Wakili: DOWANS itadhoofisha nchi

Wakili: DOWANS itadhoofisha nchi

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
4,465
Reaction score
1,172
• Ataja mashahidi walioiponza TANESCO ICC

na Happiness Katabazi

MMOJA wa mawakili mahiri wa kujitegemea nchini, Kennedy Fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.

Fungamtama aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti hili kupata taarifa kuwa wakili huyo ni miongoni mwa wanasheria walioisoma hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICC).

Mwanasheria huyo ambaye alimuelezea Sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za Watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya ICC, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili.

Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.

Wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si Waziri Sitta binafsi.

Fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma na kujiridhisha kwamba hukumu hiyo yenye kurasa 150 ya kesi namba 15947/VRO kati ya Kampuni ya Dowans na TANESCO ilipokewa na ICC Novemba 20, mwaka 2008 na ikatolewa hukumu Novemba 15 mwaka jana.

Alisema mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulisainiwa Juni 23, mwaka 2006 na mkataba huo unajulikana kama ‘Power Off - Take Aggreement (POA)" chini ya kifungu cha 14 (e) cha POA, na kufafanua kwamba pande zote mbili katika mkataba huo zilikubaliana kwamba uamuzi wa Mahakama ya ICC ndio utakuwa wa mwisho na utazibana pande zote mbili na hautaweza kukatiwa rufaa.

Fungamtama alisema kifungu cha 14 (f) cha POA, kinasomeka: "The parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability of this arbitration agreement or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this section."

Kwa tafsiri nyepesi, Fungamtama alisema kifungu hicho kinasema, TANESCO na Dowans katika mkataba wao walikubaliana kwa maandishi kuweka kando haki za kupinga au kuhoji mwenendo na tuzo zitakazotolewa na baraza la usuluhishi.

Alisema Waziri Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari akitaka serikali itumie kifungu cha 16 cha Sheria ya Tanzania ya Usuluhishi Sura ya 15 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwamba serikali inaweza kutumia kifungu hicho kutengua hukumu ya mahakama ile ya kimataifa.

"Ni kweli Mahakama Kuu ya Tanzania imepewa mamlaka ya kutengua maamuzi yanayotolewa na mahakama za kimataifa endapo tu itadhihirika kuwapo kwa mambo mawili yafuatayo:

Moja; msuluhishi wakati akiendesha kesi alikuwa akiegemea na kupendelea upande mmoja (arbitrator has miss - conducted himself. Pili: Mazingira ya kufikia uamuzi ule yalitawaliwa na rushwa au shauri lilifikishwa mahakamani bila kufuata taratibu za kisheria (an arbitration or award has been improperly procured).



"Hayo ndiyo mambo mawili peke yake yanayoweza kusababisha Mahakama Kuu ya hapa nchini kutengua hukumu zilizokwisha kutolewa na mahakama za kimataifa za usuluhishi na si kwa jambo jingine lolote.

"Sasa kama Sitta ana ushahidi, vigezo hivyo viwili vya kisheria katika lililokuwa shauri baina ya Dowans na TANESCO kwamba wasuluhishi wale ambao ni majaji waliipendelea Dawans, au walikura rushwa, ingekuwa ni vyema haraka apeleke ushahidi huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuwatuma wanasheria wake wakafungue kesi Mahakama Kuu ili iweze kutengua hukumu hiyo kupitia huo ushahidi wake kama anao na si kama anavyofanya hivi sasa kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari," alisema wakili huyo.

Aidha, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha jedwali la 3 katika Sheria ya Usuluhishi ya Tanzania, Sura ya 15 ya mwaka 2002 kinasomeka hivi:

"Each contract state undertakes to ensure the execution by its authorities and in accordance with the provisions of its national laws of arbitrarily awards made in its own territory under the preceding articles".


"Kwa tafsiri rahisi, kifungu hicho utaona tayari nchi imejifunga mikono na utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama za kimataifa kwa sababu ni nchi yetu yenyewe imeridhia sheria na mikataba ya kimataifa."

Alisema kwa hiyo maelezo ya Waziri Sitta ya kutaka Dowans isilipwe, ni kutaka kuishawishi serikali na umma kukaidi kutekeleza maamuzi halali chini ya sheria na mikataba ambayo serikali iliiridhia kuitii na kuitekeleza.

Aidha, alisema jambo jingine lililojitokeza wakati kesi hiyo ikiendelea baina ya Dowans na TANESCO ni TANESCO walitaka kujua wamiliki wa Dowans ni kina nani na Mahakama ya ICC iliona hoja hiyo ya TANESCO ya kutaka kumjua mmiliki haina umuhimu wowote katika mgogoro uliokuwa mbele yao na ikatupilia mbali, kwa sababu iliona hoja hiyo haina maana yoyote mbele yao.

"Kwa hiyo kwa kitendo cha Waziri Sitta kulianzisha suala hilo la kutaka kujua wamiliki wa Dowans wakati hoja hiyo tayari ilikwishatolewa uamuzi na ICC, kisheria hawezi kulianzisha tena jambo hilo la kutaka kujua wamiliki kwa njia anayoitumia ya vyombo vya habari.

"Kwa hiyo maelezo yote yanayoendelea kutolewa kuhusu hukumu hiyo ni kutaka kujinasua katika lawama wakati yeye na baadhi ya maswahiba zake enzi zile akiwa Spika wa Bunge ndio waliokuwa chanzo cha TANESCO kuvunja mkataba na Dowans, hivyo mwisho wa siku shirika hilo la umeme kujikuta likiburuzwa katika korti ya ICC.

"Na ifike mahala wananchi na vyombo vya habari na serikali itoke usingizini na ijiulize maswali yafuatayo kwamba Sitta hakuwepo kwenye usikilizwaji wa shauri hilo? Sitta hakuwa akijua kwamba TANESCO imefunguliwa kesi na Dowans katika Mahakama ya ICC?

"Kwa kuwa Sitta alikuwa mstari wa mbele kuzipiga vita Dowans na Richmond, ni wazi alikuwa akifahamu kwamba TANESCO imeburuzwa mahakamani na kama kweli Sitta ni mzalendo wa kweli na hana chuki binafsi katika hili ni kwanini hayo madai anayoyasema asingeiomba serikali imuweke kama shahidi wa upande wa TANESCO ili akatoe ushahidi anaousema kila kukicha kwenye vyombo vya habari?

"Amesubiri tayari shirika letu la umeme ambalo ndilo lilikuwa mdaiwa katika shauri hili limeshindwa kufurukuta kwenye kesi hiyo na tumetakiwa tulipe kiasi hicho kikubwa cha fidia ndiyo kila kukicha anazungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo,

tena ukitazama maoni anayoyatoa utafikiri si mtu aliyesomea sheria kabisa….naomba sana hasa serikali ipuuze ushauri wa Sitta kwani ni wazi kabisa anataka kuliingiza taifa kwenye matatizo mengine makubwa.

"Watanzania na huyo Waziri Sitta ambao hawajaisoma hukumu ile naomba niwaeleze wazi mimi nimeisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba, kama taifa kupitia hukumu hiyo tumeshikwa pabaya, hivyo hatuwezi kukata rufaa, isipokuwa tu kama tutathibitisha sababu zile mbili nilizozitaja," alisema wakili Fungamtama.

Aidha, Fungamtama aliviasa baadhi ya vikundi mbalimbali vya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuzungumzia hukumu hiyo ambayo hata wengine hawajawahi kuisoma wala kuiona, kwani tayari kuna baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika makala kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa TANESCO haijawahi kuleta shahidi hata mmoja kutoa ushahidi.

Jambo ambalo Fungamtama alisema si kweli na linalenga kuhadaa umma, kwani majibu na nakala ya hukumu hiyo ambayo anayo inaonyesha TANESCO ilipeleka mashahidi watano na walitoa ushahidi wao. Wakili huyo aliwataja mashahidi hao kuwa ni Subira Wandiba, ambaye ni Mwanasheria wa TANESCO, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Zabuni iliyotoa tenda kwa Dowans, Balozi Fulgence Kazaura, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idrisa Rashid, Mhasibu Mkuu wa shirika hilo, Jamhuri Ngeline na Boniface Njombe.

My Take:


1. Hizi hoja za huyu wakili mbona zinaonekana nipersonal attack kwa Sitta zaidi ya kujenga hoja kwa nini Dowans ilipwe. Kwa utaratiobu uliopo Tanzania miaka hii huyu jamaa ana interest gani hapa?

2.
Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.
Mbona Tanzania imeridhia kufuata haki za binadamu katika medani hiyo hiyo ya kimataifa na haifuati kama tulivyoona wiki iliyopita Arusha, je tumenyyimwa misaada? N hii concept ya misaada misaada mbona tumegota hapa tutatoka linni? Na ni wafadhili gani wanafurahia kuona hela za walipa kodi wao wanalipwa matapeli?

 
Tukatae kulipa halafu mmiliki ajitokeze kwenda kutushtaki ili tumfahamu
 
Kwa wanasheria nna maswali kidogo!

1. Hivi ukimuajiri mtu na under influence of joy or drugs and even alcohol mkawekeana maandishi kwamba ikitokea mkataba umevunjika kati yenu kwa sababu yeyote ile uttakiwa kumlipa mtu huyo sh milioni 100. Lakini baada ya miezi kama sita unagundua kwamba mtu huyo ni mmalawi na hana kibali cha kuishi nchini hivyo ukaamua kusitisha mkataba naye. Je ukigoma kumlipa ile Milioni 100 na akakupeleka mahakamani inakuwaje?

2. Au wewe una kiwanda cha matofali akaja mtu kuomba kazi ya uhandisi ukampa. Say Katika sheria za Tz mtuu haajiriwi kama mhandisi kama hayuko registered. Ila anakuwa exempted kama ni registered kwenye any of the common wealth countries. Mhandisi wako akakupa vyeti kuthibitisha kwamba yeye yuko registered India. Under similar influence of joy or drugs and even alcohol mkawekeana maandishi kwamba ikitokea mkataba umevunjika kati yenu kwa sababu yeyote ile utatakiwa kumlipa mtu huyo sh milioni 200. Lakini baada ya miezi kama sita unagundua kwamba mhandisi huyo hayuko registered India kama alivyodai unaamua kuvunja nae mkataba. Anakupeleka mahakamani kutaka m 200 zake wewe unagoma. Utaratibu unakuwaje ?
 
Kennedy Fungamtama is known for his corrupted mind.
 
Huyu wakili hata kama amesoma hiyo hukumu bado convincing yake kwamba tusihoji chochote ni poor.Sitta kama mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake kama yeye(Fungamtama) alivyotoa.Something fishy smells here though...With that amount of money somebody can be paid to be Dowans speaker...
 
hii cinema sijui itaisha lini,yaani kama movie la kihindi vile,halafu slow motion.
yangu macho
 
Fungamtama huwa ni wakili wa Rostam soma hii habari

THE High Court has ordered the Editor of ‘Mwanahalisi' newspaper and three other defendants to pay 3bn/- in damages to a prominent businessman, Mr Rostam Aziz, for publishing defamatory articles linking him with the Richmond scandal.

Judge Robert Makaramba entered the judgment on April 30, after the newspapers' editor, publisher and printers failed to give their defence against the suit lodged by Mr Rostam, who is also a Member of Parliament (MP) for Igunga on a Chama Cha Mapinduzi (CCM) ticket.

The newspaper is alleged to have defamed and disparaged the MP in its issue Number 084 of February 13-19, 2008, when it ran an article with his picture under headline 'Richmond ya Rostam Azizi, Ndiye aliyeileta nchini.'

According to the court's decree, the newspaper has been ordered to publish unconditional apology on the front page in similar or bigger font immediately and to retract the false and malicious publications complained of.

The court has further restrained the newspaper, their agents or otherwise howsoever from publishing news articles containing similar defamatory statements and pay the said amount, which attracts interest at court rate of 12 per cent and costs of the suit.

Advocate Kennedy Fungamtama, who represented the MP in the case, has already given the newspaper 14 days to comply with the court's decree, failure of which he shall institute execution proceedings against all the defendants.

When reached for comment, Advocate Gabriel Mnyele, for the defendants, said he would appeal to the Court of Appeal against both the court's decree and orders. Mr Rostam had stated in the suit that the heading and contents of the article published clearly indicated that he was a fraudster, dishonest, corrupt and guilty of dishonourable conduct and one of persons who participated in fraudulent dealings.

The MP also stated that the newspaper continued with its smear campaign in its Issue Number 085 dated February 20-26, 2008. The newspaper published another article at Page Two purporting to portray that he (Rostam) was the kind of person who would suppress the truth to suit his own ends.

Mr Aziz stated that the newspaper continued to publish similar news articles in its Issue Numbers 087 dated March 5-11, 2008 and Issue Number 093 of April 16-22, 2008, showing he was dishonourable and misused his position for his selfish interests.

He alleged that the offending words were calculated to disparage him in his business and career as MP, thus injuring his credit, character, integrity and reputation and has been brought into public scandal, hatred, ridicule, odium and contempt. Mr Rostam maintains that he has built up his reputation as a good citizen, businessman, politician and reliable person over several years. However, he says the offending articles had since been seriously lowered in the estimation of the right thinking members of society.


Fungamatama hapa anamtetea Mahanga Makongoro

THE High Court has ordered activist Kainerugaba Msemakweli and three other defendants to appear before it on March 23, this year, in the suit lodged against them by Ukonga Member of Parliament (MP) Makongoro Mahanga, demanding 3bn/- damages for libel.

According to a summons issued by the court's District Registrar Saul Kinemela and published by 'Daily News' last Friday, the defendants are required to show up either in person or by an advocate, failure of which the court will proceed with the matter in their absence.

The summons further indicates that the defendants are required to produce all documents on that day with which they intend to rely on in support of their defence case against the suit by Dr Mahanga, who is also the Deputy Minister for Labour, Employment and Youth Development.

Other defendants in the suit are Nipashe Newspaper reporter Muhibu Saidi, Managing Editor of Nipashe and its publisher -- the Guardian Limited.

Dr Mahanga is suing them for what he described as 'malicious publication of defamatory articles' against him.

The deputy minister says in the plaint of the suit that Mr Msemakweli convened a press conference on October 18, last year, in Dar es Salaam and told journalists that he was among politicians who are parading fake academic credentials.

Through his advocate, Kennedy Fungamtama, Dr Mahanga, who is also a member of National Executive Committee (NEC) of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), stated that Nipashe Newspaper published such defamatory statements by Msemakweli on October 19, last year.

During the press conference, he stated, Msemakweli claimed that the deputy minister was falsely claiming to be a holder of Doctor of Philosophy (PhD) degree. Such statements, according to Dr Mahanga, were defamatory and were tailored to injure his reputation in the society.

For that matter, he claimed, he was entitled to the damages of 3bn/- or as may be assessed by the court, but not less than 200m/-, as the words uttered and reproduced contained false, incorrect and distortions, aimed to tarnish his reputation as a good citizen and reliable person.
 
Naipendaa sana hii....hatimae pumba pembeni mchele huoo...RA anaanza kuonekana taratibuu
 
Hizo hela wanazolipwa DOWANS ni nyingi sana na watu wengi wameahidiwa mgao na hivyo ni budi kuwachunguza kwa kauri zao. Kwa huyu wakili under subject si tatizo kwa kuwa amekuwa anamtetea sana na kumwakilisha ktk kesi mbalimbali RA na rafiki yake Mh wa Ukonga.

Wazawa kwa kuitetea dowans mnashirki kuwaua Watz. Huo mgao wenu mnauthamanisha na maisha ya Watz walio ktk umaskini wa kutupwa, eti tutakosa misaada! To hell!
 
Hili ni tatizo la wataalam wetu kufikiria kutumia matumbo badala ya akili. Tunaishia kupata ushauri mbovu.
 
Fungamtama ni bogasi. Sababu zote mbili alizotoa hazina mantiki. Wafadhili wenyewe hawakubalini na tabia ya serikali kufuja hela wanazotupatia. Wafadhili hao wanajua historia nzima ya sakata hili na wanajua kuwa lina rushwa ndani yake. Pili wawekezaji nao wana akili kubwa sana ya kujua pumba na mchele. Serikali haitakataa kulipa bila sababu; sababu iliyowazi ni kuwa serikali haikuwa na mkataba wowote na Dowans, bali walikuwa na mkataba na Richmond na wala mkataba huo wa Richmond haukuwa na kipengele kinachoonyesha kuwa utaweza kuuzwa kwa kampuni nyingine ambayo haikuwa imetathminiwa na serikali. Dowans ilikurupuka na kuchukua mkataba wa Richmond ili kuficha udhaifu wa Richmond bila serikali kuwa imetathmini ubora wa kampuni hiyo.


Hebu angalia hii nayo:

Subira Wandiba, ambaye ni Mwanasheria wa TANESCO, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Zabuni iliyotoa tenda kwa Dowans
Dowans hawakupewa tenda yoyote na TANESCO; walichukua mkataba wa Richmond bila ridhaa ya TANESCO.
 
Dawa ni kugoma kulipa. Halafu tuone namna nchi itakavyodhoofika. Au tuone uyo mmiliki atajitokeza na kudai malipo yake!
 
kama ni kuzulumu bora tuzulumu.... tukiwazulumu wezi na mafisadi . ina maana...tuna zulumu haramu...hakuna kosa wala sidhani kama kuna nchi itakayotulaumu
 
Mimi nasisitiza ubaya wa majina yetu...yanatuathiri akili zetu....mara NUNDU sasa huyu FUNGAMTAMA...SIJUI MTAMA UMEKOSA NINI HATA UFUNGIWE
 
Back
Top Bottom