Wakenya na Passpoti za Tanzania

Wakenya na Passpoti za Tanzania

Barbarosa kauliza swali zuri tu. Mtanzania ni nani?

Kuongea lafudhi ya Kenya haimaanishi wewe si Mtanzania. Kumwona mtu anayeongea lafudhi ya kinyarwanda au kikenya na pass ya Tanzania haimaanishi sio Mtanzania mkuu.Japo wahamiaji haramu wapo wa kutoka hizo nchi.

Hili halipo TZ tu. Nenda kenya Narok uone watazania walivyojazana na wengine wanakadi za kura za Tanzania na Kenya.
Ni kweli ila hujasema kwanini passport zitolewe kiholela
 
Nijibu kwanza swali nililokuuliza, Mtanzania ni yupi? Aliyezaliwa baada ya 1961, '64 au kabla ya hapo? Na je waliozaliwa kabla? Vipi kuhusu Wamasai Utanzania wao unaupimaje? Vipi kuhusu Wamakonde waishio Mtwara waliohamia ktk Msumbiji Utanzania wao unaupimaje? Vipi kuhusu wanaojiita Wanyamwezi ambao sehemu kubwa walihamia Unyanyembe (Tabora) kutoka Baganda (Uganda na Unyarwanda ya leo hii)?
Vipi Wahindi ambao walizaliwa wakati wa Bristish East Afrika Utanzania wao?

Ninachomaanisha kwako wewe Mtanzania ni yupi? Utanzania unaupimaje?
Leo nimekukubali. Watu wote wanaoishi mipakani wapimwe DNA zao hapo ndo tutajua kuwa mipaka iliyowekwa na wakoloni haiukutendea haki makabila husika.
 
Unathibitisha vp Utanzania wa huyo Mwafrika mweusi kama hana karatasi yoyote ile? Kwa mfano Mmasai!
Tunamuapisha tu kisheria na hiyo inatosha. Maadam ni mwafrika tayari ana sifa kubwa ya kuwa mtanzania. Isitoshe, tukitaka kufuatilia ukoo wake, alikozaliwa pamoja na uthibitisho kutoka serikali za vijiji tutapata tu. Kama ukoo wako ni wa hapa Tz ukifuatiliwa utaonekana tu. Huwezi kuwa mtanzania wakati ukoo wako mzima uko nchi nyingine, wakati hakuna serikali yoyote ya kijiji inayokutambua wewe au wazazi wako kuwa ni wazaliwa na wakazi wa pale. Ni rahisi sana kugundua sema shida ni vile tumejijengea uvivu wa kufuatilia mambo kama haya. Enzi za mwalimu mambo yalikuwa rahisi Zaidi. hakuna mahali ungepokewa bila barua ya balozi kule utokako.
 
Mbona ameshatoa njia? huyo Mkenya si amesema anatoka Tarakea uhamiaji wafatilie passport zilizotoka hv karibuni kumpata huyo mtu then wakibaini ni kweli wambane awataje na wenzake
Njia aliyotoa ni ndefu mno name ipo kiprobability zaid kwamba kama kuna maafisa uhamiaji maana yake ndo walifanyie kazi hilo sulla kama hawapo ndo imetoka hiyo kitu ambacho ninachomlaumu kwamba amekaa nao lakin ameshindwa kuchukua maamuzi ya haraka. Anyway ndivyo tulivyo watanzania hatunaga uthubutu wa kufanya jambo...!!!
 
Tunamuapisha tu kisheria na hiyo inatosha. Maadam ni mwafrika tayari ana sifa kubwa ya kuwa mtanzania. Isitoshe, tukitaka kufuatilia ukoo wake, alikozaliwa pamoja na uthibitisho kutoka serikali za vijiji tutapata tu. Kama ukoo wako ni wa hapa Tz ukifuatiliwa utaonekana tu. Huwezi kuwa mtanzania wakati ukoo wako mzima uko nchi nyingine, wakati hakuna serikali yoyote ya kijiji inayokutambua wewe au wazazi wako kuwa ni wazaliwa na wakazi wa pale. Ni rahisi sana kugundua sema shida ni vile tumejijengea uvivu wa kufuatilia mambo kama haya. Enzi za mwalimu mambo yalikuwa rahisi Zaidi. hakuna mahali ungepokewa bila barua ya balozi kule utokako.

