Wakuu naombeni ushauri wenu

Wakuu naombeni ushauri wenu

Basi tulia kama unanyolewa.
Akunyoe staili zote ***** halafu akuache urudi hapa na sredi ingine.
I will be watching you. Ukirudi hapa kulialia tena nipo na wewe mwanzo mwisho.
Kiukweli mimi ndo najaribu kurudiana nae ilhali yeye anasema baada ya yale yaliyotokea ameniacha.
 
Basi tulia kama unanyolewa.
Akunyoe staili zote ***** halafu akuache urudi hapa na sredi ingine.
I will be watching you. Ukirudi hapa kulialia tena nipo na wewe mwanzo mwisho.
Kiukweli mimi ndo najaribu kurudiana nae ilhali yeye anasema baada ya yale yaliyotokea ameniacha.
 
Asante kwa kunishauri. Nimejaribu kukaa kimya wiki moja sasa.

Sijui kama atakuja kunitafuta tena maana alinambia yeye akishamuacha mwanaume huwa harudiani naye tena kwahiyo akasema nikubali kuwa hanitaki.
Fanya mambo yako utajiumiza tu na hutobadilisha chochote, achana nae ulipokosea ni kumuonesha kuwa hujiwez kwake na ukiendelea kumnyenyekea atakukomesha.
 
1: kwa nini ubaki na ma SMS ya wasap ya x zako? Ili iweje wakati ushaachana nao?
2: mmmh eti wewe ni mvivu kufuta SMS za ma x za wasap? Kawadandanye watoto wenzie.
3: kitendo cha kutofuta SMS na no ya simu za x maana yake bado unampenda, wakubwa wenzangu hii kitu mnaitambua. Note: usiingie kwenye mahusiano mapya kama unajua bado unampenda x, futa kila kitu then move on, mpaka mtu anakuwa x inamaana no relationship btn u.

Sawa nashkuru ila mi ndo yashanikuta tayari naomba ushauri
 
Hapo kwenye swala la kutokufuta mawasiliano ya ex
Unajua tuko tofauti kuna kina sie ambao yan tukiachwa tunakubali hali tumeachwa tunafuta sms calls namba za sim picha emails na kila kitu kinachomhusu ex isipokua tu blocking hatufanyi tunaona ni udhaifu kublock mtu
Kuna ambao utakula block kote kote
Kuna ambao kama mtoa mada japo unaweza kuona haimake sense sababu mtu anaweza kuishi vipi na sms za mtu aliekwisha achana naye ila utambue kila mtu ana namna ya kuhandle break up kwa mtindo anaoujua yeye waweza kuta kweli wameachana n sms tu hajafuta
Asante kwa kunielewa dada angu.
 
Habari za asubuhi.
Kwa kweli nimefikia katika hatua ngumu sana katika mahusiano yangu (japo huenda isiwe sahihi kwa mimi kuita ni mahusiano kutokana na hali iliopo hivi sasa.
Ishu yenyewe iko hivi, Hapo katikati ya mwaka nilikutana na mwanamke mmoja katika mazingira fulani na kiukweli baada ya mazungumzo kadhaa nilimpenda sana, basi tukabadilishana namba tukaanza kuwasiliana, baada ya mawasiliano kwa muda fulani tukaanza mahusiano ya kimapenzi ambayo mwanzoni yalikwenda vizuri tu.
Lakini changamoto ikaanza kujitokeza, pale nilipogundua yeye ni mtu mwenye wivu sana au naweza sema hana imani sana nami kwakuwa alianza kukasirikia mambo madogo madogo sana kwa mfano akinipigia simu akaona inatumika lazima ataanza kuuliza kwa ugomvi, akiona niko nae nikawa najibu sms basi anakasirika anahisi nachati na mwanamke mwingine. Kuna siku moja nilimfanyia surprise anakokaa nikampigia simu nikiwa stand lakini kwa sababu sikumwambia ukweli kuwa ningekuja siku hiyo ili nimsurprise akaanza kunihisi labda nimetoka kwa mwanamke mwingine mpaka nilipomuelewesha akaelewa akanyamaza.
Sasa kisanga kimetokea juzi tumekutana zetu baa kunywa supu ya samaki. Mara ya kwanza tumepiga stori vizuri tu na tukaongelea mambo mbalimbali, baada ya muda hamu ya sex ikampata akanambia anataka nikamwambia hapa tuko bar subiri kwanza tukitoka. Hakunielewa akaanza kunikalia mapajani, nikamwacha alipoanza kunilalia akiwa amekaa mapajani nikamwambia kaa kwenye siti yako tukitoka tutakwenda ku-do. Nilipomwambia hivyo alikubali ila ALIKASIRIKA SANA, kwa hasira akanambia lete simu yako niikague, akaanza kuikagua akakagua sms za kawaida akaona hamna chochote cha kunikamatisha.
Akataka kukagua na whatsapp, nikamwambia whatsapp hapana. Kiukweli nilikataa si kwa sababu nilikuwa na mwanamke mwingine, la hasha, nilikataa kwa sababu sikufuta sms za whatsapp za ma X wangu(mimi ni mvivu kufuta sms za whatsapp) hivyo niliogopa ikiwa angeziona na kwa jinsi nilivyomjua asingenielewa hivyo nilikataa yeye kukagua sms za whatsapp akawa anang'ang'ania nikamnyang'anya simu akawa anang'ang'ania tena huku akiniambia 'usiponiachia nikague simu yako basi jua mi na we ndo basi', nikamnyang'anya akaondoka kwa hasira. Kujaribu kumfata sikumuona.
Baadae nikaanza kumpigia simu ikawa inaita hapokei alivoona kero akaniblock, nikapiga kwa namba ingine alipogundua kuwa ni mimi akaikata na hakupokea tena. Nikamfata anapoishi nilopofika mlangoni alipogundua kuwa ni mimi akafunga mlango kwa ndani halafu KIMYA. Tangu hapo akawa hataki mawasiliano nami, nikaja nikampigia kwa namba ingine akapokea akanambia 'sitaki mahusiano nawewe' akakata nikapiga tena akapokea akasema 'sitaki hata mawasiliano na wewe na tukionana kila mtu kimpango wake, endelea na wanawake zako.'
Sasa ndugu zangu huko ni KUACHWA, kinachoniumiza ni kuwa naamini sina kosa na kwa kweli sina/sikuwa na mwanamke yeyote zaidi yake. Na mie bado NAMPENDA SANA TENA SANA, mpaka nimefikia hatua hii ya kuleta hapa sina la kufanya kwa kuwa hapokei simu yangu wala hataki mazungumzo nami na wala simjui ndugu yake yeyote ningemjua ningemwomba anisaidie kwa kweli kwa sababu nampenda sana, tulipanga tufunge ndoa mwakani 2020.
Na tulikuwa tunapanga maswala ya kutambulishana. Sasa naombeni mnishauri nifanyeje ndugu zangu kwa kuwa mie inaniuma sana nimejaribu kumwambia kuwa nili kataa asikague simu yangu kwa sababu hangeamini ambacho ningemwambia lakini hakunielewa.
Mnisamehe kwa kuandika maneno mengi sana kwa sababu nilitaka kueleza kila kitu.
Naomba mnishauri wakuu.
.
Pole sana mkuu kwa mastress
Apo anakupima imani yako kam ww uta react aje maana anajishaua wakat bado anakupenda
 
Huyo dada hakupendi.... Itakua ngumu kuukubali ukweli huu kwa upande wako ila habari ndio hiyo.....
Umemuambia ukweli mchungu, hapo alikuwa anamtafutia tu sababu!!

Angekuwa anampenda kweli hilo siyo kosa la kumnunia 3 weeks, watu wanafumania and after few days anasamehe na game anatoa kama kawaida!!

Mkaka, kubali hupendwi and next time usiyakurupukie mapenzi hivyo, wenzio tunaenda kwa mwendo wa kunyata!!
 
Kwa mateso hayo hapo bado hauja muoa, sasa siku ukimuoa sindio ndani patakuwa kama jela..!!
Mkuu, minaona huyo dada ni muathirika wa mapenzi, na umeingia kwenye mahusiano na mtu ambae amekuwa akijeruhiwa sana kwenye mahusiano.
Sasa kwakifupi ni kwamba piga chini huyo mwanamke kwasababu bila ya kufanya hivyo ipo siku hautoipata tena nafasi ya kuomba ushauri kama hivi, na utakuwa tayari umechelewa.
 
Pole mkuu. Ushauri wangu achana nae kwamda huu ila kabla yakuachana nae muandikie sms ndefu jieleze hali halisi, mueleze hisia zako kwake, mueleze nini malengo yako kwake. Ukishafanya hivyo relax muachie mwenyewe aamue nausimtafute tena naikibidi muage mwambie huna jinsi nauamuzi aliochukua. Naamini ukipiga kimya kabisa mwisho wasiku atakutafuta mwenyewe
 
Pole sana mkuu, unapozidi kufeli na kujiumiza ni unavyozidi kumtafuta acha kumtafuta unampa kiburi na atakuendesha ad upate vidonda vya tumbo, be a man step out of that shit relationship atakupotezea mda wako kaa kmya asipojirudi basi ni mwanzo mpya, kuishi ni mara moja ila kuna aina nyingi za kuishi jali afya ya moyo wako hakuna wa kukufanyia hili.
Asante sana kwa kunishauri japo kumsahau ni changamoto kubwa kwangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom