Wakosoaji wa Rais Magufuli

Wakosoaji wa Rais Magufuli

Hakuna anayepinga kukosolewa kwa Magu bali wengine ukosoaji wao ni upuuzi mtupu. Hebu fikiria mtu anapinga kitendo cha Rais kuwatumbua wafanyakazi wazembe na wezi. Hebu fikiria mtu anakosoa kitendo cha Rais kutosafiri nje ya nchi wakati anashughulikia matatizo ya ndani. Huu si ukosoaji bali ni utaahira

Oh mbona wapo wengi tu wanaokasirika tukimkosoa Magu....

We hujawaona?
 
Wewe umewahi kumkosoa kwa lipi? Au kila analolifanya wewe unaona sawa tu?
 
Oh mbona wapo wengi tu wanaokasirika tukimkosoa Magu....

We hujawaona?
Mkuu, ni kazima wakasirike kwa vile kile mnachokosoa ni kama hakipo. Ndo maana hata mimi nakasirika sana watu wanaposhupalia kumpinga Magufuli kwa kila anachofanya hata kama ni kwa maslahi mapana ya Mama Tanzania
 
Wakosoaji ndio wanaokujenga. Ni kama kwenye mpira kama ligi ina ushindani ndio hufanya timu kusajili wachezaji wakali...

Mfano mdogo tu, zamani JPM alikuwa anatusomea mapato na matumizi kila mwezi lakini naona miezi miwili kimya, je yameshuka? Na tabia za wapenda sifa huwa hawapendi kukosolewa
 
Pale mnapo beza kila juhud za Jpm, hata ambapo mnaelewa mamvi asinge weza fikia kwa ubora.
Uelewa wako ni mdogo sana. Hakuna anayependa taifa letu liangamie. Kuna mambo magu kama binadamu anakosea kama alivyokosea mamvi kibinadamu. Tatizo lenu nyie mnataka hata sisi wananchi tumpigie makofi kwa kila kitu, kama wabunge wa chama tawala. Kuna watu wanaona mbali mara mia yako. Wanajua maamuzi ya haraka yana hasara gani. Ndio maana wanatoa ushauri kabla ya matatizo kujitokeza. Mfano mdogo tu ni suala la sukari. Mpaka kamati ya bunge iliwashauri. Badala yake mkawatumia takukuru kuhojiwa. Huko sio kupinga, huko ni kishauri. Mnaposhauriwa msiwe wajuaji. Baada ya hapo mnaanza kusema anahujumiwa. Hivi ni nani mwenye nguvu kati ya serikali na mfanyabiashara?
 
Jana kuna jamaa nimewashangaa sana waliokuwa wanakosoa kitendo cha Serikali kutoa maelekezo kwa TANESCO kutoingia mikataba ya kuzalisha umeme na makampuni binafsi badala yake wajikite kwenye kujenga miundombinu ya kujitegemea. Watu wanawatetea uamuzi wa Symbion kutaka kuishtaki TANESCO utafikiri ni kampuni yao
 
Mkuu, ni kazima wakasirike kwa vile kile mnachokosoa ni kama hakipo. Ndo maana hata mimi nakasirika sana watu wanaposhupalia kumpinga Magufuli kwa kila anachofanya hata kama ni kwa maslahi mapana ya Mama Tanzania

Wewe kama ushalewa pombe ya Magufuli hata akifanya kosa huwezi kuliona.
 
Uelewa wako ni mdogo sana. Hakuna anayependa taifa letu liangamie. Kuna mambo magu kama binadamu anakosea kama alivyokosea mamvi kibinadamu. Tatizo lenu nyie mnataka hata sisi wananchi tumpigie makofi kwa kila kitu, kama wabunge wa chama tawala. Kuna watu wanaona mbali mara mia yako. Wanajua maamuzi ya haraka yana hasara gani. Ndio maana wanatoa ushauri kabla ya matatizo kujitokeza. Mfano mdogo tu ni suala la sukari. Mpaka kamati ya bunge iliwashauri. Badala yake mkawatumia takukuru kuhojiwa. Huko sio kupinga, huko ni kishauri. Mnaposhauriwa msiwe wajuaji. Baada ya hapo mnaanza kusema anahujumiwa. Hivi ni nani mwenye nguvu kati ya serikali na mfanyabiashara?

Tufanye wote Mimi na were hatuna uwezo wa kuona huko mbaaaaali.

Saasa tuwatumie hao waona mbaali.

Hivi unakumbuka hao hao waona mbaali ndio walio toa tetesi za wafanya biashara kutaka kuitumia kamati ya bunge hyhy kuwanufaisha wafanya biashara wabaya ambao mie huwaita uchwara?

Tufanye tuko katika mapito ya kiandaa namna bora ya kujitegemea, juhudi zetu zitatuvusha na so akili tegemezi, masikio marefu na midomo mipana.
 
Tatizo lililopo watu wanafikili magu malaika alieshushwa na mungu kuja kuitia tz utajili kumbe wanajisahaulisha kuwa huyu ndie alieuza nyumba za serilali ndie alieitia hasara serikali kupitia Samaki aliokamata kimakosa sasa leo mtakakusema yeye ni asikosolewe kweli watz wanafiki
 
Tatizo kubwa la hili jukwaa hoja haijadiliwi kwa uzito wake bali kwa maslahi na upande wa anayeijadili...yawezekana uwezo wetu wa kufikiri umeshuka sana au mapenzi kwa vyama vyetu yanatuvuta mkono..kama ni hivyo hakuna haja ya kujiita great thinkers.
 
Wewe mbona hujatoa hoja yeyote zaidi ya kublame tu
 
Wakosoaji wa JPM wamegawanyika katika makundi yafuatayo:

5. Wale ambao ni makuhadi wa soko huria na wapiga zumari wa pepo za mabwege, hawa ndio wanakuja na dhana ya kibaraguzi ya kuwa JPM ni dikteta hafuati utawala bora.

Mwalimu Nyerere alisema katika kuleta maendeleo wapo watakao pinga maendeleo hayo, lakini sisi tutasonga mbele.

Songa mbele JPM, watanzania walio wengi wako pamoja na wewe, hata ambao hawakukupigia kura wengi sasa wako na wewe.

HAYA NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Ni mimi Mwanamtaa
Mkuu Mwanamtaa Mabuba FKM, kwanza hongera kutimiza miaka 10 humu jf, ukikutana na mtu yoyote aliyejiunga jf 2006, kitu cha kwanza ni heshima adabu, na kwa sisi wapenda historia unamfuatilia tangu alipojiunga hiyo miaka yake 10 humu jf, amechangia nini!.

Hongera za pili ni hongera kwa kwa bandiko hili, maana tangu umejiunga humu jf, umeanzisha mabandiko 9, na kati ya hayo mabandiko yako 9, hili ndio bandiko lako la kwanza kufika page 2!, hongera!.

Nilipokusoma bandiko lako la kwanza humu jf, kuhusu Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilivutiwa na maneno haya "
"tumekuwa na wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo, Naumia sana", kwa kuzingatia umejieleza wewe ni mwalimu, nikapata matumaini makubwa kuwa wewe unaweza kufikiri, unasoma vitabu, unajenga hoja bila kukurupuka, unajitambua, na sio mtizamishwaji wa mitazamo, bali unatazama mwenyewe!.

Kati ya hayo mabandiko yako 9, nilichangia bandiko moja tuu la Kibanda mpiganaji au mpigaji? na huu mchango wangu humu ni bandiko la pili.

Kiukweli I'm very disappointed na bandiko hili, lingetoka kwa mwana jf mwingine yoyote, nisingejali, lakini bandiko hili limetoka kwa mwana jf msomi wa Chuo Kikuu, tena sio msomi tuu bali ni mwalimu, mtu mwenye mawazo kama haya na ujengaji hoja wa aina hii ndio anayetufundishia watoto wetu, tutegemee nini?!.

Kiukweli ujengaji hoja wako ni hafifu, sasa kama kwa uhafifu huu ndio unatufundishia watoto wetu, tutegemee nini kama sio kuzalisha wanafunzi hafifu hafifu katika ujengaji hoja?!. Samahani kukushambulia personal kwa sababu wewe ni mkongwe, mwanzilishi wa jf, umekaa humu miaka 10, umepandisha mabandiko 9 kati ya yote hili ndio limenikera hivyo kabla sijajibu hoja, nimeanza kwanza kumchambua mleta hoja, ndipo nijitathmini nikimjibu ni mtu mwenye level ya uelewa dhana ya ukosoaji, usije ukawa unalijibu lijitu lijinga ambalo halina level ya uelewa wa kiwango cha majibu yako ukajikuta unampigia mbuzi gitaa!.

Mimi ni mmoja wa wakosoaji wa JPM na miongoni wanaosema JPM ni dikteta hafuati utawala bora!.

Wewe kama mwalimu ulipaswa kujiuliza jee huu ukosoaji una ukweli ndani yake, jee ni kweli Magufuli ni dikiteta?, jee ni kweli hafuati kanuni za utawala bora?!. Baada ya hapo ndipo ungekubali kuwa hata kama ni kweli Magufuli ni dikiteta, Tanzania hapa tulipofika, tulihitaji mtu wa kaliba ya Magufuli ili atuondoe hapa tulipo kwa mkono wa chuma na kulirudisha taifa kwenye mstari, hivyo unampa Magufuli yes kwa udikiteta wake ndio unaotakiwa Tanzania kwa sasa!.

Tukija kwenye utawala bora, pia unatoa uchambuzi kuwa yes Magufuli hafuati kanuni za utawala bora, kwa sababu hizo kanuni za utawala bora ndio zimelifikisha taifa letu hapa!.

