Mwanasayansi Kalivubha
Member
- Feb 4, 2024
- 67
- 204
WAKIKWAMBIA WAKO TAYARI KUKUPENDA NA UMASKINI WAKO KATAA KABISA HUO MTEGO,WATAKUSUMBUA MBELENI
Zipo kauli kuwa mapenzi sio pesa bali ni upendo tu wa moyo ndio unaamua mapenzi, hii ni kweli lakini sio kweli kwamba pesa haitakiwi mwenye mahusiano.
Usijazwe kichwa kwa maneno kuwa atakupenda tu jinsi ulivyo na umaskini wako ukaacha kutafuta pesa ukijua tayari unapendwa maana hutaamini kitakachokukuta.
Wanavyokwambia watakupenda tu jinsi ulivyo huwa kauli hiyo haidumu sana na ukitumia jicho la tatu kuichunguza kauli hiyo utagundua kuwa anayekwambia katumia busara kubwa kukwambia tafuta hela kwa lugha isiyo umiza kwani muda mfupi tu baada ya kauli hiyo utaanza kuombwa vitu vinavyohitaji pesa na hapo ndipo utagundua kumbe pesa bado ni muhimu kwenye mahusiano.
Maskini wanalalamika sana kwenye mahusiano na ukiwasikiliza vizuri sababu kubwa ni moja wameachwa kwa sababu hawana hela au wamesalitiwa kwa sababu hawana hela yaani wenye hela wamewachukulia wapenzi wao.
Kama kijana huatakiwi kujitetea sana kuwa upendwe na umaskini wako hiyo ni hatari sana kwa afya yako wewe tafuta tu pesa na iwe kazi kwake kukupenda ulivyo ama akuache na pesa zako.
Pesa sio kitu cha kwanza kwenye mahusiano ila pia umaskini sio sifa nzuri kwenye mahusiano hivyo pesa iwepo na umaskini utoweke ndio sababu nyingine za kukoleza mapenzi zifanye kazi.
Ukiona wanakwambia watakupenda tu ulivyo kataa huo mtego.
Mwanasayansi Saul kalivubha
fikia ndoto zako.