Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,948
Wakili wa serikali Mulwambo ametoa somo kwa wanasheria na watu wengine kuwa kwa vile IGA ni makubaliano ya kimataifa kiitifaki inapaswa kuangaliwa dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo kupitia sheria za Tanzania

He implored the Court to place the IGA on one hand and the Constitution on the other, as opposed to placing the IGA on one hand and laws and processes on the other hand. Learned counsel urged the Court to exercise restraint in deciding whether the IGA conflicts with the laws. At the end of the day, he argued, the expected word from the Court is whether the IGA contravenes the provisions of the Constitution
 
Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.

Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"

Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.

Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.

=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):

Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.

Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"

Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"

Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.

Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).

The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.

Ifahamike kwamba The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ni mkataba wa kimataifa ambao serikali ya Tanzania iliusaini mwaka 1976 na kuutungia sheria maalumu ya bunge (Ratified). Hivyo ilikuwa ni sahihi kuutumia mahakamani kwa sheria ya bunge inayoruhusu utumike ndani ya mahakama zetu.

Anyway,
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.
 
Wewe unaona alichokisema Mulwambo kiko sawa kwenye mantiki ya sheria, ???
Mimi kwenye mantiki ya maisha ya kawaida siyo sheria ninaona Mulwambo yuko sawa. Unajua katika maisha ya kawaida na kuheshimiana rais anapokelewa na rais, mzee wa mji anapokelewa na mzee mwenzake. Kwa uelewa wang mdogo wa sheria na sheria za kimataifa pia nadhani yuko sahihi kwa sababu ukitumia sheria za ndani utakuwa unajenga mazingira ya kuonekana kutotenda haki
 
Mkuu, kwa heshima ya mjadala huu unaweza kutupa kilichotokea Kenya

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.
 
Mimi kwenye mantiki ya maisha ya kawaida siyo sheria ninaona Mulwambo yuko sawa. Unajua katika maisha ya kawaida na kuheshimiana rais anapokelewa na rais, mzee wa mji anapokelewa na mzee mwenzake. Kwa uelewa wang mdogo wa sheria na sheria za kimataifa pia nadhani yuko sahihi kwa sababu ukitumia sheria za ndani utakuwa unajenga mazingira ya kuonekana kutotenda haki
Hata KATIBA ni sheria ya ndani ambayo inazaa sheria nyingine zote.
 
Mkuu, kwa heshima ya mjadala huu unaweza kutupa kilicho sema na Kenya

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.
Mkuu, mimi siyo mshauri wa serikali ya Tanzania, ninyi fanyeni tafiti mtapata majawabu yote.

Ila fahamu kwamba Kenya ndiyo nchi pekee ya kwanza hapa barani Africa kuweza kuyashinda haya mabeberu kutumia sheria, ikifuatiwa na nchi ya Ghana. Wanasheria wa hizi nchi mbili wamefanya makubwa mno kwa nchi zao, naamini mawakili wetu wana kikubwa cha kujifunza.
 
Wote hawataki au hawako tayari nadhani kwa sababu wanajiita learned brothers
 
Mkuu, kwa heshima ya mjadala huu unaweza kutupa kilichotokea Kenya

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.
Je hayo ndio yalikuwa maombi ya Team yenu?Si mlitaka tafsiri tu na mahakama imetoa.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Wakili wa serikali Mulwambo ametoa somo kwa wanasheria na watu wengine kuwa kwa vile IGA ni makubaliano ya kimataifa kiitifaki inapaswa kuangaliwa dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo kupitia sheria za Tanzania

He implored the Court to place the IGA on one hand and the Constitution on the other, as opposed to placing the IGA on one hand and laws and processes on the other hand. Learned counsel urged the Court to exercise restraint in deciding whether the IGA conflicts with the laws. At the end of the day, he argued, the expected word from the Court is whether the IGA contravenes the provisions of the Constitution
Silly arguments, utetezi wa kitoto.
 
Sahihi sana sana.hata andiko langu la.leo aaubuhi kabla ya hukumu hii niliandika jinsi gani team.Mwabukusi walifanya blander ya kuchallange IGA kwa backup ya Sheria ya Natural Wealth & Resource(Parmanent Sovereignty)2017 makosa makubwa ya kiufundi.

Lakini pia IGA ingeweza kuwa challanged katika mahakama za Kimatifa za migogoro ya Uwekezaji na sio hapa kwetu.

Sasa Mwabukusi na team yake wanaweza kusimama kwenye hayo majukwaa?Nina wasiwasi nao sana

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Huyu Mulwambo mbona hajawahi tetea nchi yetu kesi za kukamatwa ndege, ndio maana rostam akasema hakuna mahakama nchi hii, inapigwa simu moja tu kisutu jaji anaachia p umbi
 
Sahihi sana sana.hata andiko langu la.leo aaubuhi kabla ya hukumu hii niliandika jinsi gani team.Mwabukusi walifanya blander ya kuchallange IGA kwa backup ya Sheria ya Natural Wealth & Resource(Parmanent Sovereignty)2017 makosa makubwa ya kiufundi.

Lakini pia IGA ingeweza kuwa challanged katika mahakama za Kimatifa za migogoro ya Uwekezaji na sio hapa kwetu.

Sasa Mwabukusi na team yake wanaweza kusimama kwenye hayo majukwaa?Nina wasiwasi nao sana

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Wanaweza
 
Mkuu uko sahihi ila ni sahihi pia ukatofautisha Sheria Katiba VS Sheria sheria
Mkuu Comte, hebu nisikilize vizuri kwenye hili,

Chini ya sheria za kimataifa, sheria zote za ndani ya nchi huitwa Municipal Law. Hapa wanajumuisha sheria (Ordinary Statutes/Legislations), sheria ndogo (Subordinate/Delegated Legislations) na Katiba (The Constitution). Katiba ni kubwa kwenu Tanzania, lakini huko duniani huchukuliwa kama sheria nyingine tu. Ila kubwa zaidi lazima ufahamu kwamba Tanzania inatumia mfumo wa sheria wa Dualism.

A Dualist State separates international law from municipal law. Henceforth, the Constitution is a law like any other law in the country. Prof Herch Lauterpatch anasema haya kuhusu hili:

"the self-evident principle of international law that a State cannot invoke its municipal law as the reason for the non-fulfillment of its international obligations"

Kiufupi huwezi kutumia sheria za ndani, KATIBA ikiwemo kukimbia wajibu ambao unatakiwa kuutimiza chini ya sheria za kimataifa, ikiwemo mikataba. Mulwambo anaposema KATIBA inatumika anataka kutunga sheria zake binafsi.

============================================================
Kama Jaji Ndunguru amekubaliana na hii kauli ya Mulwambo ambayo umeileta hapa kumsifia na kuwatuka wakina Mwabukusi, basi tuna safari ndefu mno ili kufika nchi ya ahadi. Mulwambo alitakiwa kufahamu mwanzo kabisa kwamba Tanzania is a Dualist State.
 
Sahihi sana sana.hata andiko langu la.leo aaubuhi kabla ya hukumu hii niliandika jinsi gani team.Mwabukusi walifanya blander ya kuchallange IGA kwa backup ya Sheria ya Natural Wealth & Resource(Parmanent Sovereignty)2017 makosa makubwa ya kiufundi.

Lakini pia IGA ingeweza kuwa challanged katika mahakama za Kimatifa za migogoro ya Uwekezaji na sio hapa kwetu.

Sasa Mwabukusi na team yake wanaweza kusimama kwenye hayo majukwaa?Nina wasiwasi nao sana

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Hebu tusaidiane katika hili ili tusiwachanganye watanzania:

Mosi, kipengele gani cha IGA kinasema wataenda kwenye mahakama za uwekezaji, ???

Pili, nani anatakiwa kwenda kupeleka kesi kwenye hizo mahakama za kimataifa, ???

Tatu, Hivi kwenye hizo mahakama za kimataifa za uwekezaji nchi inaweza kuishitaki nchi, ???

NB: Tukiweza kujibu hapa tutakuwa tumejenga msingi mzuri kabisa wa mjadala wetu wa sheria.
 
Ni lini Tanzania ilishinda kwenye mahakama za nje?
 
Mkuu Comte, hebu nisikilize vizuri kwenye hili,

Chini ya sheria za kimataifa, sheria zote za ndani ya nchi huitwa Municipal Law. Hapa wanajumuisha sheria (Ordinary Statutes/Legislations), sheria ndogo (Subordinate/Delegated Legislations) na Katiba (The Constitution). Katiba ni kubwa kwenu Tanzania, lakini huko duniani huchukuliwa kama sheria nyingine tu. Ila kubwa zaidi lazima ufahamu kwamba Tanzania inatumia mfumo wa sheria wa Dualism.

A Dualist State separates international law from municipal law. Henceforth, the Constitution is a law like any other law in the country. Prof Herch Lauterpatch anasema haya kuhusu hili:

"the self-evident principle of international law that a State cannot invoke its municipal law as the reason for the non-fulfillment of its international obligations"

Kiufupi huwezi kutumia sheria za ndani, KATIBA ikiwemo kukimbia wajibu ambao unatakiwa kuutimiza chini ya sheria za kimataifa, ikiwemo mikataba. Mulwambo anaposema KATIBA inatumika anataka kutunga sheria zake binafsi.

============================================================
Kama Jaji Ndunguru amekubaliana na hii kauli ya Mulwambo ambayo umeileta hapa kumsifia na kuwatuka wakina Mwabukusi, basi tuna safari ndefu mno ili kufika nchi ya ahadi. Mulwambo alitakiwa kufahamu mwanzo kabisa kwamba Tanzania is a Dualist State.
Mkuu, Mahakama imekubaliana na hoja za Mulwambo pamoja na masahihisho uliyofanya kwamba sheria katiba na sheria sheria (Municipal laws hazina) bearing yoyote kwenye IGA
Hukumu uk. 56 wanasema:
Overall, we are settled in our view that, since the parties were competent and with capacity to enter into trade and investment cooperation agreement, the signing of the IGA was not shrouded in any irregularity whichwould render it invalid or illegal. We are also settled in our minds that IGA is an international agreement whose oversight framework is not the LCA. We conclude that, to the extent this is not a normal contract, section 25 of the LCA is, in the circumstances of this case, immaterial.
 
Back
Top Bottom