Wakazi wa Dar badilikeni

Wakazi wa Dar badilikeni

Ndugu yangu ulipotaja VIROBA umegusa point sana.

Sasa hivi Dar watu wanakunywa VIROBA kama maji. Unakuta mtu ananuka KIROBA na amechoka. Tena yupo kwenye public service.

Sijui serikali inatazama vipi swala la Viroba mijini.
kwakweli wenzetu wana matatizo!
 
hahahah kweli wanaume wa dar ni shida pia mimi nimesikitika sana dah mtu mmoja watu wanamtolea macho hawatafuti hata silaha za jadi maana hata bunduki haaihitajiki looooooo kweli shame on them.

Mkuu mimi nadhani pale buguruni ni mbabe,anafahamika na pengine anaweza kuwa anagenge lake la majangiri wenzie,ni mtu wa matukio....so hii ikitokea na kuota mizizi sehemu ambazo hawana ushirikiano na ulinzi wa kutosha tabia hizi uota miziz,pengine huyu jamaa nafahamiana na watu wa polisi.....watu wanamuogopa pengine ni mtu wa visasi.....,hofu yangu kwanini nasikia mpaka mkuu wa kituo kasimamishwa kazi juu ya ishu hii,tusahidiane kuwaza wote kwa mbaliiii!
 
Kwanza kuwatofautisha wanaume wa Dar na dada zao labda uwaambie wavue nguo uangalie jinsia zao maana wote wanapaka mikorogo na lipstick
Dah! We umeua kabsa. Lakin na mi nilienda dar salun ya kiume walipomaliza kuninyoa nywele na kuniosha mdada akataka kunipaka yale mafuta sijui ya kung'arisha midomo na kuweka wekundu hivi. Kidogo nimvulie aone jinsi yangu. Akanishangaa et mi mshamba. Alafu na nguo za wanaume wa dar ....bas tu. Yan surual na skin jeans hamna tofaut. Hata uandishi wao mwanaume wa akiongeza neno ..loh!
 
Mwanaume wa Mkoani unaporwa na mwanaume mwenzio unashangaa!.
 
mi naangalia walet yake tu.. mengine hayanihusu
Kwa hiyo yale mengine unayapata kwa wa mikoani? Ila mama angalia jamaa yako anaweza akakunyang'anywa akiwa amekunja mikono tu bila msaada!
 
Naongea haya kwa uchungu mkubwa ,kuhusu wanaume na wakazi wa dar kwa ujumla .

Mnamo mwaka 2013 nilikuja dar kwa mara ya kwanza nikijiunga chuo kikuu UDSM ,
Siku moja majira ya saa 9 mchana nikiwa narudi hosteli za mabibo nilipita maeneo ya SONGAS kwenye mitambo ya umeme, hakika ilikuwa saa 9 kweupe nilikwapuliwa wallet na kunyang'anywa Pesa zangu kiasi cha 50000, nilipiga kelele kuhitaji msaada , lakini wakazi hasa Wanaume wa darisalama waliniangalia tu huku wakinipita na kumuacha yule kibaka akitamba ,..

Iliniuma sana kwani sikuwahi kudhani kwamba Wanaume na wakazi wa dar wapo hivo, nilijiuliza ni uoga au ndio kila mtu na maisha yake, kwamba kila mtu kaja kutafuta.

Niliondoka na kwenda polis kutoa taarifa waje wawakamate wale vibaka . Nilienda kituo cha polis ubungo ndani ya stendi , cha ajabu nao walinipiga dana dana wakitaka hela ndio wakamkamate..

Nikaondoka nikaenda kituo cha polis urafiki

Sikupata msaada.

Nikarudi ubungo mataa nikiwa nimechoka nisielewe tabia za wakazi wa dar.

Bahati nzuri nikakutana na mwanajeshi nikamueleza tukio zima, tukafunga safari hadi kwa hao vibaka , akakamatwa na kunirudishia pesa yangu.

SASA kuna tukio limetokea huko buguruni , kijana mmoja ansjiita Scorpion anachoma watu visu na kupora , mchana kweupe lakini ...wanaume wa dar wanakuacha hawatoi msaada .


Ni juzi amemtoboa mfanyabiashara mmoja macho na kumchoma visu lakini watu walishuhudia na hawakutoa msaada wowote.

Polis wapo siku zote wanajua kuhusu huyu kibaka...

Mpaka vyombo vya habar vimepiga kelele ndio katiwa nguvuni


NINACHOSHANGAA MBONA MIKOANI KUNA USHIRIKIANO TOFAUTI NA HUKU DAR?

HEBU WANAUME NA WAKAZI WA DAR MBADILIKE SOTE NI WATANZANIA
........huku mikoani watu kaa hao ni kugeuzwa majivu tyu bila ubishi............. !!!!!!!
 
Wanaume wa dar, badiliken toen msaada maradhi mnaficha wenyewe.
 
,,,,,,,,, sio nguvu za kuokoa tu hata 6X6 nasikia taabu ...duuh polen saana
 
Wanaume wa dar in shida,ataa ukimkopesha ela yako,harudishi.bored.badilikeni.
 
Inavyoonyesha uyo mwanajashi aliye kusaidia hakuwa mwansume wa dar
 
Dar n wavulana wanaume tupo mkoan
 
Back
Top Bottom