Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 5,277
- 8,003
Ni wazi hakuna ubishi Man of The Moment (MOTM) kwa sasa ni Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na namna alivyolibeba suala la Bandari/DP WORLD kwa mabega mawili. Wanasiasa na Wanaharakati wengi wameongea kama kina Lissu, Mbowe, Slaa, Tibaijuka, Shivji, Binti Sarungi, Madeleka na Nshala.
Lakini ni Wakili Boniphace Mwabukusi ndiyo maneno yake na haiba yake yana mvuto kuliko mtu yeyote. Mwabukusi ana uwezo wa kuwasilisha mada kwenye hadhara kama Wahubiri wa Kilokole akina Mwamposa/ Gwajima, ana maneno makali kama Mdude na ana uwezo kuchambua sheria kama Lissu.
Swali:
Je, huyu Bwana alikuwa wapi wakati wa Dikteta Magufuli 2015-21? Alipobana kabisa uhuru wa maoni na kukanyaga katiba
Je, kwa huu ubingwa wake, nini ingekuwa hatma yake kipindi cha Magufuli?