Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,473
- 757
- Thread starter
-
- #161
Enzi zile duh........raha,
Kwenye mchakamchaka ni saa kumi usiku...... kuwahi namba, Hakuna kupiga kelele darasani, mambo ya table (hesabu za kuzidisha za kushtukizwa na teacher)....kumi na mbili mara sitaaaaaa mwl anakulamba fimbo mpaka utoe jibu.
Gwaride kwa filimbi:
Baba paka aliyesema.....
sisi hapa, ni watoto wadogo, twajifunza siasi ya ujamaaa, mwalimu wetu katfundisha adabu na heshima mbele ya wazaia wetu!.......
Oh, vijana, vijaaaana, vijana,vijana tayari, ..kulitumikia, taifa, taifa Tanzania, oh Walimu.......
Nyerere yupo ukiona kundi la siasa, Nyerere yupo,...Kawawa yupo......nk
Sisi tunataka kuwasha mwenge, tunataka kuwasha mwenge,
Naapana naahidi mbele ya chama,
Naipenda sana shule yetu
shule yetu imejengwa kilimani
Azimio la Iringa, lasema siasa ni kilimo, wananchi tushike majembe tukalime, tupate mazao bora.
Tumeuona mpilipili na maua yake ......
Ahaa, chama cahetu cha mapinduzi cha jenga nchi, Nyerere ahaaaa, Karume cha jenga nchi...
Nyimbo za mchakamcha, darasani na kuhamasishana
Iddi Amiri akifa, mimi siwezi kulia,ntamtupa kagera awe chakula cha mamba.
Mwenge huo mwenge.....mbio mbio
twende tukawinde leeeeo, tukawindeee vipepeo
Hasiependa shule ni mjinga kabisa
Kikojozi na nguo twaichoma moto!
Baba yake Juma ametia vilaka matakoni mwake vinauluzana umekuja lini....
Kwaya:
Karibu sana shuleni kwetu mtukufu Mkuu wetu wa Mkoa,
Ngonjera:
Hodi hodi uwanjani,
Vitabu:
Juma na Roza
Kalumekenge
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
siku ya gulio Katelelo
Kibanga ampiga Mkoloni
Brown ashika tama
Safari yenye mkosi
Nondo mla watu
Maarifa
Barua za mapenzi zinachorwa Mkuki na moyo, unaanza na "Kwako Dada Mpendwa..."
Barua za mapenzi zinafichwa kwenye mikebe
Barua za mapenzi zikipatikana zinasomwa mstarini.
kumbebea mwalimu maembe
kumpelekea mwalimu misigo yake kwa demu
Kuchunguliwa wanafunzi wa kike wakiwa ****** au kwa vioo
Kazi za nje
Kumwagilia Busatan za shule
Kufyatua tofari
Kuja na nyasi shuleni
kuleta maji kumwagia viunga vya shule kuondoa vumbi
kulima mashamba ya Mwalimu, DRDD, Mkuu wa Wilaya nk.
Kutoka shule
sasa, sasa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri tutaonana keshoooooo!
Duh miaka ya 80 -90 kaka, mimi nilikuwa time keeper, sasa rafiki zangu walikuwa wananiambia nigonge kengere kabla ya muda ili tuwahi kucheza mpira - mpira wa makaratasi.
Darasa la tano namkumbuka mwalimu mmoja wa sayansi, akija darasani lazima aje na fimbo kama 10 hivi, anaanza kukumbushia somo la mwisho, anayeshindwa anapita mbele... anangoja super six....aisee kweli shule ilikuwa chungu kipindi chake kikifika.
Kuwahi number saa moja pia ilikuwa tatizo kwangu, ukicheliwa tu unakuta inakuwa imekula kwako.....moja...mbili.....tatu....nne etc
Mkaguo wa mwili ilikuwa soo, Kwa wale wamesoma vijijini ilikuwa hatari kukutwa na chawa, nguo hujafua, magaga ya miguu etc. Mimi nilikuwa ktk bendi ya shule nakumbuka wimbo wa mkaguo ulikuwa unaitwa kwa filimbi na bendi .... as Baba pakaa akasemaa twendeni tukawinde.....
