Ikitotanzila
JF-Expert Member
- Sep 22, 2020
- 1,409
- 2,263
Naomba msaada wajameni maana huwa siwezi kuvitofautisha kabisa.
Bajeti ya serikali huwa ni andiko linaloonesha mapato na matumizi ya serikali. GDP ni pato ghafi la taifa. Linahusisha matumizi ya serikali, watu binafsi, uwekezaji na mizania ya biashara (hasa tofauti ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na zile zinazoagizwa kutoka mataifa ya kigeni). Kwa kifupi GDP ni pana kuliko bajeti ya serikali, japokuwa vina uhusiano kwa vile matumizi ya serikali ni sehemu ya GDP.
Kuongezea GDP ni pato ghafi la ndani, na Bajeti ni mchangako wa Pato la ndani na nje, misada, mikopo na ruzuku.Bajeti ya serikali huwa ni andiko linaloonesha mapato na matumizi ya serikali. GDP ni pato ghafi la taifa. Linahusisha matumizi ya serikali, watu binafsi, uwekezaji na mizania ya biashara (hasa tofauti ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na zile zinazoagizwa kutoka mataifa ya kigeni). Kwa kifupi GDP ni pana kuliko bajeti ya serikali, japokuwa vina uhusiano kwa vile matumizi ya serikali ni sehemu ya GDP.
Ghafi maana yake nini, sisi wengine tupo Matombo huku ndani ndaniKuongezea GDP ni pato ghafi la ndani, na Bajeti ni mchangako wa Pato la ndani na nje, misada, mikopo na ruzuku.