Wakili Peter Madeleka: Mimi na mke wangu tulikamatwa na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi, nitawashtaki

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
WAKILI PETER MADELEKA: MIMI NA MKE WANGU TULIKAMATWA NA KUSHTAKIWA KWA UHUJUMU UCHUMI, NITAWASHTAKI

Source : mubashara studio

KESI Na. 10 ya mwaka 2021 SERIKALI YADAIWA FIDIA YA MALI
Wakili Peter Madeleka na mkewe, Jamila Augustine Ilomo wameishitaki Serikali wakidai fidia ya mali kwa kukaa gerezani kama mahabusu kwa zaidi ya miezi 18 na baadaye kuachiwa buru baada ya makubaliano na DPP.
Katika kesi Na. 10 ya mwaka 2021 aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Madeleka anadai fidia kwa kusababishiwa hasara na kushushiwa hadhi mbele ya jamii kwa kitendo cha kushitakiwa kwa tuhuma ambazo Serikali imeshindwa kuzithibitisha.

Kisa kilivyoanza
Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi, Wakili Madeleka, aliyewahi kuwa ofisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha mkaguzi kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 2016, alisema kisa kilianza baada ya kuhamia jijini Arusha na kufungua ofisi yake ya uwakili.

“Niliamua kuhamia Arusha nikimfuata mke wangu aliyekuwa ofisa uhamiaji. Yeye pia alikuwa mwanasheria kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo, anasema mambo yalianza kubadilika baada ya kazi yake ya uwakili kuanza kupata mafanikio.
“Mimi kazi yangu ni kwenda kuwatetea watu wenye matatizo ya kisheria, wakiwemo waliokamatwa na uhamiaji. Siwezi kuwakataa watu waliokamatwa na uhamiaji anakofanya kazi mke wangu.

“Kukawa na malalamiko kutoka Idara ya Uhamiaji wakisema kuna mgongano wa kimasilahi. Mimi nikawaeleza kuwa kuoana na ofisa wao si kosa kisheria,” alisema.

Baadaye malalamiko yalipozidi, anasema alimwandikia barua Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kumjulisha malalamiko hayo na kwamba hana hatia. Lakini anasema barua hiyo ilimgeuka.

“Nilipomwandikia barua hiyo Kamishna Jenerali mwaka 2017, hatua iliyofuata ikawa ni kuhamishwa kwa mke wangu kutoka Arusha kwenda Singida na familia yetu iliathirika.

“Mimi nikamwambia mke wangu aache kazi, wakati huo alikuwa na nyota tatu na amesomea sheria. Aliporudi tukaendelea na kazi zetu za uwakili,” anasema.

Kesi ndani ya kesi
Ilipofika Agosti 2, 2019 ikatokea kesi inayohusu idara ya uhamiaji ambayo pia alikwenda kutetea wateja wake.

“Kuna mtu alitoka Afrika Kusini, alikamatwa akiwa na visa feki za Tanzania. Agosti 11, 2019 mtu huyo akapelekwa mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa kamishna wa sheria wa uhamiaji. Mimi nikaenda kumtetea huyo kamishna baada ya kuombwa na ndugu zake,” anasema.

Alisema kitendo hicho kiliibua hasira ya uhamiaji na hapo mzozo mpya ukaanza. “Kwa hiyo nilipokuwa katika harakati za kumtetea yule kamishna ndipo nilikamatwa mimi, mke wangu pamoja na wakili mmoja aliyekuwa kwenye ofisi yangu,” anasema.

Anasema wakati kesi ikiwa imetajwa mara mbili, polisi walikwenda kwenye nyumba aliyofikia Upanga na kumkamata.

“Siku hiyo hiyo, mke wangu aliyekuwa Arusha naye akakamatwa na yule wakili mwingine, wakasafirishwa kuja Dar es Salaam, tukaunganishwa kwenye hiyo kesi ya visa feki.”

Anasema walifikishwa mahakamani Agosti 25, 2019 wakihusishwa na utengenezaji wa visa feki na kosa la utakatishaji fedha.

“Ilikuwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019. Tukapelekwa gereza la Segerea ambako tulikaa miezi saba,” alisema.

Kuanzia Agosti 25, 2019 alisema walikuwa wanahudhuria mahakamani na kuambiwa upelelezi unaendelea hadi Mei 12, 2020 Serikali iliposema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ikafutwa wakaachiwa huru.

“Wakati tunatoka mahakamani Kisutu tukijiandaa kwenda nyumbani, tukakamatwa tena na kuambiwa tuna kesi nyingine inayotukabili Arusha, hivyo tuko chini ya ulinzi, tukapelekwa Kituo cha Polisi Mburahati tukalala mpaka Mei 13, 2020 tukasafirishwa kwenda Arusha.”

Anasema wakiwa Arusha Mei 14, 2020 wakapelekwa mahakama ya Arusha wakituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hivyo baada ya kesi kutajwa wakapelekwa gereza la Kisongo ambako walikaa miezi 11 na siku 13.

Anasema huko nako kesi ilikuwa ikitajwa lakini haiendelei. “Nilijaribu kumwandikia barua Jaji anayesikiliza kesi na hakimu kwa kuwa niliona kesi yenyewe ni ya kunikomoa tu, lakini walikuwa wakipiga chenga.”

Hata hivyo, anasema ilipofika Machi 30, 2021, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), (sasa Jaji Biswalo Mganga), alitembelea gereza la Kisongo na kumtafuta.

“Alisema siwezi kutoka gerezani mpaka tufanye makubaliano, vinginevyo, nitaozea huko gerezani,” anasema.

Alisema baada ya ujumbe huo, mwakilishi wa DPP Mkoa wa Arusha alimwandikia barua mkuu wa magereza mkoani humo akiwaarifu watuhumiwa wanaotaka kumaliza kesi kwa majadiliano na DPP waandike barua.

“Kwa hiyo na mimi nikaandika barua, lakini nikijua kwamba utaratibu anaoagiza wa plea bargain umekosewa.

“Mimi nikafanya hivyo, Nikapeleka hizo fedha zilikuwa Sh2 milioni kwenye akaunti ya DPP ya BoT. Aprili 27 mwaka huu nikaitwa mahakamani, DPP akasema ameshakubaliana na mimi, akaomba mahakama iniachie.”

Baada ya kutoka jela Madeleka na mkewe sasa wamefungua kesi wakitaka walipwe fidia na Serikali, japo anasema kiasi cha fidia hiyo kitaamuliwa na mahakama.

Kuhusu kesi ya pili, Madeleka anasema bado yuko mbioni kufungua nyingine kupinga mchakato wa plea bargain uliomfanya akiri kosa na kulipa Sh2 milioni.

“Kiutaratibu, plea bargain inatakiwa ifanywe na mwendesha mashtaka wa kesi husika, lakini DPP alitaka afuatwe Dodoma, halafu yeye ndiye ajadiliane na mtuhumiwa na fedha ziwekwe kwenye akaunti yake iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 21(3(a) ya kanuni za plea bargain zilizotiwa saini na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, zinasema anayetakiwa kulipwa fedha ni msajili wa hazina ambaye yuko chini ya Wizara ya Fedha,” alisema.

Anaitaja pia kanuni ya 23 inayosema; kama plea bargain itafanyika kinyume cha hapo kwa namna yoyote ile basi aliyefanya plea bargain anaweza kwenda mahakamani na hiyo hukumu itatenguliwa.

Source : Wakili aeleza walivyosota gerezani na mkewe miezi 18, waamua kudai fidia | Mwananchi
 
IMG_0070.jpg


hii ndio dunia !

ukweli na haki zipo mbinguni tu ambako hatupafahamu !
 
KWa Sasa tulipo fika ukionewa ni kushitaki tu , tena wengine KWa majina yao
Hivi hawa watu wanaowakamata wenzao tena wazazi wote wawili wenye watoto wadogo Kwa kesi za kupikwa, ingekuwa wao wangejisikiaje?? Watoto wanateseka Kwa kukosa malezi bora kisa binadamu wenzako?? Huku watoto wao wakifurahia maisha. Kwanini watoto hao wasijekuwa kina Hamza baadae??? Nchi hii imejaa watu wabaya Sana. Mungu atawaadhibu Kwa kadri awezavyo.
 
Safi sana Ndugu wakili, haya masheria ya kikoloni ni vyema yaondolewe moja kwa moja!! Akipatikana kiongozi mwingine kama Mwendazake anayependa visasi, uungu mtu na kukomoana tutarudi kule kule!! Haiwezekani umweke mtu ndani miezi 18 kifala fala hivyo halafu huna ushahidi wowote wa kumfunga, KILA SIKU UNALETA MAHAKAMANI UPUUZI WA UPELELEZI UNAENDELEA, Thats stupid
 
Hivi hawa watu wanaowakamata wenzao tena wazazi wote wawili wenye watoto wadogo Kwa kesi za kupikwa, ingekuwa wao wangejisikiaje?? Watoto wanateseka Kwa kukosa malezi bora kisa binadamu wenzako?? Huku watoto wao wakifurahia maisha. Kwanini watoto hao wasijekuwa kina Hamza baadae??? Nchi hii imejaa watu wabaya Sana. Mungu atawaadhibu Kwa kadri awezavyo.
Usicheze na Mijitu katili
 
fasiliteta
Umesema ukweli kabisa, inawezekana kuna kitu kaficha, wanasheria na wengi na mawakili wengi ujanjajanja ni mwingi sana!
Nilivyomsikia anasema kuna sehemu kuna mapungufu kwenye sheria, hivyo anatumia mapungufu hayo kuwatetea waalifu/wahamiaji haramu!
 
Nilikuwa namchukia magufuli tangu akiwa waziri nilikuwa haamini hakuwa kiongozi Bora.nilishangaa siku anateuliwa kuwa mgombea uraisi. Nilijua wengi wangehangaika na kutaabika sana kwakuwa chini yake
POLE SANA KAKA PETER MADELEKA.
HATA MM NILIAMUA KUACHA KAZI KWENYE UTUMISHI WA UMMA KWA SABABU YA MAGUFULI
 
"Napendekeza Rais ateue kamati ichunguze ubambikizaji wa kesi. Kuachia huru mahabusu bila maelezo ya kina inachafua jina la serikali na hata heshima ya CCM. CCM ijisahihishe ijadili suala hili" - MwanaLumumba kijiweni
 
Back
Top Bottom