wakuu kutokana na mafuriko usafiri wa baadhi ya sehemu dar upo hivi;

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
kama Unaenda tegeta, africana, mbezi beach,unatoka k/koo, ubungo au posta, unapanda gari la mwenge unashuka. ukisha shuka unapanda gari ya mwenge to bondeni kawe unashuka lakini kwa sababu bondeni hamna sehemu ya kugeuzia unashukia njia panda ya kawe. ukifika njia panda ya kawe unatembea kwa miguu unavuka daraja, ambapo ukishavuka ndo unakutana na magari ya tegeta, ununio, bagamoyo n.k. so kama unapanda daladala andaa nauli ya kutosha. ni hayo tu. poleni sana. Mia
 
hapa ndo uelewe kuwa kitengo cha maafa katika serikali hakifanyi kazi kwa mda hadi sasa kungetakiwa kuwepo tayari emergency taraja
 
Si kitengo cha Maafa tu, bali ni vitengo vyote vya serikali havifanyi kazi, tusipokaa choncho kuikataa serikali ya iliyopo ipo siku tutajuta kuzaliwa.
Serikali yetu ni noma jamani; wanajaliana tu wao kwa wao.
 
Poleni sana. Kazi ya mola haina makosa. Mungu yu pamoja nanyi.
 
Jamani maafa yametokea wakati viongozi wengi wa serikali wameshaenda likizo ya mwisho wa mwaka.
 
Yaani hata wanajeshi wanashindwa kujenga madaraja ya imergency ili maisha yaendelee!!! ama kweli hili linchi limedoda, sasa ni kitu gani serikali hii inaweza kukifanya naona kina Ritz na FF wanaweza kutusaidia kutupa jibu!. Mungu ibariki Tz na watu wake ila usibariki viongozi wake. Miaaaaaaaaa!
 
kama Unaenda tegeta, africana, mbezi beach,unatoka k/koo, ubungo au posta, unapanda gari la mwenge unashuka. ukisha shuka unapanda gari ya mwenge to bondeni kawe unashuka lakini kwa sababu bondeni hamna sehemu ya kugeuzia unashukia njia panda ya kawe. ukifika njia panda ya kawe unatembea kwa miguu unavuka daraja, ambapo ukishavuka ndo unakutana na magari ya tegeta, ununio, bagamoyo n.k. so kama unapanda daladala andaa nauli ya kutosha. ni hayo tu. poleni sana. Mia

Halafu unaambiwa serikali imetumia bilioni nyingi tu kusherehekea uhuru wa Tz, swali ni je uhuru gani huo wakati tunarudi nyuma?
 
Si kitengo cha Maafa tu, bali ni vitengo vyote vya serikali havifanyi kazi, tusipokaa choncho kuikataa serikali ya iliyopo ipo siku tutajuta kuzaliwa.
Serikali yetu ni noma jamani; wanajaliana tu wao kwa wao.

Kweli wanajaliana wao kwa wao wakikohoa kidogo wanahi airport yao muhimbi wanaandikiwa transfer to India
 
Back
Top Bottom