Wakazi wa Dar badilikeni

Wakazi wa Dar badilikeni

ila si ukweli kwamba ni dar tu ambapo unakabwa na watu wanakuangalia mpaka uumizwe

arusha na moshi pia kuna baadhi ya maeneo hata upige yowe hakuna anayejitokeza kutoa msaada
 
simwonei huruma yani nafurahi jinsi wanaume wa dar wamefanya hadi analia mama,.... nashindwa kuweka aisee
Watakua wanaume wa mikoani ndo wametoa msaada huo, hawa wa wanaume wa Dar hawawezi kabisa!
 
Hili sio dar tu hata mbeya nako hakufai mke wangu kaporwa saa mbili asubuhi kweupe pale uyole hata kusaidia hakuna Watz hatusaidiani siku hizi unaibiwa watu wanakutolea mimacho tu
 
Naongea haya kwa uchungu mkubwa ,kuhusu wanaume na wakazi wa dar kwa ujumla .

Mnamo mwaka 2013 nilikuja dar kwa mara ya kwanza nikijiunga chuo kikuu UDSM ,
Siku moja majira ya saa 9 mchana nikiwa narudi hosteli za mabibo nilipita maeneo ya SONGAS kwenye mitambo ya umeme, hakika ilikuwa saa 9 kweupe nilikwapuliwa wallet na kunyang'anywa Pesa zangu kiasi cha 50000, nilipiga kelele kuhitaji msaada , lakini wakazi hasa Wanaume wa darisalama waliniangalia tu huku wakinipita na kumuacha yule kibaka akitamba ,..

Iliniuma sana kwani sikuwahi kudhani kwamba Wanaume na wakazi wa dar wapo hivo, nilijiuliza ni uoga au ndio kila mtu na maisha yake, kwamba kila mtu kaja kutafuta.

Niliondoka na kwenda polis kutoa taarifa waje wawakamate wale vibaka . Nilienda kituo cha polis ubungo ndani ya stendi , cha ajabu nao walinipiga dana dana wakitaka hela ndio wakamkamate..

Nikaondoka nikaenda kituo cha polis urafiki

Sikupata msaada.

Nikarudi ubungo mataa nikiwa nimechoka nisielewe tabia za wakazi wa dar.

Bahati nzuri nikakutana na mwanajeshi nikamueleza tukio zima, tukafunga safari hadi kwa hao vibaka , akakamatwa na kunirudishia pesa yangu.

SASA kuna tukio limetokea huko buguruni , kijana mmoja ansjiita Scorpion anachoma watu visu na kupora , mchana kweupe lakini ...wanaume wa dar wanakuacha hawatoi msaada .


Ni juzi amemtoboa mfanyabiashara mmoja macho na kumchoma visu lakini watu walishuhudia na hawakutoa msaada wowote.

Polis wapo siku zote wanajua kuhusu huyu kibaka...

Mpaka vyombo vya habar vimepiga kelele ndio katiwa nguvuni


NINACHOSHANGAA MBONA MIKOANI KUNA USHIRIKIANO TOFAUTI NA HUKU DAR?

HEBU WANAUME NA WAKAZI WA DAR MBADILIKE SOTE NI WATANZANIA

Kama ww ni mwanaume unaejiamini aka wa mkoani unakubalije kupokonywa pesa zako na mwanaume mwenzako
 
Kule kwetu....kama kukitokea mtu anasumbua hapo kijijini.....basi wazee wa kijiji wanamfanyia dawa ili kumuondosha hapo kijijini.....au la wanamtia uchizi....huku kazi yake ikiwa ni kulima tu......kila siku yeye ni shamba tu.....iwe jua iwe mvua.....
 
Ndio maana vijana wa Dar kila siku wanakuwa machizi.....kutokana na tamaa zao.....
 
mkuu mi naona tubadilishane tu hata kwa wiki moja wa mikoani tuje dar
Aseee naona tuwe tunaheshimiana kabisaaaa tusifike hatua ya kudharirishana hivi. Yani na akili zote hizi unipeleke dar?? Labda nie mahututi aseee



Hilo jiji nalichukia kama dalili za umasikini
 
Back
Top Bottom