami na wala simjui ndugu yake yeyote ningemjua ningemwomba anisaidie kwa kweli kwa sababu nampenda sana, tulipanga tufunge ndoa mwakani 2020.

Na tulikuwa tunapanga maswala ya kutambulishana. Sasa naombeni mnishauri nifanyeje ndugu zangu kwa kuwa mie inaniuma sana nimejaribu kumwambia kuwa nili kataa asikague simu yangu kwa sababu hangeamini ambacho ningemwambia lakini hakunielewa.

Mnisamehe kwa kuandika maneno mengi sana kwa sababu nilitaka kueleza kila kitu.

Naomba mnishauri wakuu.
pole muwe mnaangalia wanawake wasio na vichaa
 
Sounding kama vile unaficha baadhi ya mambo. Inshort wewe siyo mwaminifu kwenye mahusiano. Tafuta ambaye atakuelewa jinsi ulivyo.
 
Hapo usijidanganye kama una mtu... 100% wakati unamtaka alishakua na mtu tayari, na kwako lilikua behewa la kupumzika tu,.. Kukuambia bila sababu kwamba muachane lilikua jambo gumu sana kukuambia kutokana na uongo wake wa mwanzo wa kukuficha kwamba hana mtu wkt ana mtu.... Na akikuchek ulivyomwamini na kumkabidhi roho yako aliona ni jambo gumu kukuambia,.. Ndio maana hiyo janja ya lete simu ilikua mpango kabambe wa kuhitimisha plan yake... Hata asingeiona sms yyt kwenye whatsapp angekutafutia kosa kwenye contact book namna ulivyo save majina,... Kwahiyo kwake ameshinda na yuko salama,.... Kitakachoendelea hapo iwapo utamfata na kumlazimisha, tarajia maumivu au kukukutanisha na mzee baba wake... Mshukuru Mungu kwa kila jambo, kwani kama mpango ulikua ni ndoa, basi mwanzo wa safari yenu kuelekea ndoa, sio nzr... Lipokee japo linauma lkn mshukuru Mungu,.. Yaelekea unasali sana mkuu,.. Sepaaaa
Nashkuru sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom