Wakristo tuisusie Azam TV, wanatutenga Krismasi

Baraka DSM

Member
Sep 12, 2017
52
125
Wakristo tuwashangae Azam TV wameshindwa kuenzi Xmas yetu kwa kuweka alama au kiashiria cha kuonesha Kristo anazaliwa.

Sisi kama wateja ambao wakati wa sikukuu za Kiislam tunavumilia kuona alama zao zinazoashiria sikukuu zao ni vyema tukawasusia TV yao inayoonesha ubaguzi wa dini hadharani.

King'amuzi chao nishachoma moto.
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,832
2,000
Wakristo tuwashangae Azam TV wameshindwa kuenzi Xmas yetu kwa kuweka alama au kiashiria Cha kuonesha kristo anazaliwa.

Sisi kama wateja ambao wakati wa skukuu za kiislam tunavumilia kuona alama zao zinazoashiria sikukuu zao Ni vyema tukawasusia TV yao inayoonesha ubaguzi wa dini hadharani.

King'amuzi chao nishachoma moto
Acha udini boss,Kama wameamua hivyo,sie halituhusu,unaposema tuisusie,vipi kuhusu waajiriwa ambao ni wakristo,waache kazi?
Sio busara,tusipende kila kitu kukihusisha na dini.

Ukipanda boti yeyote inayoenda Zenj,vipindi vyote vinavyooneshwa kwenye Tv ndani ya boti,vina maudhui ya islam,lakini haimaniishi kwamba wanawasharau wakristo,inawezekana sababu ni kwamba asilimia kubwa ya wasafiri ni Islam,
Ukipanda Basi lolote linalotoka Mwanza kwenda Moshi,au Dar kwenda Arusha,nyimbo nyingi zinazopigwa ni za kikristo,lakini haimaniishi abiria wote ni wakristo,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom