Wakosoaji wa Rais Magufuli

Wakosoaji wa Rais Magufuli

Wakosoaji wa JPM wamegawanyika katika makundi yafuatayo:

1. Wale ambao ufisadi ulikuwa sehemu ya maisha yao, sasa wanaona mirija inakatwa, na wanakaribia kutumbuliwa au wametumbuliwa.

2. Wale ambao walifanya kazi kwa mazoea, bila posho kazi haziendi.

3. Wale ambao walitamani sana JPM asifanye haya anayoyafanya ili wao wapate namna ya kuongea. Kundi hili liliishi kwa kusema matatizo ya serikali, sasa yanatatuliwa limeanza kupinga utatuzi wake.

4. Wale ambao, ni bendera fuata upepo, hawa hawajui wanachopinga, bali huwafata watu wanaopinga.

5. Wale ambao ni makuhadi wa soko huria na wapiga zumari wa pepo za mabwege, hawa ndio wanakuja na dhana ya kibaraguzi ya kuwa JPM ni dikteta hafuati utawala bora.

Mwalimu Nyerere alisema katika kuleta maendeleo wapo watakao pinga maendeleo hayo, lakini sisi tutasonga mbele.

Songa mbele JPM, watanzania walio wengi wako pamoja na wewe, hata ambao hawakukupigia kura wengi sasa wako na wewe.

HAYA NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Ni mimi Mwanamtaa
Safi sana!
 
Kwan Magu ni Mungu? anapokosea lazima akosolewe na akifanya vizuri atapongezwa..
 
Mungu tu ndiyo hakosolewi lakini Magufuli ni binadamu mwenzetu tuna kila sababu ya kumkosoa kama haturudhishwi na utendaji wake na hayo makundi uliyoyaweka hapo juu hayahusu kitu.
 
kuna watu wakokwa ajili ya kupinga tu hasa wale ambao walifikiri mtu wao ndiye atakuwa rais na wao wataendelea kula bata kwa jasho la watanzania wengi, baada ya mambo kugeuka wamebaki wakipinga hata yale yanayofanywa kwa manufaa ya nchi.Rais ni binadamu pale anapokosea anahitaji kukosolewa ili arudi kwenye njia sahihi ila sio kumkosoa kwa sababu amefuta safari au ndugu na jamaa yako ametumbuliwa majipu
 
Unamahaba kupitiliza sidhani kama unamsaidia. Pole
 
Majizi yalikuwa yanaiba ila sote tulikuwa tunashiba. Saivi majizi hayapo ila njaa inatutawala
 
Pasco

tuongeze wanaokosoa kwa maslahi ya Taifa, ambao ni wachache sana.
 
Mkuu Mwanamtaa Mabuba FKM, kwanza hongera kutimiza miaka 10 humu jf, ukikutana na mtu yoyote aliyejiunga jf 2006, kitu cha kwanza ni heshima adabu, na kwa sisi wapenda historia unamfuatilia tangu alipojiunga hiyo miaka yake 10 humu jf, amechangia nini!.

Hongera za pili ni hongera kwa kwa bandiko hili, maana tangu umejiunga humu jf, umeanzisha mabandiko 9, na kati ya hayo mabandiko yako 9, hili ndio bandiko lako la kwanza kufika page 2!, hongera!.

Nilipokusoma bandiko lako la kwanza humu jf, kuhusu Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilivutiwa na maneno haya "
"tumekuwa na wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo, Naumia sana", kwa kuzingatia umejieleza wewe ni mwalimu, nikapata matumaini makubwa kuwa wewe unaweza kufikiri, unasoma vitabu, unajenga hoja bila kukurupuka, unajitambua, na sio mtizamishwaji wa mitazamo, bali unatazama mwenyewe!.

Kati ya hayo mabandiko yako 9, nilichangia bandiko moja tuu la Kibanda mpiganaji au mpigaji? na huu mchango wangu humu ni bandiko la pili.

Kiukweli I'm very disappointed na bandiko hili, lingetoka kwa mwana jf mwingine yoyote, nisingejali, lakini bandiko hili limetoka kwa mwana jf msomi wa Chuo Kikuu, tena sio msomi tuu bali ni mwalimu, mtu mwenye mawazo kama haya na ujengaji hoja wa aina hii ndio anayetufundishia watoto wetu, tutegemee nini?!.

Kiukweli ujengaji hoja wako ni hafifu, sasa kama kwa uhafifu huu ndio unatufundishia watoto wetu, tutegemee nini kama sio kuzalisha wanafunzi hafifu hafifu katika ujengaji hoja?!. Samahani kukushambulia personal kwa sababu wewe ni mkongwe, mwanzilishi wa jf, umekaa humu miaka 10, umepandisha mabandiko 9 kati ya yote hili ndio limenikera hivyo kabla sijajibu hoja, nimeanza kwanza kumchambua mleta hoja, ndipo nijitathmini nikimjibu ni mtu mwenye level ya uelewa dhana ya ukosoaji, usije ukawa unalijibu lijitu lijinga ambalo halina level ya uelewa wa kiwango cha majibu yako ukajikuta unampigia mbuzi gitaa!.

Mimi ni mmoja wa wakosoaji wa JPM na miongoni wanaosema JPM ni dikteta hafuati utawala bora!.

Wewe kama mwalimu ulipaswa kujiuliza jee huu ukosoaji una ukweli ndani yake, jee ni kweli Magufuli ni dikiteta?, jee ni kweli hafuati kanuni za utawala bora?!. Baada ya hapo ndipo ungekubali kuwa hata kama ni kweli Magufuli ni dikiteta, Tanzania hapa tulipofika, tulihitaji mtu wa kaliba ya Magufuli ili atuondoe hapa tulipo kwa mkono wa chuma na kulirudisha taifa kwenye mstari, hivyo unampa Magufuli yes kwa udikiteta wake ndio unaotakiwa Tanzania kwa sasa!.

Tukija kwenye utawala bora, pia unatoa uchambuzi kuwa yes Magufuli hafuati kanuni za utawala bora, kwa sababu hizo kanuni za utawala bora ndio zimelifikisha taifa letu hapa!.

Kati ya sisi wakosoaji wa Magufuli, tuko wakosoaji wa aina nyingi kama ulizozitaja ila tupo pia sisi wakosoaji ambapo ni wakosoaji washauri, na akifanya mazuri, tunamsifia, naomba nijitolee mfano mimi mwenyewe

Kwenye Mazuri ya Magufuli nimemsifu
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe ...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura;
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ..
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe .
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo .
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura;
Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!.Hii ni Bidhaa Muhimu au ...

Huu ni ukosoaji, ila kila kwenye ukosoaji huu, pia nimeweka ushauri wa the right thing to do!.

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Utumbuaji kwa Udhalilishaji!, Anachofanya Magufuli Sio Double
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti .
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais .
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu
Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance .
Wito: Magesa Mulongo afukuzwe Kazi kwa Bullying. Dr. Faisal was ...
Amri ya Rais Kuifuta Siku ya Uhuru Haijataja Usafi!. Jee Usafi ni .
Mkuu Mwalimu
Mabuba FKM
kwa vile wewe ni mwalimu, take time kosoma hoja, piga hoja kwa hoja.


Jumapili njema.

Pasco
Mkuu Pasco

Nimekuelewa sana, labda nijibu masuala uliyoyaibua kama ifuatavyo:

1. kwanza unapaswa ujue aina ya wanachama wa JF ndio ujue kwani jina la Mabuba tokea mwaka 2006 JF inaanza limeweka hapa mara 9. Jina Mabuba ni jina langu halisi tena sio la kutunga. Ni jina ambalo haliwezi kusemwa kwa kutobandika mabandiko mengi kwa jina hili. Lakini yawezekana kila siku ukawa unasoma mabandiko yangu pasipo kujua. Wewe huwezi jiuliza member toke 2006 ana mabandiko 9/

2. Hayo ni mawazo yangu yaweza kupingwa kwa hoja, lakini nasikitika badala ya kujadili hoja unajadili lini nimejiunga na JF hapa. Ungeliniambia hoja zangu hazina mashiko sawa, lakini hoja zangu zimejikita kwenye weredi wa aina ya watu wamkosoao JPM. Aina zote za watu niliowataja wapo, ndio maana hujakanusha.

3. Pamoja na uchapwa wa hoja yako nashukuru umeniongezea kundi jingine la wakosoaji ambao, ni wale ambao wanakosoa kwa maslahi ya umma, ambao mimi nina amini ni wachache sana.

Asante
 
Back
Top Bottom