Kati ya sisi wakosoaji wa Magufuli, tuko wakosoaji wa aina nyingi kama ulizozitaja ila tupo pia sisi wakosoaji ambapo ni wakosoaji washauri, na akifanya mazuri, tunamsifia, naomba nijitolee mfano mimi mwenyewe

Kwenye Mazuri ya Magufuli nimemsifu
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe ...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura;
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ..
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe .
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo .
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura;
Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!.Hii ni Bidhaa Muhimu au ...

Huu ni ukosoaji, ila kila kwenye ukosoaji huu, pia nimeweka ushauri wa the right thing to do!.

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Utumbuaji kwa Udhalilishaji!, Anachofanya Magufuli Sio Double
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti .
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais .
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu
Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance .
Wito: Magesa Mulongo afukuzwe Kazi kwa Bullying. Dr. Faisal was ...
Amri ya Rais Kuifuta Siku ya Uhuru Haijataja Usafi!. Jee Usafi ni .
Mkuu Mwalimu
Mabuba FKM
kwa vile wewe ni mwalimu, take time kosoma hoja, piga hoja kwa hoja.

Jumapili njema.

Pasco
 
Wakosoaji wa JPM wamegawanyika katika makundi yafuatayo:

1. Wale ambao ufisadi ulikuwa sehemu ya maisha yao, sasa wanaona mirija inakatwa, na wanakaribia kutumbuliwa au wametumbuliwa.

2. Wale ambao walifanya kazi kwa mazoea, bila posho kazi haziendi.

3. Wale ambao walitamani sana JPM asifanye haya anayoyafanya ili wao wapate namna ya kuongea. Kundi hili liliishi kwa kusema matatizo ya serikali, sasa yanatatuliwa limeanza kupinga utatuzi wake.

4. Wale ambao, ni bendera fuata upepo, hawa hawajui wanachopinga, bali huwafata watu wanaopinga.

5. Wale ambao ni makuhadi wa soko huria na wapiga zumari wa pepo za mabwege, hawa ndio wanakuja na dhana ya kibaraguzi ya kuwa JPM ni dikteta hafuati utawala bora.

Mwalimu Nyerere alisema katika kuleta maendeleo wapo watakao pinga maendeleo hayo, lakini sisi tutasonga mbele.

Songa mbele JPM, watanzania walio wengi wako pamoja na wewe, hata ambao hawakukupigia kura wengi sasa wako na wewe.

HAYA NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Ni mimi Mwanamtaa

Halafu nyie wenye mawazo kama haya ndiyo mnajua kweli mnakolipeleka taifa hili?

Na nyie ndiyo washauri pengine wa Rais wenu huyu!!

Yaani always thinking; kuna watu wanapenda posho, tubane!

Kuna watu walikuwa wanalikuwa wananufaika na hili au lile...tubane!!

Then, what is next?

Je, ni ili in return wawekwe wengine kunufaika na kutafuna kwa mtindo mwingine....au??

Sijaipata logic iliyoko ktk hili andiko lako kabisaaa zaidi ya kwamba labda na wewe unafutia mwanya flani hivi wa kupenya huko huko!!

Hebu tuletee wewe mawazo yako mbadala hata kama ni ya kusifu....leta hizo sifa za Magufuli ili wakosoaji wakose cha kukosoa!!
 
Wakosoaji wa JPM wamegawanyika katika makundi yafuatayo:

1. Wale ambao ufisadi ulikuwa sehemu ya maisha yao, sasa wanaona mirija inakatwa, na wanakaribia kutumbuliwa au wametumbuliwa.

2. Wale ambao walifanya kazi kwa mazoea, bila posho kazi haziendi.

3. Wale ambao walitamani sana JPM asifanye haya anayoyafanya ili wao wapate namna ya kuongea. Kundi hili liliishi kwa kusema matatizo ya serikali, sasa yanatatuliwa limeanza kupinga utatuzi wake.

4. Wale ambao, ni bendera fuata upepo, hawa hawajui wanachopinga, bali huwafata watu wanaopinga.

5. Wale ambao ni makuhadi wa soko huria na wapiga zumari wa pepo za mabwege, hawa ndio wanakuja na dhana ya kibaraguzi ya kuwa JPM ni dikteta hafuati utawala bora.

Mwalimu Nyerere alisema katika kuleta maendeleo wapo watakao pinga maendeleo hayo, lakini sisi tutasonga mbele.

Songa mbele JPM, watanzania walio wengi wako pamoja na wewe, hata ambao hawakukupigia kura wengi sasa wako na wewe.

HAYA NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Ni mimi Mwanamtaa

well said!!

amewakalia kooni
 
Maisha yamekuwa magumu kwa mwananch wa kawaida,lzm JPM angundue wanaoteseka si wale aliowalenga.
 
Back
Top Bottom