Wakopaji Twiga Bancorp rudisheni fedha, mnasakwa

Kukopa benki si dhambi na kama benki itafilisika kuna mambo mengi sana ya kuangalia. Jee waliokopa walikopa hela hizo kwa ajili ya kufanyia nini na je benki ilijiridhisha kwamba miradi iliyokopewa hela italeta faida itakayorudisha mkopo?

Mkuu Benki ya Twiga ilikuwa inakopesha kwa kujulikana na wengi walio firisi Benki hiyo ni Wakubwa au wenye connection na Establishment kumbuka visanga vya import support funds nani walipewa hizo funds wengi walikuwa ni Govt Officials jwa kuwatumia jamaa zao wenye makampuni kwenye briefcase, Augustino Mlema aliwahi kulivalia njuga saula hili akazimwa!

Tusije tukajidanganya kwamba kundi ambalo lina influence kubwa katika Taifa letu wanaweza kurudisha hata senti tano - walisha jiona ni demi Gods uwambii kitu ni Dk.Magufuli tu ambaye anaweza kuwabana na ku deal nao effectively.

Ujinga huu wa kukwapua fedha za UMMA bila kuturudisha haupo kwenye Mabenki tu hata Mashirika ya hifadhi ya jamii, kundi hilo ovu linakwenda kukopa huko huko wakati wala si wanachama wa mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii, wanachama awapewi mkopo - ma culprit awachukuliwi hatua yoyote!!

Haya tuje Benki kuu kwenyewe nayo kuna sehemu inapashwa kulahumiwa - miaka ya nyuma iliwahi kumsimamia former Minister/mbuge apewe mikopo ya mabillion kujenga kiwanda cha kusindika nyama ya ng'ombe au ranch sikumbuki vizuri, je, hao Benki kuu wanaweza kuwathibitishia wananchi kwamba hizo hela zimekwisha rudishwa na muhusika au kiwanda hicho kipo kweli? Watanzania wangapi wa kawaida wanaweza kupewa fulsa kama hizo na Benki kuu?
 
Haya tuje Benki kuu kwenyewe nayo kuna sehemu inapashwa kulahumiwa - miaka ya nyuma iliwahi kumsimamia former Minister/mbuge apewe mikopo ya mabillion kujenga kiwanda cha kusindika nyama ya ng'ombe au ranch sikumbuki vizuri, j
Ni mzindakaya ndio aliekopeshwa hayo mabilioni
 
Tuweke akiba ya maneno tusubirie majina ya wanasiasa wanaodaiwa, ila Magu mjanja sana, ukitaka ku deal vizuri na mwanasiasa kulipa deni muanike uchi tu, naamini baadhi ya ela itarudishwa tu na wahusika saivi watakuwa wanahangaika kupata ela ya kulipia mkopo.
 
"Niacheni kwanza ninyooshe nchi" pamoja na nchi ilikopinda ni kwenye suala hili la mikopo ya Twiga. Ili tuweze kuwa na siasa safi na wanasiasa safi ni bora wale waliotajwa kijumla jumla orodha ya majina yao yawekwe hadharani kama "defaulters". Pia ikiwezekana pasipo kuangalia sura zao wafilisiwe ikiwa sehemu moja wapo ya kunyoosha nchi!
 
Hivi nyie mna matatizo gani? Kufilisika kwa twiga bancorp kuna uhusiano gani na CCM? mnaelezwa sababu za kuu ni fedha kutorejeshwa na wateja wake waliokopa. Wengine mnakuja na comment za kuishambulia ccm bila sababu za msingi kabisa. Kwan kama huna hoja si ukae tu kimya?
 
sasa waliopewa dhamana ya kulitumikia taifa ndio wafilisi. Yani inasikitisha. Benki wanafilisi, madini wanafilisi hazina wanafilisi misaada kutoka nje wanafilisi viwanda wamefilisi nyumba za serikali wamefilisi. Hivi hawa ni binadamu wa aina gani???
 
Back
Top Bottom