Wakenya tumwombee mwanzilishi wa Jamii Forums

Kuna taarifa kwamba mwanzilishi wa Jamii Forums ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao wetu huu maarufu wa Jamii Forums, Maxence Melo, amekamatwa na kushtakiwa kwa kugoma kutoa majina ya watumiaji wa huu mfumo. Nafikiri sheria ya Tanzania ilibadilishwa kwamba kila mtandao wa kijamii unahitajika kutoa majina na taarifa za watumiaji wake.

Hapa ni kwa sisi Wakenya wanachama wa JF, na hata Wabongo tunaokutana nao kila siku kwenye Kenyan section ya JF kuomba busara kutumika ili mambo yafanyike bila kufikia hatua au maamuzi ya huu mtandao kupigwa chini, maana kwa sasa upo maarufu Afrika Mashariki, sote tunakutana humu, tuna wachangiaji kutokea Rwanda, Kenya na hata Nigeria. Kwa kifupi tumekua jamii moja, ukiweka pembeni utani wa kutambiana.

Lakini pia tunafaa kuheshimu dola na mamlaka zetu, anyway kweli tumwombee Max.

NEWS ALERT: mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence melo ashikilwa na jeshi la polisi, kupanda kizimbani leo | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
Tumuombee na Ben Saa nane asiuawe huko aliko baada ya kupotea siku chache baada ya kuanzisha mjadala wa kuhoji PHD ya JPM!!
 
Watanzania unafik tuu ila wanaukabila nyoyoni kupita kiasi! Mbona wanafiki hivi?
Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 hivi na ushee hapa bongo..utamfanyia nani sasa huo ukabila? Ukabila huko active zaidi kama kuna makabila makubwa mawili au matatu ndani ya nchi na hayana any instrument of unification kama vile wabongo tunavyokuwa unified na lugha adhimu ya kiswahili.

Bongo nikikuuliza kabila ujue nataka tutaniane which in turn inakusaidia unaetaniwa kujishape upya na kuacha mabaya uliyonayo na hakuna kuchukia...ukichukia na kurusha ngumi nakusue mahakamani.

Kenya mkiulizana makabila basi ujue mnataka kubaguana na kuibua chuki.

Mungu awasaidie sana Kenya, maana tunawapenda sana our distant relatives ila mjue hates is the poison love is the remedy.

Sio kwamba we are perfect, no we embrace our similarities and tolerance our differences.
 
Tatizo jamii forum inaangaliwa kwenye makosa tu hawaoni faida zake ,mfano ishu ya yule Binti wa Raila Odinga aliyesema Oldupai Gorge ipo Kenya kwa umoja wetu tulipinga upotoshaji ule wa wazi

Au ishu ya Museveni kutaka kutumia bandari yetu ya Tanga ,ninyi Wakenya mkafanya lobbying zenu na propaganda kibao mpaka kumuingiza sijui kiongozi gani kwenye Chopa ambaye hakuwepo kwenye manifest kutembelea bandari ya Tanga ila kwa umoja wetu tulitetea hilo na maafisa uhamiaji walimzuia

Ukiacha na mitambo ya hapa na pale sisi na Wakenya ni ndugu
Wakifunga forum hii sijui ni nini kitatuleta pamoja

JF haiwezi kufungwa, domain yake imesajiliwa USA
 
Na ilihusika kikamilifu.
Huu mtandao hauwezi kupigwa chini, sema ameshikiliwa kwa muda baada ya hatua za awali kushindikana. Hakuna wasiwasi, sababu serikali ipo katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.

Naamini yuko salama na kuna baadhi ya mambo wanayaweka sawa.

Asante kwa kutuhakikishia usalama wake.
 
Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 hivi na ushee hapa bongo..utamfanyia nani sasa huo ukabila? Ukabila huko active zaidi kama kuna makabila makubwa mawili au matatu ndani ya nchi na hayana any instrument of unification kama vile wabongo tunavyokuwa unified na lugha adhimu ya kiswahili.

Bongo nikikuuliza kabila ujue nataka tutaniane which in turn inakusaidia unaetaniwa kujishape upya na kuacha mabaya uliyonayo na hakuna kuchukia...ukichukia na kurusha ngumi nakusue mahakamani.

Kenya mkiulizana makabila basi ujue mnataka kubaguana na kuibua chuki.

Mungu awasaidie sana Kenya, maana tunawapenda sana our distant relatives ila mjue hates is the poison love is the remedy.

Sio kwamba we are perfect, no we embrace our similarities and tolerance our differences.

Ubaguzi wa kikabila chanzo chake sio lugha, hili nimelisema mara nyingi. Somalia kule wanaongea lugha moja, dini moja lakini wanauana na kubaguana kwa misingi ya kiukoo.
Kenya, kuna sababu chache zilizotuponza hapo awali ndio vikasababisha ukabila, japo tunajaribu sana kupunguza.

- Muingereza alizoea kuwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila hata kabla ya uhuru, yaani divide and rule. Hivyo wakati anatuachia nchi, alikua tayari keshaachia sumu na mbegu ya ukabila imezagaa. Lakini Tanzania mambo yalikua tofauti, kwanza Muingereza aliwatawala akijua ataachia hivyo hakua na sababu za kung'ang'ania nchi yenu na akawaacha muishi bila vita au ugomvi wowote baina yenu.

- Pili, Muingereza wakati anaachia Kenya, alikabidhi uongozi kwa mtu wa kutokea kwa kabila kubwa, kabila langu la Wakikuyu. Hilo lilichangia pia, maana kwenu kaachia kwa mtu wa kabila ndogo sana, Mzanaki. Lakini angeachia uongozi kwa mtu wa kabila kubwa mfano Wachagga, mungekoma.

Zaidi nataka kusema, ubaguzi ni asili ya binadamu, huwa lazima tubaguane kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano hapo Bongo mnabaguana sana kwa misingi ya kidini, hilo nimeona hata video za masheikh wa kiislamu wakilalamika balaa.

Ubaguzi mwengine ambao upo duniani kote ni wa baina ya matajiri na maskini, walio nacho na wasiokua nacho. Huo upo Bongo, Kenya na hata Marekani.
 
Wewe Una akili sana na
Umeeleza Vyema.
 
Masunga Maziku
Jacob Juma kama ni yule namfahamu, huyo tayari ni maiti na keshazikwa hivyo maombi yetu kwake hayatakua na umuhimu.
Huyo aliuawa kinyama jameni, kumekua na tetesi system ya serikali ilihusika.

Anyway hii mada inamhusu mumiliki wa huu mtandao wetu wa JF maana kama vipi ukipigwa chini basi hatutakua hata na fursa ya kuagana.

Sipati picha jamii ya watu 300,000 sote tukipoteana ghafla. Tumuweke kwenye maombi.
Najua utawamiss sana Geza Ulole na bagamoyo.
 
Ubaguzi wa kikabila chanzo chake sio lugha, hili nimelisema mara nyingi. Somalia kule wanaongea lugha moja, dini moja lakini wanauana na kubaguana kwa misingi ya kiukoo.
Kenya, kuna sababu chache zilizotuponza hapo awali ndio vikasababisha ukabila, japo tunajaribu sana kupunguza.

- Muingereza alizoea kuwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila hata kabla ya uhuru, yaani divide and rule. Hivyo wakati anatuachia nchi, alikua tayari keshaachia sumu na mbegu ya ukabila imezagaa. Lakini Tanzania mambo yalikua tofauti, kwanza Muingereza aliwatawala akijua ataachia hivyo hakua na sababu za kung'ang'ania nchi yenu na akawaacha muishi bila vita au ugomvi wowote baina yenu.

- Pili, Muingereza wakati anaachia Kenya, alikabidhi uongozi kwa mtu wa kutokea kwa kabila kubwa, kabila langu la Wakikuyu. Hilo lilichangia pia, maana kwenu kaachia kwa mtu wa kabila ndogo sana, Mzanaki. Lakini angeachia uongozi kwa mtu wa kabila kubwa mfano Wachagga, mungekoma.

Zaidi nataka kusema, ubaguzi ni asili ya binadamu, huwa lazima tubaguane kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano hapo Bongo mnabaguana sana kwa misingi ya kidini, hilo nimeona hata video za masheikh wa kiislamu wakilalamika balaa.

Ubaguzi mwengine ambao upo duniani kote ni wa baina ya matajiri na maskini, walio nacho na wasiokua nacho. Huo upo Bongo, Kenya na hata Marekani.
Mimi na mtazamo tofauti kidogo na wewe, tukianzia kwa wasomali, wasomali wanachinjana kwasababu ya tamaa ya pesa. Wasomali wengi wanapenda pesa kuliko kitu kingine chichote, hakuna wa kumuachia mwingine na yeye ale. Kwa wao kabila moja, lugha moja na dini moja havija saidia kudumisha umoja wao, tamaa ya mali na pesa ndio inawatafuna Wasomalia. Naamini vita itaendelea hadi pale kizazi kilicho jaa ubinafsi na kupenda mali kita kufa na kupote. Somalia needs new breed of youth who are less selfish and more progressive.

