BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,120
"Tuna masuala ya kisheria na masuala ya kimaadili. Mfano nikitoka hapa kwenye kipindi nikasaula nguo zangu, nikashuka chini nikaanza kutembea sina chochote sio kosa la kisheria lakini ni kosa la kimaadili.
Na hamtoniamini kunileta kwenye kipindi kwa sababu kimaadili sio kitu sahihi lakini sio kosa kisheria kwamba huyu mtu ametembea uchi, sio kosa.
Kwahiyo inapofikia hatua mtu anasema nguo wanazovaa wanawake zinawashawishi wanaume wawabake sio kweli" - Wakili Getrude Dyabene, Kutoka Kituo Cha sheria na haki za Binadamu (LHRC)