Ni wapi Dunia hii uliona karne ya 21 Uraia wa mtu unathibitishwa kwa kuuliza Ukoo na Vijiji? Dunia nzima Makaratasi ndiyo yanayothibitisha uraia wa mtu, hivyo tulipaswa tuanzie hapo kwanza kwamba watu wote wanaozaliwa nchini kwetu wapate Cheti cha kuzaliwa na waandikishwe Serikali iwajue, awe ni Mmasai aliyezaliwa kwenye Manyata au Muhadzabe na Msandawe wote Serikali iwafikie iwaandikishe na kuwapa Cheti cha kuzaliwa kuwasajili na kuwa raia rasmi, baada ya hapo sasa ndiyo tunaweza kusema huyu ni Mtanzania yule siyo na kwa maana anaweza kuthibitisha mara moja, lkn sasa hivi ni chaos tu!
 
Sasa utajuaje kuwa ni mzaliwa wa Tz bila kuwa na ufuatiliaji wa aina Fulani kuhusu kijiji alichozaliwa?
 
Sijaribu kujustify chochote bali nimeuliza, Mtanzania ni nani? Unatumia kigezo gani kusema huyu ni Mtanzania, yule siyo? Kama ni cha kuzaliwa Je, Mmasai ni nani? Kwa maana amezaliwa kwenye Manyata huko hana karatasi yoyote ile ya kusajiliwa mahali, leo yuko Kenya kesho yuko Tanzania, sasa huyu unamuitaje? Yaani kigezo cha Utanzania ni kipi?
Bado naamini unajaribu ku-justify jambo kwa sababu swali lako hapa sio pahala pake!!! Sio pahala pake kwa sababu mada haihusiani na Mtanzania wala Watanzania bali Wakenya na pasi za kusafiria za Kitanzania!!!

Anzia hapo!!!

Lakini kukujibu swali lako, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Tanzania ya Mwaka 1995 Sura ya 357 pamoja na kanuni zake za mwaka 1997, kuna uraia wa aina tatu: Uraia wa Kuzaliwa, wa Kurithi na Kujiandikisha.

Kama mtu alizaliwa kabla ya uhuru wa Tanganyika na mzazi wake mmoja alizaliwa Tanganyika na mzazi huyu alitokana na ama raia wa Uingereza, makoloni yake au nchi zilizokuwa British Protectorates, basi mtu huyo alihesabika raia wa wa kuzaliwa wa Tanganyika.

Aidha, mtu aliyezaliwa Tanganyika baada ya uhuru nae alitambulika raia wa Tanganyika wa kuzaliwa provided mmoja wa wazazi wake alikuwa Mtanganyika!

Vile vile, mtu aliyezaliwa Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi alitambulika ni raia wa Zanzibar wa kuzaliwa provided wazazi wake hawakutokana na wale wakoloni waliokuja Afrika except German & UK! Vile vile wazazi wao hawakutokana na US, Canada, Ireland, South Africa, Sri Lanka na Australia.

Raia hao wa Tanganyika na Zanzibar ( wa kuzaliwa) hapo juu automatically walikuja kuwa raia wa Tanzania baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Likewise, mtu aliyezaliwa siku ya na baada ya muungano huyu alitambulika kama raia wa Tanzania provided mmoja wa wazazi ni raia wa Tanzania!

Tafuta mwenyewe sheria niliyotaja hapo juu ili ufahamu ni kwa namna gani mtu anatambuliwa kama Raia wa Tanzania wa kurithi na kuandikishwa...

Hivyo basi, huyo Mmasai hata kama amezaliwa Manyata kama ulivyosema na kesho yupo Kenya na mtondogoo Tanzania bado anaweza kuhesabika ni Mtanzania provided anakidhi vigezo hivyo hapo hapo juu (uraia wa kuzaliwa) au ni raia wa kurithi au kuandikishwa!

Haya, rudi kwenye mada sasa; hususani hati za kusafiria kutolewa mgahawani hali inayoibua shaka kwamba inawezekana kabisa hao watu hawana haki KISHERIA kupata hati za kusafiria za Tanzania!!!
 
vitambulisho vya kupigia kura ni janga jingine...maeneo haya ya mipakani, imekua kawaida sasa kwa wasio raia kuvipata..
 
