Namkubali sana Wakili msomi Mwabukusi lakini...

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,929
Katikati situation aliyonayo anapaswa kutulia sana na kwenye baadhi ya maamuzi anapaswa kutafakari kwa muda kabla hajaongea.

Matamshi ni kama kama risasi hayana rivasi, yakitoka yametoka, kifuatacho watu wanaweza kusamehe lakini sio kusahau natambua umakini wake.

Natambua uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, kuchambua na kushawishi ili ukubaliane naye, natambua uthubutu wake linapikuja suala la haki na kuipigania Tanganyika. Yaani kuna wakati anaongea yeye wanatetemeka wengine.

Nia yake ni thabiti na uhalisia wake unauona kabisa kwenye matamshi yake na body language yake, lakini amakinike mno na mfumo maana hauishiwi mbinu za kukwamisha ama kufelisha mambo! Juzi OCD wa Mbeya alimuingiza mtegoni kizembe sana.

Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda kulalamika polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA.

Hivi kweli wakili msomi Mwabukusi alishindwa kuuona mtego hapo? Ni lini polisi wamekuwa wema kiasi hicho cha kuchukua hatua za haraka walipopata malalamiko ya CHADEMA? Kuna kesi ngapi polisi za uonevu, za kubambikwa za kusingiziwa za viongozi na wanachama wa CHADEMA kila mahali Tanganyika ambazo zinasuasua mpaka kesho?

Hekima ya CHADEMA iliepusha mfarakano mkubwa sana! CHADEMA kabla ya kujibu kwa haraka tuhuma hizo walichukua muda kujiridhisha kwamba hizo taarifa zilikuwa za uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa. Baada ya hapo ndio kupitia kiongozi wa eneo husika alimtafuta Mwabukusi na kumwambia hali halisi kwamba hakuna mahali popote CHADEMA ilifanya hivyo.

Wakili msomi Mwabukusi ni mnyenyekevu na mkweli sana baada ya taarifa hiyo aliita waandishi wa habari na kuwapa mrejesho huo huku akiapa kumburuza kortini OCD.

Mwabukusi amakinike na timu aliyonayo! Sina mashaka na Mdude lakini kwa Dr. Slaa kuna ukungu. Ukimsikiliza kwa makini katikati ya matamshi yake kuna vitu haviko sawa sana! Kwa mfano alipopata wasaa wa kuwasalimia Wanambeya waliokusanyika nyumbani kwa Mwabukusi alitoa mfano wa kushangaza kwamba bunge lisiwe la chama kimoja tu bali kuwe walau na uwiano! Akatoa mfano CCM ikiwa na wabunge 200 basi wengine wawe na wabunge 100

What a grave mistake! Hapo alijidhihiri anasimamia nini na anaamini nini. Kwamba bado ana imani kubwa na CCM kuliko vyama vingine! Katika nyakati hizi za harakati kubwa za kuiondoa CCM madarakani, mpiganaji mpambanaji kamwe hawezi kuongea kitu kama hicho! Sitaki kumuita Dr. Slaa pandikizi, lakini nyayo zake zimechafuka!

Kuhusu Buberwa kila nikimuangalia yuko moderate sana na mara nyingi sauti yake haiakisi uhai na uhalisia!

Huu ni mtazamo wangu binafsi.
 
CCM ikiwa na wabunge 200 Basi wengine wawe na 100- Dr.Slaa...


Kwa kauli hii inaakisije yeye kuwa na imani na CCM ?!!

Ikumbukwe IMANI pia si lazima liwe jambo la UHALISIA....

Je ikiwa IMANI yake ni thabiti dhidi ya CCM inawezaje kuuondoa UHALISIA kuwa CCM ina NGUVU majimboni zaidi ya vyama vyengine?!!!

Mfumo wake madhubuti kuanzia NYUMBA 10 za "wajumbe" unaweza kuletewa "mbango" kuwa ni DHAIFU na kukosa mchango katika ushindi wa chama majimboni ?!!!

#Siempre JMT
 
Katikati situation aliyonayo anapaswa kutulia sana na kwenye baadhi ya maamuzi anapaswa kutafakari kwa muda kabla hajaongea
Matamshi ni kama kama risasi hayana rivasi, yakitoka yametoka... Kifuatacho watu wanaweza kusamehe lakini sio kusahau
Natambua umakini wake
Natambua uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, kuchambua na kushawishi ili ukubaliane naye
Natambua uthubutu wake linapikuja suala la haki na kuipigania Tanganyika ... Yaani kuna wakati anaongea yeye wanatetemeka wengine

Nia yake ni thabiti na uhalisia wake unauona kabisa kwenye matamshi yake na body language yake! Lakini amakinike mno na mfumo maana hauishiwi mbinu za kukwamisha ama kufelisha mambo! Juzi OCD wa Mbeya alimuingiza mtegoni kizembe sana..

Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda KULALAMIKA polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi.. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA

Hivi kweli wakili msomi Mwabukusi alishindwa kuuona mtego hapo? Ni lini polisi wamekuwa wema kiasi hicho cha kuchukua hatua za haraka walipopata malalamiko ya CHADEMA? Kuna kesi ngapi polisi za uonevu, za kubambikwa za kusingiziwa za viongozi na wanachama wa CHADEMA kila mahali Tanganyika ambazo zinasuasua mpaka kesho?

Hekima ya CHADEMA iliepusha mfarakano mkubwa sana! CHADEMA kabla ya kujibu kwa haraka tuhuma hizo walichukua muda kujiridhisha kwamba hizo taarifa zilikuwa za uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa.. Baada ya hapo ndio kupitia kiongozi wa eneo husika alimtafuta Mwabukusi na kumwambia hali halisi kwamba hakuna mahali popote CHADEMA ilifanya hivyo

Wakili msomi Mwabukusi ni mnyenyekevu na mkweli sana baada ya taarifa hiyo aliita waandishi wa habari na kuwapa mrejesho huo huku akiapa kumburuza kortini OCD

Mwabukusi amakinike na timu aliyonayo! Sina mashaka na Mdude.. Lakini kwa Dr. Slaa kuna ukungu.. Ukimsikiliza kwa makini katikati ya matamshi yake kuna vitu haviko sawa sana! Kwa mfano alipopata wasaa wa kuwasalimia Wanambeya waliokusanyika nyumbani kwa Mwabukusi alitoa mfano wa kushangaza kwamba bunge lisiwe la chama kimoja tu bali kuwe walau na uwiano! Akatoa mfano CCM ikiwa na wabunge 200 basi wengine wawe na wabunge 100

What a grave mistake! Hapo alijidhihiri anasimamia nini na anaamini nini... Kwamba bado ana imani kubwa na CCM kuliko vyama vingine! Katika nyakati hizi za harakati kubwa za kuiondoa CCM madarakani, mpiganaji mpambanaji kamwe hawezi kuongea kitu kama hicho! Sitaki kumuita Dr. Slaa pandikizi.. Lakini nyayo zake zimechafuka!

Kuhusu Buberwa kila nikimuangalia yuko moderate sana! Na maranyingi sauti yake haiakisi uhai na uhalisia..!
Huu ni mtazamo wangu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ulivyo sema ni mtazamo wako nami pia ni mtzamo wangu watatulia kama walivyotulia wengine hizo ni kelele za mafuta kuchanganyika na maji kwenye kikaango!
 
Tanganyika dola haipo.....

Kuitajataja ni sawa na kuondoa umakini katika masuala mtambuka ya hoja kuntu.....
014ab9329eb5b0ecf142dcdf7b743548.jpg
1ea3a383309b1d4c0f964172dee484cb.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani ni ngumu kwa Mwabukusi kuweza kuwa bora ktk kila nyanja. Ni kweli kwamba ni mzalendo, mbobezi wa sheria na mtu jasiri sana. Basi nyanja nyingine (hasa umakini) ambazo ana udhaifu inabidi asaidiwe.

Mwabukusi akiendelea hivi ataikomboa nchi hii. Ni suala la muda tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom