Kataeni kuwalipa muone yatayojiri. Mlishinikiza kuvunja mkataba sasa matokeo mnayaona.
Nyerere alijidai kuwataifisha LONRHO, ingawa taifisha yake ya Ma Benki na Mashamba Na Viwanda vya wazungu ilikuwa ya geresha kwani wote alikuwa akiwalipa, wote walilipwa, wasiolipwa ni waIslam tu waliokuwa na mali zao. Akajidai kuwalipa LONRHO anavyotaka yeye, mbona ilimtokea puani! Jee hamkumbuki? Kama wengi wenu hamkuwepo wakati huo, m-google mtazipata data.
Sasa haya ya Dowans tunapiga kelele na madudu tumefanya wenyewe, huwezi kuvunja mkataba na mtu aliyekwisha kuingia hasara ya kukuletea mlivyo ahidiana, labda viwe chini ya kiwango mlichokubaliana au viwe vibovu au awe hajavileta kabisa. Lakini hakuna sababu nyengine yoyote utayoitowa ukashinda, mahakama yoyote duniani labda iwe haifati haki.
Hili La Dowans, tutapiga kelele weee, at the end lazima lilipwe.