Wakristo wa Iran washerehekea Pasaka mafichoni

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
16,726
Reaction score
20,030
Juu ya meza sebuleni, Tina - si jina lake halisi - amefanya onyesho na miali ya chai, mayai ya rangi ya pastel, mishumaa na msalaba mdogo wa mbao. Ni njia yake mwenyewe, ya karibu ya kuashiria Pasaka.

Yeye na mume wake walibadili dini na kuwa Wakristo miaka mingi iliyopita, jambo ambalo katika nchi yao ya Iran, limekatazwa na sheria. Wanaweza kukamatwa wakati wowote.

Katiba ya Iran inatambua dini ndogo ndogo. Wakristo wa Armenia na Ashuru wanaweza kufuata dini zao, lakini wamepigwa marufuku kuwahubiria Wairani wengine au hata kuwaruhusu kuingia makanisani mwao.

Huo ndio uhuru wa kuabudu kwa jamaa zetu wa uarabuni. Eti kubadili dini ni kosa linaloweza Fanya uuawe! Aisee!
Uhuru lazima uwe na mipaka wewe usingependa mwanao abadili maadili na aanze kufundishwa ushoga, kisa ni uhuru wake.
 
Wewe mtoto wako ( anaishi maisha yake na hakutegemei kwa lolote) akibadili dini utamfanya nini!?
 
Kama wao wanaona ukrisito ni hatari kwa usalama na maadili ya taifa lao wana haki ya kuudhibiti.
Alafu hata hivyo wakristo ndani ya Iran wametengewa mpaka viti maalumu ndani ya bunge la nchi hiyo sasa sijui hizi habari za Iran kukandamiza wakristo zinatoka wapi?
 
Wewe mtoto wako ( anaishi maisha yake na hakutegemei kwa lolote) akibadili dini utamfanya nini!?
Umesha sema akiwa anajitegemea lakini kama yuko chini yangu ni lazima afuate maadili yangu.
 
Na muelekeza mazuri na kumzuia mabaye, na sotakubali kumpa uhuru wakujifunza mabaya, lazoma uhuru uwe na mipaka.......
 
Ukiona Imani Fulani inalinda dini yake kiasi hiki ujue kuna shida na hawajiamini maana wanajua wakiruhusu Uhuru wa kuabudu na kujenga makanisa ujue baada ya miaka 5 hiyo dini na watu wake wote watahama.

Ule utamaduni wa Uhuru wa kuabudu kama wa nchi za ulaya ukiruhisiwa nchi za kiarabu baada ya miaka kadhaa hakutakuwa tena wavaa kobazi...hawa jamaa wanajua udhaifu uliopo kwenye Imani Yao ndiyo maana wanalinda Kwa gharama kubwa acheni waendelee kumpigania MUNGU wao
 
Ndio maana ya swali langu na ndio maana nimeweka hayo maelezo kwenye mabano hapo. Mtoto akiwa chini Yako ndio unaweza kumuwekea hizi kanuni zako na sio mtu mzima anayejitegemea. Na ndio maana nimekuuliza mwanaye akibadili dini yeye atamfanyaje!?
 
Na muelekeza mazuri na kumzuia mabaye, na sotakubali kumpa uhuru wakujifunza mabaya, lazoma uhuru uwe na mipaka.......
Nimekuuliza akibadili dini, hayo mengine sijauliza
 
Juu ya meza sebuleni, Tina - si jina lake halisi - amefanya onyesho na miali ya chai, mayai ya rangi ya pastel, mishumaa na msalaba mdogo wa mbao. Ni njia yake mwenyewe, ya karibu ya kuashiria Pasaka.

Yeye na mume wake walibadili dini na kuwa Wakristo miaka mingi iliyopita, jambo ambalo katika nchi yao ya Iran, limekatazwa na sheria. Wanaweza kukamatwa wakati wowote.

Katiba ya Iran inatambua dini ndogo ndogo. Wakristo wa Armenia na Ashuru wanaweza kufuata dini zao, lakini wamepigwa marufuku kuwahubiria Wairani wengine au hata kuwaruhusu kuingia makanisani mwao.

Muislam akiingia ktk ukiristo ashapoteza kila kitu ktk familia.
 
Ukiona Imani Fulani inalinda dini yake kiasi hiki ujue kuna shida na hawajiamini maana wanajua wakiruhusu Uhuru wa kuabudu na kujenga makanisa ujue baada ya miaka 5 hiyo dini na watu wake wote watahama.

Ule utamaduni wa Uhuru wa kuabudu kama wa nchi za ulaya ukiruhisiwa nchi za kiarabu baada ya miaka kadhaa hakutakuwa tena wavaa kobazi...hawa jamaa wanajua udhaifu uliopo kwenye Imani Yao ndiyo maana wanalinda Kwa gharama kubwa acheni waendelee kumpigania MUNGU wao
Hapa bongo ambapo kila mtaa una kanisa zinazo shinda zinatupigia kelele mbona hao wavaa kobanzi hawajaisha badala yake wanaongezeka kila siku?

Alafu aliye kwambia kuwa Iran hakuna makanisa ni nani?
 
Back
Top Bottom