BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Mimi ni Mkazi wa Kijiji cha Mekomariro Wilaya ya Bunda, naomba jamii ijue kuwa kuna ugomvi wa ardhi kati Wananchi wa Kijiji chetu na Wananchi wa Kijiji cha Wilaya ya Serengeti, mpaka sasa kuna ugomvi mkubwa, watu wamechomana mishale.
Huu mgogoro hauwezi kumalizika kwa kuwa kuna viongozi au viongozi wapo nyuma ya kinachoendelea na wamekuwa wakifanya mambo kwa maslahi yao.
TAMKO LA POLISI
RPC Mara Salum Morcase amesema “Kinachoendelea ni amani, vurugu zimedhibitiwa, upande wa Mekomariro wamejeruhiwa watu watano, mmoja yupo hospitali, wengine wamepata majeraha madogo na walienda zahanati wakapata dawa wakarejea nyumbani, upande wa pili Kijiji cha Ryaming’orori aliyejeruhiwa ni mmoja tu naye alipata majeraha machache akarejea nyumbani.
“Vurugu zilitokea jana mchana (Septemba 17, 2013), mgogoro huo ni wa muda mrefu, kuna timu imeenda eneo la tukio kufuatilia na baadaye nitapata ripoti kamili.”