Sasa huo ndiyo ujinga wenyewe, ni wapi Dunia hii Utaifa utambulika kwa watu kusikilizana kilugha? Vipi Mjaluo wa Kenya na wa Tanzania wanasikilizana pia, Watu wa Mara na Waluya wa Kenya wanasikilizana pia, au Wahaya/Waganda/Wanyarwanda wanasikilizana pia, ukienda Kilimanjaro Wataita wa Kenya na Wapare wa Tanzania wanasikilizana pia, Wadigo wa Tanga na wa Mombasa Kenya wanasikilizana pia, Wamasai wote wa Kenya na Tanzania wanasikilizana pia, sasa Utanzania ni upi?
Hapo suala sio lugha kwani sio kila mhaya lazima awe anakijua kihaya hapo linalozungumziwa ni utambulisho kuanzia ngazi ya taifa mpaka familia, usipotoshe mjadala.
 
Bado naamini unajaribu ku-justify jambo kwa sababu swali lako hapa sio pahala pake!!! Sio pahala pake kwa sababu mada haihusiani na Mtanzania wala Watanzania bali Wakenya na pasi za kusafiria za Kitanzania!!!

Anzia hapo!!!

Lakini kukujibu swali lako, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Tanzania ya Mwaka 1995 Sura ya 357 pamoja na kanuni zake za mwaka 1997, kuna uraia wa aina tatu: Uraia wa Kuzaliwa, wa Kurithi na Kujiandikisha.

Kama mtu alizaliwa kabla ya uhuru wa Tanganyika na mzazi wake mmoja alizaliwa Tanganyika na mzazi huyu alitokana na ama raia wa Uingereza, makoloni yake au nchi zilizokuwa British Protectorates, basi mtu huyo alihesabika raia wa wa kuzaliwa wa Tanganyika.

Aidha, mtu aliyezaliwa Tanganyika baada ya uhuru nae alitambulika raia wa Tanganyika wa kuzaliwa provided mmoja wa wazazi wake alikuwa Mtanganyika!

Vile vile, mtu aliyezaliwa Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi alitambulika ni raia wa Zanzibar wa kuzaliwa provided wazazi wake hawakutokana na wale wakoloni waliokuja Afrika except German & UK! Vile vile wazazi wao hawakutokana na US, Canada, Ireland, South Africa, Sri Lanka na Australia.

Raia hao wa Tanganyika na Zanzibar ( wa kuzaliwa) hapo juu automatically walikuja kuwa raia wa Tanzania baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Likewise, mtu aliyezaliwa siku ya na baada ya muungano huyu alitambulika kama raia wa Tanzania provided mmoja wa wazazi ni raia wa Tanzania!

Tafuta mwenyewe sheria niliyotaja hapo juu ili ufahamu ni kwa namna gani mtu anatambuliwa kama Raia wa Tanzania wa kurithi na kuandikishwa...

Hivyo basi, huyo Mmasai hata kama amezaliwa Manyata kama ulivyosema na kesho yupo Kenya na mtondogoo Tanzania bado anaweza kuhesabika ni Mtanzania provided anakidhi vigezo hivyo hapo hapo juu (uraia wa kuzaliwa) au ni raia wa kurithi au kuandikishwa!

Sheria ni makaratasi tu yaliyoandikwa, lkn uhalisia ni jambo lingine kabisa, sasa nakuuliza Uraia wa Mmasai unaithibitisha vipi?
 
Hapo suala sio lugha kwani sio kila mhaya lazima awe anakijua kihaya hapo linalozungumziwa ni utambulisho kuanzia ngazi ya taifa mpaka familia, usipotoshe mjadala.

Wamasia Je, unathibitisha vipi uraia wao? Asubuhi anakwenda kuchunga Ng'ombe Kenya Jioni anarudisha zizini Tanzania, huyo vipi?
 
