Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 4,946
- 12,515
Sea taxi ni usafiri wa boti au meli ndogo zenye kubeba abiria kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ndani ya bahari, na ndani ya boti abiria huweza kupata sehemu za burudani kama televisheni, eneo la wazi, mgahawa na sehemu ya mkutano.
Hii imekuwa ikifanyika katika nchi mbalimbali mfano kwa wenzetu Thailand au India wamethubutu kuchonga hata za mbao na kuziwekea injini.
Kwa jiji letu la Dar es Salaam sea taxi inaweza ikafanya kazi kwa njia hizi Kijichi - Posta, Kibada - Kigamboni ferry na Tegeta - Mbezi Beach - Kawe - Msasani - Masaki Oysterbay - Ferry.
Sea taxi itakuwa ni usafiri mbadala au usafiri ambao ni luxury mtu atauchagua ili atalii na atumie muda mfupi kukwepa foleni na adha ya joto barabarani.
Hii huduma itakuwa ni kivutio kikubwa na chachu ya kuwafanya wageni wafurahi kutembelea eneo la bahari ndani ya jiji.
NAMNA YA UENDESHAJI
Huduma ili iwe nzuri na ya kuvutia inabidi serikali itangaze tenda na kampuni itayoshinda ipewe zabuni ya kununua boti zitakazoweza kufanya huduma.
Huduma ziwekwe kwa madaraja na ikiwezekana kuwe na application ambayo itasaidia watumiaji kufanya booking private mfano mtu hatayeitaji Sea Taxi kwa ajili ya makutano binafsi au V.I.P services.
"Sea never dry"