Mwalimu Mkuu alikuwa mzee anaitwa Bebenya.... sasa lazima muimbe kumsifika kila siku asubuhi na jioni kabla hamjaenda nyumbani - tuliimba twampenda bembenya twampenda bembenya twampenda bebenyaaa eeeee aiyelele twampenda bebenyaaaa - tukae kwa amani tukae kwa amani tukae kwa amani eeee.....
Haraiki ya zile nyimbo za utaifa tumeziimba sana, hawa walimu waliokuwa wametoka JKT wakati huo walikuja na vinyimbo kibao walikuwa wanatufundisha - Nakumbuka wimbo mfupi mmoja siku ya kumaliza darasa la saba picknic , tulichapishiwa vyeti kila mmoja aliitwa mbele kuchukua cheti kwa mgeni rasmi mratibu tarafa..huku shule nzima ikiimba wimbo huu
Ndugu... ( anatajwa mhitimu darasa la saba)
Simama ukachukue cheti chakooo
kiitikio - Ukachukue Cheti, Ukalijenge taifa, taifa lakungoja ukatende uliyoangizwaa ..
Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana, best student wa mwaka pia tulikuwepo wazee wa mizawadi.
aisee acha tu, siku ya mkesha wa x-mas miaka hiyo, majibu yanakuja kijijini sita tumefaulu - mimi Moshi tech, Mengine Tabora Boys, Girls, na Mazengo
acha bwana, mkuu unaturudisha enzi za utaifa kwa kweli kakaa - tumetoka mbali wengine.
Mfunyukuzi kweli unafukunyua.
ha ha ha, mi nakumbuka vilikuja vitoto toka mjini viwili vinavaa safi uniform smart, tatizo havikuwa na akili sasa navionyesha hesabu na sayansi, asubuhi vinaniletea maadazi- saa 4 vinanipe hela kila siku. aaaa kile cha kiume kwa nini kisiwe ki shemeji - akili ikanisaidia nikavuta mzigo fastaa - hapo darasa la tatu.
aaaa kile cha kiume kwa nini kisiwe ki shemeji - akili ikanisaidia nikavuta mzigo fastaa - hapo darasa la tatu.
kuna kamwalimu ka hesabati kalikuwa kananambia nikapenyezee bange, hako kamwalimu kalikuwa kanavuta kuliko bobu male! kama hujakapenyezea bange kanakuloga wewe na familia yako! kakishavuta bange zake mpaka 1+1 utakaona kanatafuta kalkuleta.
hee mwenzetu umekula chumvi nyingi hongera
umesahau cha cha cha,au zile raba za boraMabraza men wa enzi hizo walikuwa wakivaa taugh boot aina ya BENQ na raba za kina Ken Mkapa na suruali za LEGGS wakati kina FirstLady wa enzi hizo walikuwa wanatoka na raba za Leso na magauni yenye mikanda ya vipepeo bila kusahau sie wagumu tulikuwa tunatune Kung-fu shoez teh teh
nilikuwa mvivu sana kuamuka asubuhi mama akiniamsha nilikuwa namdanganya leo tumeambiwa twende mchana, sikumoja nikakosea step nikamwambia shule imefungwa eebwanaa.. alinibeba kimsobesobe hadi shuleni nikakuta wenzangu wako mstarini mwl mkuu alikuwepo nililambwa mboko kwanza mama akaja mwl wa darasa akaja mwl wa zamu mwisho mkuu mwenyewe wiki nzima matak o yakawa yamevimba sikurudia tena.