Wanajamvi
Hili suala linatisha. Mimi ni member wa sehemu moja maarufu hapa Jijini. Ni sehemu ya Kula. Mnamo tarehe 31 May 2017 jioni, nilikaa meza Jirani na wakenya kama watano hivi wanaume wanne na mwanamke mmoja. Mara baada ya dakika kadhaa, alikuja jamaa mmoja aliyejumuika nao. Takriban dakika 30 baadae Yule jamaa kufika, alitoa rundo la Pasi ZA kusafiria ZA kitanzania ambazo hawa wakenya waligawiwa. Bila kupoteza muda, wakenya walitoa mfuko mweusi wa plastiki na kumkabidhi hawa jamaa na ghafla kuondoka. Nilitamani kujua kwamba zile pasi mpya zilikuwa za nini?

Sikufanikiwa ila, nilifanikiwa kuongea na mmoja wa hawa wakenya, ambaye pamoja na lafudhi yake aliniambia yeye ni mchaga wa Tarakea. Hawa Jirani zetu wananunua ardhi kwa kasi ya kutisha kutumia vitambulisho vya kitanzania. Wanajiita watanzania. Wanyarwanda pia hivyo hivyo. Ofisini kwetu kuna mdada mnyarwanda pia mwenye Pasi ya Tanzania anajiita muangaza. Nadhani kuna tishio kubwa mbeleni utakaotokana na watu kujizolea hizi passport za kutanzania
kuna haja ya wakuu kuwajibika kusafisha uhamiaji. raia tutoe taarifa kama hii ifike mahali rasmi. ifike mahali hata kama mgeni kafanikiwa kudhibiti ardhi ya tanzania kwa hila akijulikana anyang'anywe mara moja.
 
Tena hii speed ya wachina ni hatari sana na wanajifunza lugha ya kiswahili kwa haraka sana. Nadhani wangekuja kama wawekezaji ila sio wafanyabiashara ndogo ndogo. Hizi kazi watuachie wabongo.
Lazima tulinde taifa letu lakini pia lazima tupokee wageni (Kwa njia halali) ili tupate ushindani ni akili na mbinu mpya tuweze kuiendeleza nchi yetu. Wamarekani wameendelea sana kutokana na tabia yao ya kukaribisha wageni toka kila pembe ya dunia.
 
Sheria ni makaratasi tu yaliyoandikwa, lkn uhalisia ni jambo lingine kabisa, sasa nakuuliza Uraia wa Mmasai unaithibitisha vipi?
Usitake kuhamisha mada kiasi kwamba mwelekeo wote wa thread umebadilika!!

Awali umeuliza Mtanzania ni nani na nimekujibu... hivi sasa unataka kufahamishwa utafahamu vipi kwa Mmasai X ni Mtanzania na Y sio Mtanzania! Kwa maelezo yako haya unathibitisha kwa mara nyingine kwamba kuna jambo unajaribu ku-justify!!!

Mada iliyopo mezani ni ile ya hati za kusafiria kutolewa mgahawani hali inayoibua shaka kwamba inawezekana kabisa hao watu hawana haki KISHERIA kupata hati za kusafiria za Tanzania!!!

RUDI KWENYE MADA!!!!
 
Sheria ni makaratasi tu yaliyoandikwa, lkn uhalisia ni jambo lingine kabisa, sasa nakuuliza Uraia wa Mmasai unaithibitisha vipi?
kila masai anajua yeye ni wa wapi kutoka na sehemu aliyozaliwa. tena siku hizi wanadhibitiana kutokana na uhaba wa ardhi.
 
Usitake kuhamisha mada manake kiasi kwamba mwelekeo wote wa thread umebadilika!!

Awali umeuliza Mtanzania ni nani na nimekujibu... hivi sasa unataka kufahamishwa utafahamu vipi kwa Mmasai X ni Mtanzania na Y sio Mtanzania! Kwa maelezo yako haya unathibitisha kwa mara nyingine kwamba kuna jambo unajaribu ku-justify!!!

Mada iliyopo mezani ni ile ya hati za kusafiria kutolewa mgahawani hali inayoibua shaka kwamba inawezekana kabisa hao watu hawana haki KISHERIA kupata hati za kusafiria za Tanzania!!!

RUDI KWENYE MADA!!!!

Siyo kweli, Wamasai nimekupa kama mfano tu, lkn sehemu kubwa ya watu waishio Tanzania hawako documented mahali popote pale, hivyo uthibitisho pekee ambao tunautegemea ni wa mdomo na kuuliza watu, sasa karne ya 21 hakuna nchi inafanya hivi, ilipaswa wote tuwe na documents na kumbukumbu zinazotutambulisha kama sisi ni Watanzania, isitoshe sehemu kubwa ya wanaoishi hapa Tanzania uthibistiho pekee ni labda kama ni Mkristo na alibatizwa sasa Kanisa linakuwa na kumbukumbu lkn kinyume na hapo hakuna mahali unapoweza kuthitisha rasmi kwa makaratasi, hivyo tuanzie hapo kwanza kuwaingiza watu wote kwenye mfumo, ndiyo tuanze kujishuguliha na kuuliza nani Mtanzania na yupi siyo!
 
Wanajamvi
Hili suala linatisha. Mimi ni member wa sehemu moja maarufu hapa Jijini. Ni sehemu ya Kula. Mnamo tarehe 31 May 2017 jioni, nilikaa meza Jirani na wakenya kama watano hivi wanaume wanne na mwanamke mmoja. Mara baada ya dakika kadhaa, alikuja jamaa mmoja aliyejumuika nao. Takriban dakika 30 baadae Yule jamaa kufika, alitoa rundo la Pasi ZA kusafiria ZA kitanzania ambazo hawa wakenya waligawiwa. Bila kupoteza muda, wakenya walitoa mfuko mweusi wa plastiki na kumkabidhi hawa jamaa na ghafla kuondoka. Nilitamani kujua kwamba zile pasi mpya zilikuwa za nini?

Sikufanikiwa ila, nilifanikiwa kuongea na mmoja wa hawa wakenya, ambaye pamoja na lafudhi yake aliniambia yeye ni mchaga wa Tarakea. Hawa Jirani zetu wananunua ardhi kwa kasi ya kutisha kutumia vitambulisho vya kitanzania. Wanajiita watanzania. Wanyarwanda pia hivyo hivyo. Ofisini kwetu kuna mdada mnyarwanda pia mwenye Pasi ya Tanzania anajiita muangaza. Nadhani kuna tishio kubwa mbeleni utakaotokana na watu kujizolea hizi passport za kutanzania
Hili linaogofywa something has to done.
Haraka iwezekanvyo.La sivyo tutakuwa too late kujiokoa.
 
Siyo kweli, Wamasai nimekupa kama mfano tu, lkn sehemu kubwa ya watu waishio Tanzania hawako documented mahali popote pale, hivyo uthibitisho pekee ambao tunautegemea ni wa mdomo na kuuliza watu, sasa karne ya 21 hakuna nchi inafanya hivi, ilipaswa wote tuwe na documents na kumbukumbu zinazotutambulisha kama sisi ni Watanzania, isitoshe sehemu kubwa ya wanaoishi hapa Tanzania uthibistiho pekee ni labda kama ni Mkristo na alibatizwa sasa Kanisa linakuwa na kumbukumbu lkn kinyume na hapo hakuna mahali unapoweza kuthitisha rasmi kwa makaratasi, hivyo tuanzie hapo kwanza kuwaingiza watu wote kwenye mfumo, ndiyo tuanze kujishuguliha na kuuliza nani Mtanzania na yupi siyo!
Sawa, RUDI KWENYE MADA au kuwa wazi ni nini hasa unachojaribu ku-justify !!

Hayo yote uliyozungumzia sio sehemu ya mada! Na kama unadhani ni muhimu kujadiliwa basi ungeanzisha mada nyingine lakini iliyopo mezani ni hii hapa:
Wanajamvi
Hili suala linatisha. Mimi ni member wa sehemu moja maarufu hapa Jijini. Ni sehemu ya Kula. Mnamo tarehe 31 May 2017 jioni, nilikaa meza Jirani na wakenya kama watano hivi wanaume wanne na mwanamke mmoja. Mara baada ya dakika kadhaa, alikuja jamaa mmoja aliyejumuika nao. Takriban dakika 30 baadae Yule jamaa kufika, alitoa rundo la Pasi ZA kusafiria ZA kitanzania ambazo hawa wakenya waligawiwa. Bila kupoteza muda, wakenya walitoa mfuko mweusi wa plastiki na kumkabidhi hawa jamaa na ghafla kuondoka. Nilitamani kujua kwamba zile pasi mpya zilikuwa za nini?
Acha ujanja ujanja kijana... mada ni hiyo hapo juu! Twende kazi...
 
Back
Top Bottom