Wakopaji Twiga Bancorp rudisheni fedha, mnasakwa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Dar es Salaam. Kama ulikopa Twiga Bancorp, bado hujasalimika inabidi tu uwasilishe fedha hizo, kwani Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema inaendelea na uchunguzi wa watu waliokopa ili iwabane.

Benki hiyo imefilisika na kuwekwa chini ya usimamisi wa BoT baada ya kubainika kuwa mtaji uko katika hali mbaya kiasi cha kuweka hatarini fedha za wateja.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu alisema wiki iliyopita kuwa benki hiyo ilikuwa na mtaji hasi wa Sh21 bilioni baada ya kuanza na mtaji wa Sh7.5 bilioni unaokubalika kisheria.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu orodha ya wakopaji wa benki hiyo, msimamizi wa benki wa BoT, Kennedy Nyoni amesema kwa sasa bado wanachunguza waliokopa na ripoti itatolewa wiki ijayo.

“Tulichofanya ni kuchukua usimamizi wa hiyo benki na kumweka mtu wetu pale. Sheria ya Benki inatoa siku 90 za uchunguzi, lakini hadi wiki ijayo tutakuwa tumepata taarifa. Hata leo (jana) tuko ofisini tunaendelea na uchunguzi,” amesema Nyoni.

Akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza kufilisika kwa benki hiyo, Gavana Ndulu alisema bado benki hiyo inazo mali zinazofikia Sh90 bilioni na Sh9 bilioni kati ya hizo haziko vizuri.

Alisema wametumia kifungu namba 56(1) (g)(I) na 56(2) (a-d) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, kuiweka Twiga chini ya usimamizi wa BoT.

Twiga Bancorp ilianzishwa mwaka 1992 ikiwa chini ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), na mwaka 1998 ikabadilishwa na kuruhusiwa kufanya kazi zote za kibenki isipokuwa za kibenki isipokuwa kupokea au kuchukua fedha za akaunti za kawaida.
 
mimi hizi kelele sizielewi kabisa. Hata mheshimiwa alipoongelea hilo akapindishia kwenye siasa na wanasiasa sikumwelewa kabisa. kwa nini suala hili liwe kama kampeni? Kwani benki hizo zilikopesha watu bila collaterals za kutosha kulipia madeni yao pindi wanaposhindwa kulipa kwa wakati? kama waliangalia sura tu kuwa huyu ni mheshimiwa acha tumpe, basi na wafilisiwe tu..ili wanyonge walioweka pesa zao huko wapate haki yao. Ujinga mtupu!
 
Kukopa benki si dhambi na kama benki itafilisika kuna mambo mengi sana ya kuangalia. Jee waliokopa walikopa hela hizo kwa ajili ya kufanyia nini na je benki ilijiridhisha kwamba miradi iliyokopewa hela italeta faida itakayorudisha mkopo?
Mkuu hiyo ndio nadharia lakini linapokuja suala la wanasiasa katika nchi hii nadharia na sheria zinawekwa pembeni mambo yanasonga. Huenda wengine walikopa kwa ajili ya kampeni ili wakipata vyeo walipe kwa kutumia mapato yanayotokana na siasa; hayapo sasa!!
 
Kimbunga hili ndilo tatizo la nchi yetu kila kitu kinafanywa kisiasa na maamuzi yote makubwa ya nchi yetu yako mikononi mwa wanasiasa. Hata hiyo NBC ilipouzwa ni wanasiasa peke yao tena bila hata ya wao wenyewe kwa wenyewe kushirikishana ndiyo waliamua benki hiyo iuzwe.
 
Allen Kilewella
Mkuu juzi wakati raisi anaongea na wahariri wa vyombo vya habari alikuwa analalamika sana kwa kusema kwamba benki hii Twiga imefisilika kwa sababu watu wamekopa hawajarudisha wengi ni wanasiasa.
Kama ntakuwa nakosea utanikosoa ninavyojua mimi utaratibu wa kukopesha pesa una taratibu zake na masharti yake unapoenda kukopa pesa au kuna benki kama Twiga wao wanaangalia sura za watu maarufu ndo wanapewa mkopo?Je baada ya kukopa pesa na kushindwa kurudisha kuna hatua zinafuata kwa wahusika waliokopa ? Nisaidie kwanza hapo mkuu.
 
Kukopa benki si dhambi na kama benki itafilisika kuna mambo mengi sana ya kuangalia. Jee waliokopa walikopa hela hizo kwa ajili ya kufanyia nini na je benki ilijiridhisha kwamba miradi iliyokopewa hela italeta faida itakayorudisha mkopo?
kwa hiyo unataka wasirudi....aisee unatia aibu sana...kulipa deni ni wajibu usitake kuleta siasa za mbowe hapa.
 
kuna benki kama Twiga wao wanaangalia sura za watu maarufu ndo wanapewa mkopo? Nisaidie kwanza hapo mkuu.

Tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyotaka lionekane. Kufanya biashara ya kibenki ni sayansi ya biashara ambayo ina kanuni zake, lakini kwa nchi kama Tanzania wanasiasa ndiyo hizo kanuni zenyewe. Kama Rais anaweza kuamua hela zitumike vipi bila ya kupitia Bungeni, basi ujue tuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo ya kuendesha nchi yetu.
 
kwa hiyo unataka wasirudi....aisee unatia aibu sana...kulipa deni ni wajibu usitake kuleta siasa za mbowe hapa.
Huu ni mwendelezo wa Kagoda, Meremeta,Tangold,Escrow,EPA, ambazo kila tunapokaribia kwenye uchaguzi lazima CCM waibe pesa za umma kufanikisha mambo yao ya kulazimisha kubakia madarakani! Kwa hisani Allen Kilewella
 
Tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyotaka lionekane. Kufanya biashara ya kibenki ni sayansi ya biashara ambayo ina kanuni zake, lakini kwa nchi kama Tanzania wanasiasa ndiyo hizo kanuni zenyewe. Kama Rais anaweza kuamua hela zitumike vipi bila ya kupitia Bungeni, basi ujue tuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo ya kuendesha nchi yetu.
Kwa hali hiyo kufanya maamuzi hivyo benki nyingi sana zitafilisika kwenye utawala huo JPM.
Nashangaa hili swala raisi kuhamisha pesa kwenye matumizi mengine bila kupitia bungeni. Tatizo la nchi yetu ni mfumo raisi amepewa madaraka makubwa sana ndo maana anafanya anavyotaka yeye hata kama anakosea.
 
Back
Top Bottom