Nilikuwa nasubiri wakati wa mapumziko kukunua bagia,mabumunda,visheti na ubuyu,na iskirim alafu unatemea mate ili usiombwe
Hii..." Saaa..imefikaaa..ya kwenda nyambani....mama amepikaaa...wali na nyama....Saa imefika ya kwenda nyumbani Mama amepikaaa wali na nyama.......Kwaheri mwalimu .....kwaheriii...tutaonana keshooooooooooo..."basi hapo ni Mbio mtindo mmoja madarasa ya udongo...basi wengine tunaruka madirishani.....hapo jumatatu lakini SHATI halitamaniki...daaaah...aiseee...nakumbuka mbali..mno....daaaah..Wandugu,
Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.
Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;
" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."
Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.
Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;
" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....
Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Tatizo la kizazi cha sasa ni chipsi kuku, simu, kuangalia movie, series, kuangalia uchafu kwenye internate basi unafikiri akili zitatoka wapi sana sa wanachofikiria ni kuiba pepa tu ili wafaulu.Shule zetu nyingi tulizosoma zilikuwa hivi na akili zilikuwemo leo hii mazingira mazuri na facility kwenye shule nyingi hasa za mjini zipo ila mitoto bomu bomu sijui tatizo ninini hasa au ndio hivyo tena nchi imeharibika na haina mwenyewe kuanzia chini hadi kwa wenye nchi???
Enzi zile duh........raha,
Kwenye mchakamchaka ni saa kumi usiku...... kuwahi namba, Hakuna kupiga kelele darasani, mambo ya table (hesabu za kuzidisha za kushtukizwa na teacher)....kumi na mbili mara sitaaaaaa mwl anakulamba fimbo mpaka utoe jibu.
Gwaride kwa filimbi:
Baba paka aliyesema.....
sisi hapa, ni watoto wadogo, twajifunza siasi ya ujamaaa, mwalimu wetu katfundisha adabu na heshima mbele ya wazaia wetu!.......
Oh, vijana, vijaaaana, vijana,vijana tayari, ..kulitumikia, taifa, taifa Tanzania, oh Walimu.......
Nyerere yupo ukiona kundi la siasa, Nyerere yupo,...Kawawa yupo......nk
Sisi tunataka kuwasha mwenge, tunataka kuwasha mwenge,
Naapana naahidi mbele ya chama,
Naipenda sana shule yetu
shule yetu imejengwa kilimani
Azimio la Iringa, lasema siasa ni kilimo, wananchi tushike majembe tukalime, tupate mazao bora.
Tumeuona mpilipili na maua yake ......
Ahaa, chama cahetu cha mapinduzi cha jenga nchi, Nyerere ahaaaa, Karume cha jenga nchi...
Nyimbo za mchakamcha, darasani na kuhamasishana
Iddi Amiri akifa, mimi siwezi kulia,ntamtupa kagera awe chakula cha mamba.
Mwenge huo mwenge.....mbio mbio
twende tukawinde leeeeo, tukawindeee vipepeo
Hasiependa shule ni mjinga kabisa
Kikojozi na nguo twaichoma moto!
Baba yake Juma ametia vilaka matakoni mwake vinauluzana umekuja lini....
Kwaya:
Karibu sana shuleni kwetu mtukufu Mkuu wetu wa Mkoa,
Ngonjera:
Hodi hodi uwanjani,
Vitabu:
Juma na Roza
Kalumekenge
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
siku ya gulio Katelelo
Kibanga ampiga Mkoloni
Brown ashika tama
Safari yenye mkosi
Nondo mla watu
Maarifa
Barua za mapenzi zinachorwa Mkuki na moyo, unaanza na "Kwako Dada Mpendwa..."
Barua za mapenzi zinafichwa kwenye mikebe
Barua za mapenzi zikipatikana zinasomwa mstarini.
kumbebea mwalimu maembe
kumpelekea mwalimu misigo yake kwa demu
Kuchunguliwa wanafunzi wa kike wakiwa ****** au kwa vioo
Kazi za nje
Kumwagilia Busatan za shule
Kufyatua tofari
Kuja na nyasi shuleni
kuleta maji kumwagia viunga vya shule kuondoa vumbi
kulima mashamba ya Mwalimu, DRDD, Mkuu wa Wilaya nk.
Kutoka shule
sasa, sasa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri tutaonana keshoooooo!