Wakosoaji wa Rais Magufuli

Wakosoaji wa Rais Magufuli

mabuba

Senior Member
Joined
Dec 5, 2006
Posts
133
Reaction score
90
Wakosoaji wa JPM wamegawanyika katika makundi yafuatayo:

1. Wale ambao ufisadi ulikuwa sehemu ya maisha yao, sasa wanaona mirija inakatwa, na wanakaribia kutumbuliwa au wametumbuliwa.

2. Wale ambao walifanya kazi kwa mazoea, bila posho kazi haziendi.

3. Wale ambao walitamani sana JPM asifanye haya anayoyafanya ili wao wapate namna ya kuongea. Kundi hili liliishi kwa kusema matatizo ya serikali, sasa yanatatuliwa limeanza kupinga utatuzi wake.

4. Wale ambao, ni bendera fuata upepo, hawa hawajui wanachopinga, bali huwafata watu wanaopinga.

5. Wale ambao ni makuhadi wa soko huria na wapiga zumari wa pepo za mabwege, hawa ndio wanakuja na dhana ya kibaraguzi ya kuwa JPM ni dikteta hafuati utawala bora.

Mwalimu Nyerere alisema katika kuleta maendeleo wapo watakao pinga maendeleo hayo, lakini sisi tutasonga mbele.

Songa mbele JPM, watanzania walio wengi wako pamoja na wewe, hata ambao hawakukupigia kura wengi sasa wako na wewe.

HAYA NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Ni mimi Mwanamtaa
 
Tumkumbushe na Escrow, Richmond, Lugumi, Nyumba za umma, Meli Chakavu, Mabehewa fake, Rada, EPA, NBC, Kuchakachua Katiba ya wananchi, kuchakachua uchaguzi, Kupuuza sheria kanuni na taratibu za nchi na Utumishi wa umma, kuhamisha fedha za umma bila idhini ya Bunge, meremeta, kiwira, kagoda...
 
Unatafuta ukuu wa wilaya? Haya endelea umakaribia kuupata.
 
Tumkumbushe na Escrow, Richmond, Lugumi, Nyumba za umma, Meli Chakavu, Mabehewa fake, Rada, EPA, NBC, Kuchakachua Katiba ya wananchi, kuchakachua uchaguzi, Kupuuza sheria kanuni na taratibu za nchi na Utumishi wa umma, kuhamisha fedha za umma bila idhini ya Bunge, meremeta, kiwira, kagoda...
mwishowe hii list itakuwa national anthem of tz, we've to luk 4ward at the future not the past
 
Uje ukute mtoa mada hajawahi hata kulipa kodi au kama keshalipa hajui kwa nini analipa kodi.
Mtu kukosolewa haimaanishi kwamba anadharaulika, hizo ni changamoto anapewa sababu yeye sio malaika kusema kwamba hakosei. Posho sio kitu katika kusukuma gurudumu la maendeleo ila inaongeza morali ya utendaji wa kazi, halafu sio watumishi wote walikuwa wanapokea posho hilo lazima utambue mtoa mada.
 
toka aseme vijana ndo mnatakiwa basi sasa nikukanyagana sana kuleta post ili tu uonekane nawe upate kacheo
 
Aliyeandika anahitaji elimu atoke kwenye gurudumu la wajinga.
Kwani Magu ndio nani kwamba hakosei? Ashabugi kwenye sukari mmeona bei zilivopanda ovyo mnataka evidence ipi kua na yeye ni kama binadamu wengine?

Kukosoa lazima tukosoe anapokosea, na kusifia tutasifia anapopatia, tumesifia mengi tu. Ila yamempa kichwa sasa inabidi tuonyeshe anapokosea ili arudi akae ajipange upya.

We kundi lako ni la wale ambao wanamuona kama mungu kwamba neno lake ndio mwisho na halina makosa. Wewe ungekua north korea ungekua wa kwanza kupiga magoti kwa Kim Jong Eun. Hujawahi lipa kodi wewe kwa hiyo huwezi jua inavouma kuona hela unalipa nyingi na watu wanafanyia ujinga hiyo hela.
 
Uje ukute mtoa mada hajawahi hata kulipa kodi au kama keshalipa hajui kwa nini analipa kodi.
Mtu kukosolewa haimaanishi kwamba anadharaulika, hizo ni changamoto anapewa sababu yeye sio malaika kusema kwamba hakosei. Posho sio kitu katika kusukuma gurudumu la maendeleo ila inaongeza morali ya utendaji wa kazi, halafu sio watumishi wote walikuwa wanapokea posho hilo lazima utambue mtoa mada.
Nilichogundua ni kuwa wewe ni mfanyakazi wa serikali
 
Tumkumbushe na Escrow, Richmond, Lugumi, Nyumba za umma, Meli Chakavu, Mabehewa fake, Rada, EPA, NBC, Kuchakachua Katiba ya wananchi, kuchakachua uchaguzi, Kupuuza sheria kanuni na taratibu za nchi na Utumishi wa umma, kuhamisha fedha za umma bila idhini ya Bunge, meremeta, kiwira, kagoda...

Sitasema Mengi, ila tu la kuhamisha pesa sa serikali.

Swali huhamishwa ili zikafisadiwe, au huhamisha ili Mimi na wewe tupate huduma kwa urahisi na kupunguza urasimu wa wabunge wanao ishi kwa kupinga hata jema?

Kmbk, si kila atakaye ita Baba baba atauona ufalme wa mbingu.

Wakati flani niliwasikia ( katika kampen) mkidai kurahsiha upatikanaji wa huduma. Acha magu afanye mda ukifka mtaelewa tu.
 
Tumkumbushe na Escrow, Richmond, Lugumi, Nyumba za umma, Meli Chakavu, Mabehewa fake, Rada, EPA, NBC, Kuchakachua Katiba ya wananchi, kuchakachua uchaguzi, Kupuuza sheria kanuni na taratibu za nchi na Utumishi wa umma, kuhamisha fedha za umma bila idhini ya Bunge, meremeta, kiwira, kagoda...
Tulikwisha sema hatutafunua makaburi!
 
Watu hampendi Magufuli akikosolewa eh?
Kukosolewa ni sehemu ya maisha. Ila kuna wengine hawakosoi kwa lengo la kutaka kurekebisha bali wanakosoa ili mfumo mbovu uliokuwepo hapo awali uendelee
 
Haha wanaccm siku hizi wanasema hatuhitaji mfumo , kwa sababu Magu ni mfumo!
 
Huyo Magafuli tuts kosa tu. Kwani ye nani hadi asikosolewe.
Hakuna anayepinga kukosolewa kwa Magu bali wengine ukosoaji wao ni upuuzi mtupu. Hebu fikiria mtu anapinga kitendo cha Rais kuwatumbua wafanyakazi wazembe na wezi. Hebu fikiria mtu anakosoa kitendo cha Rais kutosafiri nje ya nchi wakati anashughulikia matatizo ya ndani. Huu si ukosoaji bali ni utaahira
 
Back
Top Bottom