KERO Wakazi wa Matosa Uzaromoni – Goba tuna changamoto ya Kalavati, huu mwaka wa pili TARURA wanakuja kupiga picha wanaondoka

KERO Wakazi wa Matosa Uzaromoni – Goba tuna changamoto ya Kalavati, huu mwaka wa pili TARURA wanakuja kupiga picha wanaondoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
121
Reaction score
218



Tunaomba ujumbe wetu huu ufike hadi kwa Waziri wa Ujenzi, kwa muda wa Miaka miwili, sisi Wananchi wa Matosa Uzaromoni, Mtaa wa Mikumi, Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam tunapitia changamoto kubwa ya usumbufu wa maji ya mvua kutokana na udogo wa ‘Kalavati’

Tumelalamika sana, tumefikia hatua hadi ya kuandika barua kwa Mamlaka ya TARURA, kila tunapofanya hivyo wanakuja kupiga picha kisha wanasema watashughulikia, wakiondoka hawarudi hadi twende tena, tukienda kama kawaida wanakuja kupiga picha na kuondoka.

Makazi yetu yanazidi kuharibika, usalama wa nyumba na miundombinu mingine ni mdogo kutokana na maji kupita juu ya Barabara kutokana na njia ya Kalavati kuzidiwa na maji.

Kama mnavyojionea kwenye picha na video hyo ndio adha tunayopitia, wakati huu wa mvua mambo ndio huwa mabaya zaidi.
WhatsApp Image 2025-04-11 at 16.06.58_e3cd8a63.jpg

Screenshot 2025-04-11 171141.jpg

Barua yetu kwa Mamlaka husika
WhatsApp Image 2025-04-11 at 13.01.48_60d642ea.jpg

WhatsApp Image 2025-04-11 at 13.01.56_9c665885.jpg

WhatsApp Image 2025-04-11 at 13.01.50_fbf2f31b.jpg

Pia soma ~ Wakazi wa Matosa - Goba, Mwaka wa 3 tunabembeleza kujengewa kalavati, TARURA wanakuja kupiga picha wanaondoka
 
Back
Top Bottom