Wakoloni kuipa kabila dogo utawala hauchangii kupunguza ukabila, Rwandan waliwachia kabila dogo kutawala, Zanzibar na wao hivyo hivyo, South Africa na wao waliwapa wazungu wachache. Sisemi kama huko hakuna ukabila, lakini kama ukipata kiongozi anayeweza kuunganisha makabila bila kujali maslahi yake binafsi au ya kabila lake, ukabila utapungua kwa asilimia kubwa sana katika nchi hiyo. Nyerele came from very small tribe, lakini alijitahidi kumpa kila mmoja nafasi japo kuna wengine waliona wanatakiwa kupewa zaidi. Mwisho wa siku alifanikiwa na kuacha Tanzania ikiwa na sura ya umoja. FYI wachanga sio kabila kubwa Tanzania, ni kabila dogo sana, usidanganyike kwa kuwaona wao kila upande wa nchi, huwezi kuwalinganisha na Wasukuma au Wanyakusa.
 
Tunashukuru sana kwa kutambua mchango wa JF katika kukuza tasnia ya habari na uhuru wa kutoa maoni kwa watu wote hasa waswahili duniani kote
Mkuu MK254 nikuombe sasa kuanzia muda mfupi ujao pia uanze kutupatia habari kuhusu uelekeo wa siasa za Kenya na elections for 2017.
 
Kwa sasa Kenya tunasubiri wapinzani waibuke na UKAWA wao ndio pawe patamu kisiasa. Wapo kwenye mazungumzo, wanaandaa kitu kinaitwa NASA, ambacho kinategemewa kuwaunganisha wapinzani wote. Tatizo lipo nani ataachiwa awe ndiye kama walivyofanya mwaka wa 2002.
 
Mimi na mtazamo tofauti kidogo na wewe....

We nae punguza ubishi na uwe unaelewa bas, what he says here:

" Muingereza alizoea kuwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila hata kabla ya uhuru, yaani divide and rule. Hivyo wakati anatuachia nchi, alikua tayari keshaachia sumu na mbegu ya ukabila imezagaa. Lakini Tanzania mambo yalikua tofauti, kwanza Muingereza aliwatawala akijua ataachia hivyo hakua na sababu za kung'ang'ania nchi yenu."

has a point. Afu ulivyo mbishi you couldn't overlook past wachaga kuwa kabila kubwa Tz.
 
We nae punguza ubishi na uwe unaelewa bas, what he says here:

" Muingereza alizoea kuwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila hata kabla ya uhuru, yaani divide and rule. Hivyo wakati anatuachia nchi, alikua tayari keshaachia sumu na mbegu ya ukabila imezagaa. Lakini Tanzania mambo yalikua tofauti, kwanza Muingereza aliwatawala akijua ataachia hivyo hakua na sababu za kung'ang'ania nchi yenu."
Hivi mzungu hapa Afrika alitawala kenya tuu? Miaka zaidi ya hamsini haitoshi kuondoa ukabila kenya?, na taifa lina watu wenye elimu nzuri ambao wanaelewa faida ya kuachana na vitu vidogo vidogo kama ukabila. Yani hata Uganda, nchi iliyo jaa mambo ya ukoo (clan) na ngome (kingdoms), wanaweza kuweka chini tofauti zao na kujenga umoja. Kwa wale wakenya ambao hajawahi kuja Tanzania, watu wa kawaida huku Tanzania ambao hawajawahi kuja Kenya wanashangaa kwamba what is all that fuss na ukabila wa kenya, can't they get along and forgive each other? Rwandan wamechabuana kama karanga mpaka basi, kila mtu akasema sasa wamekwisha, leo hii wanajitahidi kujaribu kusahau mabaya yaliyo tokea, na hiyo ni miaka ishirini tuu iliyopita. Kenya mkubali, hamjapata kiongozi wa kuwaambia ukweli, mtu wa kuwaambia sasa basi, lets first build a ONE NATION and then ONE COUNTRY.
 
Afu ulivyo mbishi you couldn't overlook past wachaga kuwa kabila kubwa Tz.

Mimi nita kujibu kwa namba, japo unamapenzi na kabila la wachanga (na mimi si kulaumu, kina mama wa kichaga wana vutia sana), lakini kabila lao ni dogo. Sensa ya 2010 Moshi ilikuwa na watu takriban laki tano, ukiongeza hao wengine walio zagaa kila mahali Tanzania, milioni moja hawafiki. Sasa Mwanza tuu ina watu zaidi ya million tatu na nusu, sio wote wanaishi Mwanza ni wasukuma, lakini kabila la kisukuma linachukua mikoa mitatu au three provinces. Wewe unaona wachaga wapo kila kona unasema ni wengi, kuna makabila makubwa zaidi Tanzania but kwetu hatunaga kusema wewe ni kabila gani. Kwanza kupata kimwana swali lao la kwanza lisiwe wewe kabila gani, utatupwa hapo hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom